Kwa CV hii ya Dkt. Mashinji simuoni wa kumfikia pale Lumumba, jamaa kapiga shule namtabiria uteuzi wa mapema

Kuna watu wamepiga shule lakini wako kimya kabisa tofauti na yule msomi wa uchumi first class aliyetumbuliwa baada ya kutunukiwa PhD.

Nimeipitia CV ya Dr Mashinji kisha nikavuta CV kadhaa za madaktari wetu pale Lumumba kiukweli sijamuona wa kufanana naye Jamaa ni kichwa ndio maana Chadema wameumia sana.

Nikasema hebu nivute na CV za makamanda wa Ufipa nikakuta ni yale yale jamaa aliwaacha mbali mno.

Sikuchoka nikasema hebu basi niivute CV ya aliyekuwa kipenzi cha Ufipa Dr Slaa hapo ndio nikabaki najichekea moyoni kimya kimya.

Kwa hakika hii hazina inatakiwa ipate uteuzi wa haraka ikatumike serikalini.

Niishie hapo.

Maendeleo hayana vyama!

Kwahiyo unataka Kutuaminisha tena kilazima kabisa kuwa ndani ya CHADEMA na hata huku CCM alipohamia hakuna Watu ambao ama wana Elimu hiyo Kubwa na CV nzuri kuliko Yeye? Je, baada ya Kuipitia hii CV yake umeshafanya Juhudi zozote zile pia za ama Kuomba au Kutafuta CV's za wengine hasa hawa Wanasiasa? Na aliyekudanganya kuwa Kipimo sahihi cha Utendaji wa Mtu ni Elimu na CV yake pekee? Hivi waliopewa Nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania tokea Uhuru hadi hii leo hawakuwa na hizo Elimu na CV's kubwa na nzuri? Je, hizo Elimu na CV's zao zimeikomboa Tanzania na Umasikini wake na kuifanya isiwe Tegemezi kwa Maraifa makubwa ya nje? Je, hizo Elimu na CV's kubwa kama zingekuwa na Tija Rasilimali mbalimbali za Watanzania zingepotelea mikononi mwa Wajanja hasa Mataifa makubwa hasa Kiuchumi? Nitaheshimu Elimu na CV's za Waafrika ( hasa za Watanzania ) pale tu zitakapotumika kuleta Mabadiliko hasa ya Kiuchumi na Kimfumo kwa Watanzania wote kinyume na hapo bado nitaendelea tu Kuzipuuza japo Wewe unaonyesha ukisikia fulani ana Elimu kubwa na CV ya Kutisha huwa unababaika na kuwa tayari hata Kuwalamba Nyayo zao kama ukiwaona hata kabla hawajakuambia uwafanyie hivyo.
 
Akienda jela familia yake utailisha wewe bwashee?!
Kwa hiyo sababu kubwa iliyompeleka huko ni dili ya kufutiwa mashitaka katika kesi inayomkabili pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Chadema, na kama ni hivyo huu ni ushahidi kuwa Mahakama inafanya kazi zake kwa maagizo toka Lumumba. Waswahili wanasema kuchamba kwingi kuondoka na mavi. Johnthepaptist unafikiri unaitetea CCM kumbe unaipaka mavi. Asante kuijuza dunia kuwa Mahakama zetu haziko huru.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo unataka Kutuaminisha tena kilazima kabisa kuwa ndani ya CHADEMA na hata huku CCM alipohamia hakuna Watu ambao ama wana Elimu hiyo Kubwa na CV nzuri kuliko Yeye? Je, baada ya Kuipitia hii CV yake umeshafanya Juhudi zozote zile pia za ama Kuomba au Kutafuta CV's za wengine hasa hawa Wanasiasa? Na aliyekudanganya kuwa Kipimo sahihi cha Utendaji wa Mtu ni Elimu na CV yake pekee? Hivi waliopewa Nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania tokea Uhuru hadi hii leo hawakuwa na hizo Elimu na CV's kubwa na nzuri? Je, hizo Elimu na CV's zao zimeikomboa Tanzania na Umasikini wake na kuifanya isiwe Tegemezi kwa Maraifa makubwa ya nje? Je, hizo Elimu na CV's kubwa kama zingekuwa na Tija Rasilimali mbalimbali za Watanzania zingepotelea mikononi mwa Wajanja hasa Mataifa makubwa hasa Kiuchumi? Nitaheshimu Elimu na CV's za Waafrika ( hasa za Watanzania ) pale tu zitakapotumika kuleta Mabadiliko hasa ya Kiuchumi na Kimfumo kwa Watanzania wote kinyume na hapo bado nitaendelea tu Kuzipuuza japo Wewe unaonyesha ukisikia fulani ana Elimu kubwa na CV ya Kutisha huwa unababaika na kuwa tayari hata Kuwalamba Nyayo zao kama ukiwaona hata kabla hawajakuambia uwafanyie hivyo.
Mkuu huyu ndiyo hasa ana akisi picha halisi ya utawala wa CCM mpya,yaani wanathamini makaratasi na titles za watu bila kujali uwezo wao wa kudeliver.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda aokoe Tumbo lake

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Swadaktaaaaaaa
tapatalk_1582037457335.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom