Kuzaa kwa uchungu haitoshi, wameona waingilie na Adhabu ya kula kwa jasho ya wanaume

Kuzaa kwa uchungu haitoshi, wameona waingilie na Adhabu ya kula kwa jasho ya wanaume

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Kwa mujibu wa simulizi za pale bustani ya Eden, baada ya Adam na Hawa kula tunda lililokatazwa, Hawa akapewa adhabu ya kuzaa kwa uchungu, huku Adam akiambiwa atakula kwa jasho la uso wake. 😂

Sasa cha kushangaza, wanawake wameona adhabu yao haitoshi! Wameamua kuingilia na adhabu ya mwanaume pia. 🤣

Yaani kuzaa kwa uchungu haitoshi, sasa wanataka na kula kwa jasho! Mwanamke anafanya kazi, anatafuta pesa, anajenga nyumba, ananunua gari.

Ikumbukwe Purpose ya Mwanamke kuumbwa ilikuwa kwa ajili ya Adamu, yani kuwa msaidizi wa Adamu, yani kwa lugha nyingine kuwa chini ya Adamu, ndio maana kamili ya msaidizi. Na watakuwa mwili mmoja maana yake ni kuwa na familia.

Lakini siku hizi Mwanamke anataka asiwe chini ya Mwanaume, awe huru (Independent Woman) afanye kila kitu kiwe chake tu, wengine hawataki ndoa kabisa wanona watabanwa, wanadai talaka. Sijawai kusikia Single Father, naonaga tu Single Mothers. Unakuta kila mtoto na Baba yake.

Swali ni moja tu: Mwanamke anataka haki sawa au ameamua kutekeleza adhabu zote mbili kwa niaba ya familia? 😂😂🔥
 
Lakini siku hizi Mwanamke anataka asiwe chini ya Mwanaume, awe huru (Independent Woman) afanye kila kitu kiwe chake tu, wengine hawataki ndoa kabisa wanona watabanwa, wanadai talaka. Sijawai kusikia Single Father, naonaga tu Single Mothers. Unakuta kila mtoto na Baba yake.

Zama zimebadilika.

Zaman Mwanamke alijiona kiumbe dhaifu kwasababu kazi nying za zaman zilikuwa zinatumia nguvu na ujasiri (uvuvi, uwindaji, kubeba vitu vizito, kulima, nk)

Sasa kwa zama hizi kazi nying wanawake wanazimudu.

Na Wanapata hela hata zaidi ya wanaume. mwanamke yuko na hela zake alafu utakuta mwanaume anamzingua kwa mahusiano.
Anaona ya nn. Bora amani ya moyo.
Na as long as anajimudu.
Anakutema mchana kweupe.

Na jamii pia imebadilika.
Single mothers au kuona mwanamke hajaolewa sio big deal.
Ni jambo la kawaida na halimuondolei Heshima yake kwa jamii. Tofaut za zamani.

Waswahili wanasema, Kila zama na Mtume wake.
 
😀😀😀 wenye akili ndiyo watakuelewa.

Ila kuna watu wataanza kuzaa kwa uchungu soon 🤣🤣

literally hata huu uzi ni uchungu(iamsorry 😉)
 
Back
Top Bottom