Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Tulikua bado wadogo japo sio sana.Kwamba 2008 ulikuwa mdogo sana?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tulikua bado wadogo japo sio sana.Kwamba 2008 ulikuwa mdogo sana?
Ila we jamaa ni mpumbavu sana. Hufai hata kujibiwa na mpumbavu mwenzioKwamba Lowassa 'Urais ulikuwa ni Haki yake kutoka Kwa Mungu' kwahiyo kadhulumiwa?
Cha ajabu wanaolia Lia na hili ni Chadema. Kama Lowassa aliona CCM wamemdhulumu why alirudi CCM?
Kama alisamehe why Chadema inawauma sana?
Lowassa hii Haki ya kuwa Rais ilitoka wapi?si na Kambona nae watoto wake watadai Nyerere alimdhulumu Urais?watoto wa Sokoine je waseme Baba Yao aliuwawa ili asiwe Rais?
Mijitu mizima inalialia na consipiracy theory za kitoto kabisa
Kuna tofauti kubwa sana kati yangu na Lowassa.Sasa Kiranga, umemsema Lowasa sana ktk ujenzi wa hoja zako na Bams kuhusu kwanini Lowasa alijiuzuru na kumuachia matatizo rafiki yake Kikwete.
Hapa na wewe unasema umepiga kura uchaguzi wa kwanza tu na kutokomea ughainuni. Huoni na wewe umetuachia matatizo ya nchi tuhangaike nayo wenyewe halafu unakuja kutusimanga sisi tuliowachagua hawa viongozi.
Huoni unafanya kama Lowasa. Ama labda utuambie sababu ya kwenda ughainuni haikusababishwa na siasa na maisha mabovu ya hapa nyumbani.
Inasemekana mipango ilikuwa fresh tu na wanamtandao, sema katika mipango yao ilikuwa baada ya JK kupata urais Sita ndiyo atakuwa waziri mkuu na Lowasa yeye atakuja kuwa rais awamu ikifika, shida ilianzia pale baada ya JK kuwa rais wakina rost walimweleza lowasa anatakiwa awe waziri mkuu ili kujijenga zaidi kwahiyo sita akatoswa na kupewa uspika.Hapa inadhihirisha nguvu za Mwenyekiti wa Chama Mwaka huo 2014.
Ila sasa nashangaa jambo moja, hawa wanachama wa Wanamtandao mbona hili la presidential candidates wa 2015 ni Kama lilifanyika kwa zima moto?!
Kwanini na wakati “masterplanner na “kingmaker walikua na more than 5 yrs za kujiandaa na walikua jikoni kabisa na wao ndio walikua wapishi rasmi wa mambo mengi nyakati hizo?
Ama hiyo Richmond scandal na kujiuzulu kwa member muhimu wa wanamtandao kulipindua meza na plans zote?
Hivi kipi kilitangulia, kujivua Gamba ama Kujiuzulu uwaziri mkuu?
Lowassa aliposema “mheshimiwa speaker, tatizo ni uwaziri mkuu..” alimaanisha nini haswa?
Kuna kipindi rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alichoka kuibaiba chaguzi, akasema tuwaachie hawa wapinzani.
Wale watu wa security organs wakamwambia haaachiwi mtu hapa. Sisi tushawapiga na kuwaua sana hawa wapinzani. Wakija kuchukua nchi watatulipizia kisasi.
Wakamwambia wewe Mugabe kaa utulie, sisi tutafanya michezo yetu.
Rais mwenyewe kuna wakati anakuwa hostage wa system.
Sasa, sisi badala ya kuangalia mfumo, tuubadilishe, tunaangalia mtu.
Hatuwezi kumaliza matatizo ya kimfumo kwa kutafuta lawama za mtu.
Mjinga sana wewe ,kwani kama huelewi si ukae kimya??Kwamba Lowassa 'Urais ulikuwa ni Haki yake kutoka Kwa Mungu' kwahiyo kadhulumiwa?
Cha ajabu wanaolia Lia na hili ni Chadema. Kama Lowassa aliona CCM wamemdhulumu why alirudi CCM?
Kama alisamehe why Chadema inawauma sana?
Lowassa hii Haki ya kuwa Rais ilitoka wapi?si na Kambona nae watoto wake watadai Nyerere alimdhulumu Urais?watoto wa Sokoine je waseme Baba Yao aliuwawa ili asiwe Rais?
Mijitu mizima inalialia na consipiracy theory za kitoto kabisa
Confidential source. Kigogo wa CCM aliyekuwa katika kamati ya ufundi ya kusaidia kutoa ujuzi wa CCM kubadili matokeo huko Zimbabwe."Kuna kipindi rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alichoka kuibaiba chaguzi, akasema tuwaachie hawa wapinzani.
Wale watu wa security organs wakamwambia haaachiwi mtu hapa. Sisi tushawapiga na kuwaua sana hawa wapinzani. Wakija kuchukua nchi watatulipizia kisasi.
Wakamwambia wewe Mugabe kaa utulie, sisi tutafanya michezo yetu".
Ndugu Kiranga ,hii umeitoa wapi tafadhali!!!??
Waingereza wanasema "There is no honor among thieves".Kikwete mtu mbaya sana
Kwa sababu gani tujute?Mimi nachoshukuru lowasa hajawa rais tungejuta.
Kama mtu akinisaidia kunipandisha juu kisha baadaye na yeye akataka msaada wangu nimsaidie naye apande huku nilipokuwepo lakini mimi nikaamua kumkaushia na kumpiga biti asije huku juu watu lazima watasema mimi ni mtu mbaya sana. !Jambo la Msingi ni kumuombea heri marehemu, lakini hizi ngonjera za uaminifu, sijui usafi, upendo nk nk ni yeye tu ndiye aliujua ukweli wake.
Urais ni haki ya Mtanzania yeyote mwenye sifa na hakuwa na hakimiliki ya nafasi hiyo, hivyo kukosa kwake ni sawa na wale wengine walioukosa.
Humu wengi ni wa nineties 🙏Kwamba 2008 ulikuwa mdogo sana?
Alikua na genge la majambazi limemzunguka.Kwa sababu gani tujute?
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.
Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.
Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.
Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.
Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.
Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.
Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.
Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.
Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.
Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.
Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.
Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.
Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.
Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.
Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?
Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uzee wetu.
Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.
Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
Mfumo unabadilishwa kwa uwazi, sheria, teknolojia, ushirikishwaji wa umma.
Mpaka leo bungeni mambo yanapitishwa kwa kura za sauti. Kura mbunge anapiga bila kuogopa personal responsibility.
Ilitakiwa kura zote muhimu zirekodiwe kwa majina mbunge gani kapiga kura ku support mkataba wa Dubai kuchukua bandari, halafu wananchi wanaopinga jambo hilo wote wawajue wabunge kwa majina nani kapiga kura vipi, wawabane. Sasa hivi tunasema tu "bunge limeridhia" lakini hakuna personal accountability kwa mbunge mmoja mmoja.
Sanasana tutasema tu Halima Mdee alipinga.
Sasa, ukiweka mfumo wenye uwazi zaidi, hata mbunge anayetakankupigabkura ya kijinga lazima atajiuliza mara mbili, maana anajua atabanwa kwa ushahidi mkubwa.
Hao watu unaowasema ni pipa na mfuniko, inabidi wenye nia nzuri na elimu bora wa speak up zaidi, wapo, tatizo wajinga wenye hila wanapewa promo kuliko wenye akili na nia nzuri.
Jambo la Msingi ni kumuombea heri marehemu, lakini hizi ngonjera za uaminifu, sijui usafi, upendo nk nk ni yeye tu ndiye aliujua ukweli wake.
Urais ni haki ya Mtanzania yeyote mwenye sifa na hakuwa na hakimiliki ya nafasi hiyo, hivyo kukosa kwake ni sawa na wale wengine walioukosa.