1. Hapana aliyekomba jina la kiarabu, mbona waislamu kutoka nje ya Arabia wako wengi kuliko hao waarabu wenyewe? Mfano ni Indonesia, na wao wana majina yao ya kikabila yao. Halafu baadhi ya majina ya kiarabu wala siyo ya kiislamu, na yako mengi tu. Mfano hata yule aliyekuwa Waziri wa Iraq Tariq Aziz alikuwa mkristo, kwa hivyo hayo ni maoni yako finyu tu.
2. Kanzu siyo uislamu hata kidogo kwani hata mapadri wanavaa, au kwa kuwa zao zimerembwa rembwa ndiyo unaona siyo kanzu? Mbona nyinyi munavaa suti mulizoletewa na wazungu?
3. Hiyo unayosema biriani ni chakula cha waarabu kwa kweli umekosea kwani asili ya chakula biriani na pilau ni India, hata hao waarabu wenyewe wameiga. Labda bokoboko.
4. Hiyo dufu ni ngoma tu kama vile munavyoiga ngoma za akina Michael Jackson na wenzake.
5. Kuvaa nguo wakati wa ndoa pia ni mbwembwe tu, kuna wanaovaa kanzu na jambia na kuna wanaovaa suti zilizoletwa na wabeba biblia.
6. Hata quran kuwa kwa lugha ya kiarabu si usome uelewe kilichoandikwa? Tafsiri zipo hata kwa kiswahili anaetaka kuelewa ataelewa tu, tena tafsiri zipo kwa kila lugha, kichina, kizungu na lugha nyingine nyingi.
Hebu jaribu kutafsiri sentensi moja tu ya kizungu kwenda kiswahili, kizaramo, kichaga, kihaya na kisukuma halafu uone zitakavyokuwa na maana tafauti.