uarabu una mila na desturi zake na uislam una sheria zake lakini huku kwenye uislam tumekomba mpaka uarabu, nimeuliza swali uislamu ni uarabu?
Majina - yani mpaka jina la ukoo linanyofolewa.
Kutukuza waarabu - kuwa na dhana potofu kwamba waarabu ni ndugu zake Mwenyezi Mungu, kuiita ngozi ya kiarabu ngozi ya mtume, mwarabu akitaka kitu flani ni ngumu kumkatalia, akikosea kitu flani rahisi kumsamehe.
Mavazi - Kudhani kwamba kanzu ni uislam
Dufu - Ngoma hii wengi huipiga hasa kwenye sherehe kudhani ni uislam
taratibu za Kuoa - Kuvaa kanzu huku kiunoni kuna jambia la vitani kudhani ndio uislam.
Vyakula - kikiwa kina asili ya uarabuni mfano biriani kitapewa heshima zaidi kuliko pilau
lugha - Kusoma quran kwa kiarabu hata kama huelewi, kusalimiana kwa kiarabu, n.k.
mtume angekuwa mchina tungevaa kishaolin temple na tungekuwa na vidoti sita au kadhaa kwenye makomwe yetu ?
Biriani sio cha kula cha kiarabu na wala mtume hajakula wali, ubwabwa, pilau, biriani na vifananiavyo. Biriani inatoka India na nchi za karibu na hapo, hujasoma wewe shule ya Msingi Burma na mpunga?
Kusalimiana kiarabu ama Quran kuwa kiarabu haimaanishi unafata mila ya kiarabu, hio ni Sheria ya kiisilamu, mwarabu mkristo hana mila ya Quran ama Salamu ya kiisilamu.
Kanzu ni vazi la mitume, limevaliwa na mitume yote musa, Yesu wote wamevaa kanzu mpaka leo viongozi wa kikristo wanavaa kanzu.
kanzu ya Papa John wa pili.
Pia Dufu ni mila za Masufi ambazo nyingi zinatoka India, misri, uturuki etc na imeenea sana wakati wa Ottoman Empire, ambayo hata haikua Empire ya kiarabu. waarabu wana mila zao asili vigoma vyao, magitaa na flute, siku hizi Internet nje nje ingia youtube kujua nyimbo za kiasili za kiarabu.
Moja ya Nyimbo maarufu ambazo zime survive toka Enzi hizo hadi leo ni
-lamma baada yatathanna
-taala Al badr alayna
Kuna orchestra ya kiarabu huwa wana recreate hii kama upo interested kusoma
kama una bundle angalia hizo video mbili utaona mziki wa kiarabu.
Ukimaliza angalia na hii video ya Sufi
sikiliza hicho kigoma halafu niambie huku tunapiga kigoma gani