Kwa mujibu wa simulizi za pale bustani ya Eden, baada ya Adam na Hawa kula tunda lililokatazwa, Hawa akapewa adhabu ya kuzaa kwa uchungu, huku Adam akiambiwa atakula kwa jasho la uso wake. 😂
Sasa cha kushangaza, wanawake wameona adhabu yao haitoshi! Wameamua kuingilia na adhabu ya mwanaume pia. 🤣
Yaani kuzaa kwa uchungu haitoshi, sasa wanataka na kula kwa jasho! Mwanamke anafanya kazi, anatafuta pesa, anajenga nyumba, ananunua gari.
Ikumbukwe Purpose ya Mwanamke kuumbwa ilikuwa kwa ajili ya Adamu, yani kuwa msaidizi wa Adamu, yani kwa lugha nyingine kuwa chini ya Adamu, ndio maana kamili ya msaidizi. Na watakuwa mwili mmoja maana yake ni kuwa na familia.
Lakini siku hizi Mwanamke anataka asiwe chini ya Mwanaume, awe huru (Independent Woman) afanye kila kitu kiwe chake tu, wengine hawataki ndoa kabisa wanona watabanwa, wanadai talaka. Sijawai kusikia Single Father, naonaga tu Single Mothers. Unakuta kila mtoto na Baba yake.
Swali ni moja tu: Mwanamke anataka haki sawa au ameamua kutekeleza adhabu zote mbili kwa niaba ya familia? 😂😂🔥