Kwa CV hii ya Dkt. Mashinji simuoni wa kumfikia pale Lumumba, jamaa kapiga shule namtabiria uteuzi wa mapema

Lakini ile report ya TWAWEZA si ilisema kuwa CCM ndiyo inayopendwa na watu wenye elimu ndogo na wazee?
 
Siasa ni sayansi bwashee!
 
Kaungana na watu waliomfungulia kesi ya mauaji ya Aquelina.

Anayekuambia elimu ni ukombozi anakudanganya.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tatizo kubwa ni kwamba ukishaingia kwenye siasa, CV yako unaiweka pembeni, unapigishwa kwata na ilani za vyama.
Ndiyo maana utakuta mtu ana CV nzuri sana kwenye fani fulani, na angeweza kuzalisha watu wazuri kwenye fani hiyo, lakini akishaingia kwenye siasa, anafanya vituko vya ajabu.

Kuwa na nafasi kwenye chama au nafasi za kuteuliwa na mkuu haiitaji kuwa na cv nzuri, ndiyo maana kuna watu wana Phd, Dr, nk lakini hawakuteuliwa hata kuwa wakurugenzi, wakuu wa wilaya au wakuu wa mikoa, lakini bahite anawapigisha kwata.
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Ninachoshangaa mimi ni kuwa mtu mwenye cv ya namna hii anawezaje kwenda ccm? Hajui kuwa kule ni lazima utoe akili yako kwanza? Masikini mwone Bashiru alivyo sasa, mwanzo alikuwa mwanazuoni wa kuaminika lakini sasa akili yote imeondoka!! Mashinji naye ngojeni atakapoanza kutumiwa, hutaamini kuwa ni msomi wa kiwango hiki.
 
Kwa bike
Kwa vile ni mpwa wa aliyeketi cha enzi ataupata faster
 
Nimekuelewa bwashee!

Tumeuwa vipaji na hazina ambayo ingezambazwa kwa vizazi vyetu kwa kuingiza wataalamu kwenye siasa.

Hawa watu wangekuwa vyouni, mashuleni wangewafundisha na kuwagawia watu wengi sana hiyo taaluma waliyo nayo.
Kinyume chake wamekuwa watu wakuamrishwa na kupiga makofi bila kuuliza wanachopigia makofi ni nini na je ni kizuri au kibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…