umeongea ukweli mkuu ambao wanawake wengi hawataki kuambiwa, nimesha wai kukombiwa live kabisa mkuu, nilienda mpaka kujitambulisha kwao, baadae nikamuambia kwanini tusifunge ndoa kanisani tukarudi nyumbani tukaweka bajeti ya watu 80 (40 upande wake 40 upande wangu ) tukafanya tafrija ndogo, mkuu ilikuwa vita, yule dada aliibuka na sauti ambayo sikuwai kuisikia kwa kusema rafki zake watamuonaje, kama ni ivyo bora ndoa yenyewe isiwepo, nikamuambia wasalimie, ni mwaka wa 4 sasaivi, na bado anasaga vumbi kutafuta ndoa