Kuzaliwa mwanaume ni hatia

Kuzaliwa mwanaume ni hatia

Ottu Jazz Band Msondo Ngoma Baba ya Muziki Waliimba wimbo Ajali ukiwa na Maneno,"Ukizaliwa mwanaume kaa ujue kila kitu kwako itakua tabu, wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika"
Kuna shoga alikua maarufu Moshi miaka ya nyuma maeneo ya kindoroko pale mjini Moshi sasa marehemu alikua akiitwa KINJE. Siku Moja hii nyimbo ilipigwa akasema " Mimi nilijua mapema ndio maana nimejitoa huko" 😂😂😂😂
Mwanaume kweli ukizaliwa jua uko peke yako hata watoto wakija kuwatembelea hela utapewa mbele ya mkeo ila mkeo atapewa hela na mtoto chumbani au jikoni huko.
Mke wako anaweza kuamua kuwatembelea watoto na kukaa hata miezi SITA na utabaki peke yako.
Ndio maana mwanaume unatakiwa ukaze kivyako na maisha yako ya uzeeni uyaandae mapema.
 
Duuh nimeamini wanaume wa siku hizi mnapenda sana kulialia na kuplay victims, pale jamii inapowatukana wanawake na inapowasifia wanaume kwa kufanya kitendo kimoja mnachokiita umalaya eti kisa jinsia zao na maumbile yao mbona huwa hamsemi, kwanza mnastahili hayo kila jinsia ina angle yake ambayo inaandamwa ila kiujumla wanawake ndio wanaandamwa sana ni vile tu siku hizi hawajali wameamua kujibu mapigo na kuacha kulalamika
 
Duuh nimeamini wanaume wa siku hizi mnapenda sana kulialia na kuplay victims, pale jamii inapowatukana wanawake na kuwasifia wanaume kwa kufanya kitendo kimoja 'umalaya' eti kisa jinsia zao na maumbile yao mbona huwa hamuongei, kwanza mnastahili hayo kila jinsia ina angle yake ambayo inaandamwa ila kiujumla wanawake ndio wanaandamwa sana ni vile tu siku hizi wameamua kujibu mapigo na kuacha kulalamika wamewaachia nyie
Kapeace njoo huku tayari kasi ya mashambulizi imeongezeka.
 
Ukiangalia topics za natafuta ajira kwa juu juu unaweza dhani anachukia wanawake, ila kwa asilimia kubwa anaongea ukweli Anita Makirita
Ukweli gani, anachukia wanawake huyo...mtu balanced anaonekana hata michango yake...wewe kila siku kuponda wanawake...huyu mtu hayuko emotionally balanced na mtakaomfuata mtaishia kuwa na mahusiano rocky kama yeye ..
 
Ukweli gani, anachukia wanawake huyo...mtu balanced anaonekana hata michango yake...wewe kila siku kuponda wanawake...huyu mtu hayuko emotionally balanced na mtakaomfuata mtaishia kuwa na mahusiano rocky kama yeye ..
Aisee...
 
Wee thubutuu!!! Huyo mwizi mwanamke angemwibia mwanamke mwenzake uone angevojambishwa na huyohuyo mwanamke mwenzake, adui wa mwanamke ni mwanamke.

Kuna mwizi mwanamke alimwibia mwanamke mwenzake sim kwenye gari alikula kichapo Cha wanawake wenzake na maneno makali juu, afu wanaume wakakaa pembeni kwanza.

Kuna na yule mwizi mwingine wa kike aliyeiba mume wa mwanamke mwenzake majuzi, walimfanya kitu mbaya mpaka akaomba maji ya kunywa na hakupewa.

Wizi ni mbaya tuu hauangalii jinsia jichanganye useme wee ni wa kike utahurumiwa uone Cha moto, waweza jikuta unakula kiberiti bila kutegemea na uanamke wako, ohooooo Dunia haieleweki hii.
Sasa kichapo cha mwanamke mwenzie nacho unakiita kichapo, si wataishia kuvuana mawigi na kuchaniana nguo tu.
 
Kipindi tupo shule tuliwahi kuambiwa wake zetu bado hawajazaliwa au kuanza hata shule. Tukajikuta sisi tunajua sana tukapuuzia tulichoambiwa. Picha likaja tupo mtaani sasa, tunajitafuta na hao tunaowaita wapenzi wetu ambao hatujaachana sana umri. Msoto umepiga na wao wameamua kwenda kwa wenye hela na waliojipata, na wengine imebidi tuwaache waende maana hali imezidi kuwa tafrani dah. Ndio tukajua kumbe hatujui. Tumekuja kujipata tunapata vitoto vya 2000 ambao kimsingi ndio wa kuja kuwaoa.
Kijana usipoteze muda, nguvu wala pesa na mwanamke wa age yako. Mwenzako kutoboa ni suala la kulala na kuamka tu lakini wewe kutoboa ni mchakato.
 
Mleta mada andiko hili pamaja na mengi mazuri na yenye mafunzo uliyo wasilisha hapa kwa manufaa yetu kama vijana na wote kwa ujumla una ushauri gani kwetu tulio na watoto wa kike ambo kesho watakuwa wadada ambo ni kama hawa tunao waongelea hapa?
Natanguliza shukurani Natafuta Ajira
Kwa kizazi tulichopo kwa kusena kweli suala la malezi ni changamoto, binafsi nafikiri tuwafundishe heshima na uthubutu ws kujitegemea tangu wakiwa wadogo pia tusiwaachie uhuru usiokua na mipaka(lengo sio kuwabana lengo ni kuwalinda).
 
Hii Iko kwenye nature hata lijogoo huponda majogoo wengine na kulisha mitetea!
Ila binafsi huwa napenda sana kuwapa vipaumbile vidume wenzangu kutokana na niliyoyapitia kama mwanaume
Wakati tuliopo tujitahidi kutumia zaidi logic. Tufate nature pale ambapo hakuna namna nyingine.

Mfano, nature inataka nimuhudumie mwanamke lakini logic itakuja na maswali kwanini nimuhudumie? hana ndugu? ni mtoto yatima? ni mlemavu asiweza kufanya kazi?

Binadamu wamebuni mbinu nyingi za kufanya exploitation kupitia iyo nature, so you have to be very careful.
 
Wanawake hawana tatizo lolote, tatizo ni sisi wanaume tutawalaumu bure ila mwisho wa yote tatizo ni sisi. Mwanamke anaishi kama kioo atakuonesha tu ujinga wako ulivyo utake usitake kwa kujua au kutojua. Amekuja kukusaidia wewe (Msaidizi) Kwa maana nyingine Mwanaume ndiye mwenye kazi haswaa..

Ni jukumu la Mwanaume kukubali kubadilika ukishaoneshwa ujinga wako badala ya kulaumu, unalaimu nini sasa kama ukioneshshwa tatizo? Mi nadhani ukishaoneshwa tatizo suala la msingi ni kukubali kuwajibika wewe kama wewe siyo kutafuta wa kumlaumu.

Mwanamke kama ukikaa naye kizembe atakuonesha tu uzembe wako utake usitake, kuna watu tulishapitia hayo maisha tukajifunza ila Kwa kuumia sana. Unaweza ukalaumu kila mtu ila ukikaa peke yako kimya mahali tulivu kabisa na kujichunguza utabaini shida siyo wanawake.

Mwanamke ameumbwa kufanya mambo yake kwa hisia sana yaani karibu kila jambo alifanyalo anaangalia anajisikiaje kwanza. Anatawaliwa sana na hisia lakini Mwanaume anapaswa kufanya mambo yake bila kuangalia anajisikiaje. Hata kama hali ni ngumu vipi hata utamaduni unatufundisha kutojisikiliziasikilizia.

Maana ya hakuna anyempenda Mwanaume ni ukweli kuwa Mwanaume hapaswi kujionea huruma katika hali zote. Ni kiumbe aliyeumbwa Kwa mfano wa Mungu. Jiulize ni nani anamuonea Mungu huruma licha ya yeye kutupa kila kitu na bado tunamwomba na wengine tunakufuru kabisa.

Kuzaliwa Mwanaume ni sifa ya kipekee na bahati Kwa sababu Mwanaume ni alama ya uwezekano wa chochote kile. Mwanaume ni mtoaji, Mwanaume ni mlinzi n.k. Mwanaume hakuumbwa kupokea ila kutoa hata maumbile yetu ya uzazi yamekaa mkao wa kutoka ndani kuja nje tofauti na wenzetu ambao maumbile yao ni ya kupokea (yanaingia ndani).

Hata ujauzito Mwanamke hupewa na kuutunza ndani miezi tisa kisha huja kuonesha alichokuwa amekitinza ni nini. Hii inaonesha kuwa wenzetu wameumbwa kutoneshea tulichowapa ni kitu gani? Wanawake wengi unaowaona wanaonesha walichowekewa na wanaume.

Kwa mtazamo wangu Mwanaume kutoa ndiyo sifa yake ya asili na jukumu lake kuliko kupokea. Tusiogope tunapoona kila upande unatuhitaji kutoa Kwa sababu ndilo jukumu letu na siyo laana au hatia.
Inaendelea........
 
Back
Top Bottom