Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Mengine ni dua za kuku tu kwa Mwewe.
 
Huoni kwamba hili ni jambo jema sana la uwajibikaji kiongozi yeyote hata ikiwa ni Rais kujiuzulu pale inapoonekana ameshindwa kutimiza majukumu yake sawasawa?!

Mbona Mwinyi aliwahi kujiuzulu akiwa waziri halafu akaja kuwa Rais baadaye?
Kujiuzulu inawezekana likawa jambo jema, lakininsi qualification ya kuwa kiongozi.

Enzi za Mwinyi hazikuwa za siasa za uwazi na ushindani kama sasa, ni enzi ambazo mtu mmoja aliweza kutawala miaka 24. Ni enzi tofauti kabisa.
 
Umeweka links nyingi mno, hembu summarize.
 

Tatizo unachangia bila kuelewa hoja.

Hayo mambo ya urafiki kati ya marehemu na Kikwete yamewekwa tu ili kuonesha mmoja alivyomsaliti rafiki yake.

Jambo la msingi ni ushetani wa Jakaya:

1) Kwa katiba ya CCM, Lowasa na mwanaCCM mwingine yeyote, wote walikuwa na haki ya kugombea nafasi ya Urais na kisha kupigiwa kura na wajumbe. Lakini Kikwete kwa kujua kuwa Lowasa lazima angeshinda kama jina lake lingekuwemo katika watu wa kupigiwa kura, akaamua kulikata jina la Lowasa.

Jambo la pili, ni ule ushetani wa siku zote wa CCM. Lowasa kagombea kupitia chama kingine, lakini kwa kutumia madaraka yake ya Urais akapora ushindi wa Lowasa na wa Maalim Seif.
 
Sina chochote kumlaumu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuhusu Marehemu Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Vyote vilivyofanyika ndivyo vinatufanya leo hii kuwa huru kutoa maoni.
Tumshukuru Mungu Kwa Maisha ya wote wawili,ingawa mmoja katangulia mbele za haki.
Nina hakika siku Mzee Kikwete naye akiondoka kuna watu watasema tena kama ambavyo leo tunasema.
Mwenyezi Mungu mpumzishe mpendwa wetu mahala pema na uwajaaliwe Viongozi wengine na sisi kwa ujumla tuishi maisha marefu yenye fanaka.
 

Nakubaliana nawe. Kikwete ni mtu wa kuuma.na kupuliza lakini lengo lake ni kuuma.
 
JK anamiaka 70 huko sasa una taka afe na miaka mingapi? Ukiona amekufa ujue ahadi yake ilishafika ndio maana yupo hadi Leo maana angeweza kufa hata na miaka 20.

Kikwete 73 years as to date.

Lowasa 71 years
 
Kuwaelewa watanzania walio wengi ni ngumu na ugumu zaidi ni kuwa wanaamini wanaelewa kila kitu kilichotokea kuliko wahusika wenyewe na hivyo hata Mzee JK angesema nini bado wangeendelea kuamini wanachoamini.Sina baya na Mzee Lowassa ila alikuwa binadamu mwenye mapungufu yake na mazuri yake. Huu ukamilifu watu tunaompa na ustahili unatufanya tusijifunze kwake na mchakato mzima wa hicho anacholaumiwa Mzee JK. Kuna yaliyositiriwa ambayo umma haujui na kwahiyo lawama zote zitaelekezwa kwa mtu.
 
Unajuaje Kikwete alimkata jina Lowassa kwa kudhulumu haki yaje na si kwa kuifanyia Tanzania haki kwamba alijua Lowassa ni kiongozi dhaifu ambaye kashindwa hata Uwaziri Mkuu na kwenye urais angeleta shida kubwa zaidi?

Lowasss alijuwa na haki ya kugombea urais, lakini si haki ya kushinda urais.

Na kugombea urais katimiza hiyo haki yake, nje ya CCM, lakini bado hakushinda urais.
 
Kikwete ni mnafiki mkubwa.
Maradhi alopata lowasa yaliasisiwa na kikwete.
Mungu atamlipa
 
Lowassa anaweza kuwa na matatizo yake ila sio la kiongozi dhaifu, alikuwa ni mtu mwenye maamuzi na pia mchapakazi tukiangalia alivyosimamia mpango wa shule za kata na mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kupeleka mikoa kadhaa.

Sidhani kama kuna mawaziri wakuu waliowahi kuwa na nguvu kuliko Sokoine na Lowassa.
 
kiukweli Masai yero kazingua mzee wa Msoga hana baya kumpa shavu la uwazirii kazingua mwenyewe alf then anataka Uraisi JK akaona wee bhana acha kuzingua...
 
Wewe mzenj mambo ya huku Tanganyika huwezi kuyajua! Bila Lowassa Kikwete asingepata Urais; mipango yote ya kampeni iliratibiwa na Lowassa!
Nyie wazenj pambaneni na hali yenu kuamua kama Rais wenu Hussein Mwinyi ni Mzanzibari au sio!
Alipewa nafasi ya uwaziri mkuu amelipwa chake JK hana baya
 

Halafu kama alidhulumiwa huko CCM mbona alisamehe na kurudi...
Nongwa imebaki Kwa hawa wafuasi uchwara ambao hata alipokuwa Ccm walimwita fisadi...Leo ghafla Eti kadhulumiwa
 

Kutokuwa dhaifu na kuwa na nguvu hata Hitler ana sifa hizo. That does not mean Hitler was good for Germany or the world.

Sokoine alikuwa na maamuzi sana lakini alikuwa na papara. Kuna siku Nyerere alitania tu akisema barabara zetu hususan vijijini ni mbovu sana, inaonekana kama tutahitaji wakuu wa wilaya wajifunze kupanda farasi ili kufikia wananchi.

Kesho yake Sokoine akaanza maongezi ya kuagiza farasi. Balozi Raphael Lukindo akatoa tahadhari, jamani farasi wanataka maandalizi, wanataka mipango, mkiwaleta kwa pupa watakufa tu. Sokoine akatumia turufu ya Uwaziri Mkuu kunyamazisha hoja za balozi Raphael Lukindo, akaagiza farasi tu kutoka Argentina. Mwishowe farasi wale wakafa kama alivyotabiri balozi Raphael Lukindo.

So much for being a strong lrader.

Whether Lowassa ni kiongozi mzuri au si kiongozi mzuri is debatable, what is not debatable, ni kwamba, Lowassa kujiuzulu, against Kikwete's advice per Bams, ilikuwa fatal mistake, ilikuwa shooting oneself in the foot before starting a marathon, and hoping to win.

Na kumtegemea Kikwete am support Lowassa baada ya Lowassa kujiuzulu kwa scandal, against Kikwete's wishes, is pure naivette.
 
Na JK kutoikataa hiyo barua, ndio hofu kwake ikaanza akiamini kama Lowassa angekuwa Rais, basi angekuja kulipa kisasi.

Pia, uchafu wa Ridhiwani wakati wa utawala wa baba yake, JK akaamua kumtosa Lowassa, ndio maana Ridhiwani akaropoka "Rais hatatoka Kaskazini", kwasababu ya hofu ya kisasi.

Walijua angekuwa Membe ili awalinde, bahati mbaya mambo yakatibuka bahati ikamuangukia Magufuli, hapo tena ikabidi waliokuwa na dili chafu waanze kujisalimisha kwa Magufuli, akiwemo Home Shopping Centre na GSM.

Makubaliano yao yaliitwa; Gentleman's Agreement.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…