Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Kuna aliye msafi kwenye huo mfumo? Humo kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake humo.
rejea uzi una,mtoa mada ana hanikiza huruma kwa lowassa ndo maana nikaleta haya yote,hakuna mwanasiasa kwenye taifa hili anatakiwa aonewe huruma labda wapinzani coz hawapo kwenye hiyo mifumo tunayoizungumza hapa
 
Uliyoyasema ni sahihi, kuwa Mungu hutenda kazi kwa namna ambayo wakati fulani hata hatuifikirii. Ndiyo maana tunaambiwa tushukuru katika kila jambo.

Siamini kama kuna anayesikitika kwa nini Lowasa hakuwa Rais, bali watu wanasikitikia unafiki na dhuluma. Na Mungu kutenda kazi kwa namna tofauti tofauti, haiondoi ukweli kuwa unafiki na dhuluma ni ushetani. Na pia tukumbuke kuwa hata shetani hutenda kazi kwa namna tofauti tofauti kwa kuangalia udhaifu wako ulipolala. Kama udhaifu wako ni tamaa ya madaraka, basi unaweza kukuingia kupitia hiyo tamaa yako, ndiyo maana wengine wanafanya dhuluma mbalimbali ikiwemo hata kuua. Wanawaua wapinzani wao kisha kwa unafiki na ushetani wao, wanakimbilia kusema ama ni mapenzi ya Mungu, ama Mungu hakupenda awe kiongozi, n.k.
Kuna mengi ya kiusalama yaliyomfanya ENL ashindwe kuwa rais wa TZ, naamini hatuyajui tunafanya kuandika ubashiri wetu. Alianza kukataliwa na Mwalimuu JKN akaja kukataliwa na mwanafunzi wa Mwalimu miaka 20 baadae hao wakongwe wa siasa wanazo sababu zenye mashiko za kwanini walilikata jina lake.

Mengineyo ni maongezi ya hisia tu hayana uwezo wa kubadili ukweli kwamba alizaliwa akatimiza wajibu wake na hatimeye Bwana amemtwaa.
 
Katika upumbavu ambao sijawahi kuukubali ni ile kauli ya marehemu pale Sheikh Amri Abeid Stadium, Arusha kwamba yeye na Kikwete walishaongea kuwa akitoka JK ni zamu yake kuwa Rais kama vile walikuwa na hatimiliki ya hii nchi. Wewe Bams umeandika ushuzi mtupu. Tanzania ni ya watu wote. Kama una vigezo vilivyowekwa kikatiba ruksa kuutaka urais. Hakuna dhuluma yoyote aliyofanyiwa marehemu Lowassa. Na hata kama alidhulumiwa basi ilikuwa sahihi kabisa kwasababu alishakufuru kwa kudhani yeye tu ndo anastahili kuwa Rais. Hayo mambo ya laana hakunaga kwenye siasa.
Majitu ya Pwani huwa ni ovyo na hayajali. Hili jambazi la msoga halijali chochote
 
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.

Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.

Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.

Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.

Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.

Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.

Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.

Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.

Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.

Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.

Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.

Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.

Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.

Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.

Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?

Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.

Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.

Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
Umeandika vizur sana. Huyu JK kizazi chake kitaishi kwa laana. Na hata, yeye atapata mapigo mazito. Huyu mzee anawafanya watanzania mazuzu wakati yeye ndio zuzu. Siri zake zote, zitawekwa, hadharani.
 
mkuu unamwonea imani Lowasa vp ufisadi wake alioufanya kutajirisha familia yake...hutuonei huruma sisi watanzania!!!
au na wewe family member
Lowassa anasingiziwa kwa ufisadi ambao hajawahi kuufanya.
 
Umeandika vizur sana. Huyu JK kizazi chake kitaishi kwa laana. Na hata, yeye atapata mapigo mazito. Huyu mzee anawafanya watanzania mazuzu wakati yeye ndio zuzu. Siri zake zote, zitawekwa, hadharani.

haya mashambulizi yote yalipaswa ayapate rostamu huyo ndo devil namba 1 tanzagiza sema kama kawaida anatuma niggas mbele wauwane wao kwa wao, yeye anachekelea tu benki na sasa hivi yuko vatikani au sijui norwayi kwa gharama zetu ofcourse …
 
Umeandika vizur sana. Huyu JK kizazi chake kitaishi kwa laana. Na hata, yeye atapata mapigo mazito. Huyu mzee anawafanya watanzania mazuzu wakati yeye ndio zuzu. Siri zake zote, zitawekwa, hadharani.
Dua la kuku
 
Hii ni Kama nimeiona ikijirudia 2016-2021.


Inawezekana kabisa anaekalia kiti kikuu kutokua na taarifa ya mambo mengi na mengi mengine akasaidiwa “kuamua na outcome ya mwisho kabisa kwetu sisi watazamaji ikaonekana vyovyote vile iwavyo muhusika mkuu ni mkaaji wa kiti kikuu.

Yawezekana pia ndicho kilimkuta Nyerere mpaka akatangaza “kung’atuka, vijana walimchezea rafu za gizani nyingi.

Mwinyi yeye aliona isiwe tabu, “Ruksa era ikazaliwa wakati wake.

Pia inaweza kutoa mwanga ni kwanini Mkapa hakucheka na nyani. (Alikaa mbele mwenyewe)
Ukweli na Uwazi.
Kuna kipindi rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alichoka kuibaiba chaguzi, akasema tuwaachie hawa wapinzani.

Wale watu wa security organs wakamwambia haaachiwi mtu hapa. Sisi tushawapiga na kuwaua sana hawa wapinzani. Wakija kuchukua nchi watatulipizia kisasi.

Wakamwambia wewe Mugabe kaa utulie, sisi tutafanya michezo yetu.

Rais mwenyewe kuna wakati anakuwa hostage wa system.

Sasa, sisi badala ya kuangalia mfumo, tuubadilishe, tunaangalia mtu.

Hatuwezi kumaliza matatizo ya kimfumo kwa kutafuta lawama za mtu.
 
Wewe ndiye umepanic. Mimi mara zote first post inakuwa na makosa halafu na edit.

Wewe ndiye umepanic.
Hakuna ku panic hata kidogo, sababu nyingine ilinifanya nikuache upoe ni baada ya kuona kwenye huu uzi unagombaniwa kama mpira wa kona, kila mmoja anataka kufunga kupitia wewe, ndio maana kichwa yako inapata moto.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hakuna ku panic hata kidogo, sababu nyingine ilinifanya nikuache upoe ni baada ya kuona kwenye huu uzi unagombaniwa kama mpira wa kona, kila mmoja anataka kufunga kupitia wewe, ndio maana kichwa yako inapata moto.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Kugombaniwa mimi ni kawaida, kwa sababu huwa sijali watu wanafikiri au wanapenda nini, huwa najieleza ninavyofikiri mimi kwa kiasi changu, kwa kuangalia ukweli ninavyouelewa.

Ila kunradhi, ukiona post ya kwanza ina typos nipe dakika chache, yumkini post ya kwanza inapita na typos lakini mara nyingi huwa narekebisha right away.
 
Back
Top Bottom