Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Dua la Kuku. Elewa kuwa watu wabaya ndio hudumu muda mrefu na kula nchi sana kuliko watu wema
 
Nitakuunga mkono kwa dhuluma ya uaminifu lakini si dhuluma ya kura za 2015. 2015 Lowasa alipigwa na CCM ilishinda kwa kishindo. Ingawa ushindi ulikuwa wa magine ndogo. So acha kupotosha. Maswala ya urafiki wao hapo nakuunga mkono. Ila kura za 2015 Dr John Pombe Joseph Magufuli alishinda kwa kishindo.
 
Uliyoyasema ni sahihi, kuwa Mungu hutenda kazi kwa namna ambayo wakati fulani hata hatuifikirii. Ndiyo maana tunaambiwa tushukuru katika kila jambo.

Siamini kama kuna anayesikitika kwa nini Lowasa hakuwa Rais, bali watu wanasikitikia unafiki na dhuluma. Na Mungu kutenda kazi kwa namna tofauti tofauti, haiondoi ukweli kuwa unafiki na dhuluma ni ushetani. Na pia tukumbuke kuwa hata shetani hutenda kazi kwa namna tofauti tofauti kwa kuangalia udhaifu wako ulipolala. Kama udhaifu wako ni tamaa ya madaraka, basi unaweza kukuingia kupitia hiyo tamaa yako, ndiyo maana wengine wanafanya dhuluma mbalimbali ikiwemo hata kuua. Wanawaua wapinzani wao kisha kwa unafiki na ushetani wao, wanakimbilia kusema ama ni mapenzi ya Mungu, ama Mungu hakupenda awe kiongozi, n.k.
 
Any way labda kwasababu humu hatujuani status zetu za wasifa wa maisha yetu.
Kiuhalisia huenda haya makubaliano yanayo semwa hata haya kuwepo bali ni hear say tu za kutengenezwa ili kuongeza umaarufu wa mtu flani.
Na hata kama ni kweli nadhani watu hawa wawili walifahamiana kiundani zaidi kuliko sisi tunavyo Dhani.
Pia maisha yetu sisi binadamu tuna pambana sana kufikia mafanikio lkn ukweli unabaki kuwa muamuzi wa Mwisho ni Mwenyezi Mungu pekee ndio huamua wapi tufikie
 
Hivi mlutheri anaweza kuwa rais wa tanzania mkuu
Maana naona ni wakatoliki na waislam kutoka bakwata tu ndy marais

Ova
 
Waswahili wa Pwani sio watu wakuwaamini.

Lowasa alifanya kosa kubwa kumuamini mswahili.
Wale washkaji kitambo na wanajuana
Mbona nakumbuka kijiwe chao kilikuwa pale peace bar mwananyamala miaka hiyo na walikuwa wanakutana sana pale

Ova
 


Hii ni Kama nimeiona ikijirudia 2016-2021.


Inawezekana kabisa anaekalia kiti kikuu kutokua na taarifa ya mambo mengi na mengi mengine akasaidiwa “kuamua na outcome ya mwisho kabisa kwetu sisi watazamaji ikaonekana vyovyote vile iwavyo muhusika mkuu ni mkaaji wa kiti kikuu.

Yawezekana pia ndicho kilimkuta Nyerere mpaka akatangaza “kung’atuka, vijana walimchezea rafu za gizani nyingi.

Mwinyi yeye aliona isiwe tabu, “Ruksa era ikazaliwa wakati wake.

Pia inaweza kutoa mwanga ni kwanini Mkapa hakucheka na nyani. (Alikaa mbele mwenyewe)
Ukweli na Uwazi.
 
Mleta mada una ushahidi wa hilo? Ukikamatwa utaenda mahakamani kujibu nini haliyakua ushahidi huna!
 


Hapa inadhihirisha nguvu za Mwenyekiti wa Chama Mwaka huo 2014.


Ila sasa nashangaa jambo moja, hawa wanachama wa Wanamtandao mbona hili la presidential candidates wa 2015 ni Kama lilifanyika kwa zima moto?!

Kwanini na wakati “masterplanner na “kingmaker walikua na more than 5 yrs za kujiandaa na walikua jikoni kabisa na wao ndio walikua wapishi rasmi wa mambo mengi nyakati hizo?

Ama hiyo Richmond scandal na kujiuzulu kwa member muhimu wa wanamtandao kulipindua meza na plans zote?

Hivi kipi kilitangulia, kujivua Gamba ama Kujiuzulu uwaziri mkuu?

Lowassa aliposema “mheshimiwa speaker, tatizo ni uwaziri mkuu..” alimaanisha nini haswa?
 
mkuu unamwonea imani Lowasa vp ufisadi wake alioufanya kutajirisha familia yake...hutuonei huruma sisi watanzania!!!
au na wewe family member
Kuna aliye msafi kwenye huo mfumo? Humo kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…