Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Wewe mpuuzi waliotangaza nia walikuwa 38 na majina yalihitajika matano. Kwanini unamuongelea mtu mmoja tu?
 
Hiyo stori ya Sokoine na kuleta farasi inaonyesha jinsi gani alikuwa kiongozi anayejali hali za raia wa chini, kama mpango wake huo wa kuwapa wakuu wa Wilaya farasi ungefanikiwa( na kama pia haukuhujimiwa ukizingatia farasi ni mmojawapo ya wanyama wanaovumilia mazingira magumu sana) huenda viongozi wangejibidiisha na leo hii vijiji vyote vingekuwa na lami kuepuka kuendelea kutembelea farasi.

Hiki pia ndicho Lowassa alikuwa akikipigia kelele, kwamba watu wafanye maamuzi katika nafasi badala ya kujizungusha zungusha tu. Akiwa waziri alisimama kidete kwamba tutatumia maji ya Ziwa Victoria kupelekea raia maji safi potelea pote na leo hii maji ya Ziwa Victoria yanatumiwa na mamilioni ya raia.
 
JK inawezekana ana matatizo yake, mengi tu.

Lakini, kwenye hili la Lowassa.

Mimi sielewi kwa nini JK analaumiwa kwenye hili.
Kwa sababu kwenye kinyang'anyiro muhimu alimpitisha Membe akamuacha Lowassa.
 
Lowqssa kuiandika hiyo barua alijimaliza mwenyewe.

Hizo nyingine zote ni detail tu.
 
Hiyo story ya Sokoine inaonesha Sokoine alivyokuwa kiongozi aliyefanya maamuzi kwa papara, bila kujipanga vizuri wala kusikiliza wenzake.

Lowassa alijimaliza mwenyewe kisiasa kwa kukubali kujiuzulu, hapa asilaumiwe mtu mwingine yeyote.
 
Hiyo story ya Sokoine inaonesha Sokoine alivyokuwa kiongozi aliyefanya maamuzi kwa papara, bila kujipanga vizuri wala kusikiliza wenzake.

Lowassa alijimaliza mwenyewe kisiasa kwa kukubali kujiuzulu, hapa asilaumiwe mtu mwingine yeyote.
Sasa mbona hata aliyepitishwa na kuupata tena huo Urais baadaye mojawapo ya malalamiko makubwa zaidi kwake ni kufanya maamuzi ya papara!
 
Watu Bwana, yaani walitaka JK amzawadie Urais EL halafu watu hawa hawa wanapinga ujamaa kwenye uongozi.

kifua cha JK kina mambo mengi sana ambayo wengi hatuyajui, ila ninachoweza kusema yule ni mwamba na amevuka vikwazo vingi Sana vigumu na hata tukizogoza anabaki anacheka tu.
 
Sasa mbona hata aliyepitishwa na kuupata tena huo Urais baadaye mojawapo ya malalamiko makubwa zaidi kwake ni kufanya maamuzi ya papara!
This is a logical non sequitur argument.

Two wrongs do not make a right.

Tusiikubali papara popote.

Mseme huyo aliyepitishwa naye, tujifunze, tuikatae papara.

Na tunamsema. Tunamsema hapa. Binafsi namsema. Kwangu hii si hoja.

Usihalalishe papara ya aliyekatwa kwa sababu hata aliyepitishwa naye alikuwa na papara.
 
Mada hii inaweza kuonekana ni nzuri muda huu wakati wa kuuhani msiba wa Lowassa, lakini ghafla pumzi ikimrudia hayati naamini huu uzi utakosa kabisa mashiko.

JK anazeeka na amani sio kwa sababu aliishi vizuri alipokuwa rais na kabla ya hapo, ni kwa sababu hana vinyongo vingi na hujitahidi kucheka na kusamehe kabla hajaenda kulala usiku.

JPM alikufa na vinyongo vingi na vikautesa moyo wake, Lowassa nae alihamia kwenye ulevi wa pombe kali baada ya kuukosa urais.

Ukiwa mwanasiasa punguza kabisa uwezekano wa kulala na chuki moyoni, itautesa moyo wake na itakuua siku moja.

Hilo ni somo la maisha ya JK, hana wema huo na haonekani kupigania ile hulka ya kutaka watu wamuone mwema lakini kajaliwa sana ule moyo wa kiswahili wa kuchukulia kila kitu katika mtazamo wa masihara.
 
in politics there is no permanent enemies....

hiyo ni mambo ya siasa na ilikwisha nyakati hizo na maisha ya kila moja yakaendelea na mpaka hivi sasa yanasonga....

Siasi sio yakuweka kwa roho aliwahi kusema haya rafiki yangu sana huko Kenya anaitwa Governor Mandago wa county ya Uasin Gishu wakati huo, ingawa sasahivi ni senator....

hakuna mtu anaweza kukaa bila amani eti kwa sababu ya fulani katika siasa...
hiyo ikikupita ndio imeisha hiyo hakuna kuangalia nyuma tena....

R.I.P Laigwanan comrade ENL
 
Sasa mtu kashajiuzulu uwaziri mkuu kwa kashfa, kinyume na ishauri wa rais, JK ampitishe vipi kugombea urais tena?
Sijui sababu zilizopelekea JK kutoingiza jina la Lowassa katika mojawapo ya majina ya kupelekwa kwa wajumbe kupigiwa kura ila kama ni hiyo sababu ya kujiuzulu kinyume na ushauri wake basi itakuwa sababu dhaifu sana na gubu la aina yake.
 
Mengi hatuyajui na hii mada inatokana na mahaba binafsi ya mkuu Bams kwa hayati Lowassa.

Kuongoza nchi mgombea anachaguliwa na Mungu hajichagui yeye mwenyewe, ukitumia nguvu nyingi sana kuutaka urais unakuwa na shida fulani ambayo kwa nchi za kiafrika ni hatari sana kuwa nayo.

Ikulu kuna biashara gani mpaka mtu atumie pesa kutaka kufika - Julius Nyerere Mei Mosi 1995 uwanja wa sokoine Mbeya.
 
Hapa hakuna logical non sequitur wala nini,
Kwa sababu umejenga hoja kwamba maamuzi aliyofanya Lowassa huenda yalionyesha ni kiongozi mwenye papara hadi ukatolea na mfano wa Sokoine wa farasi, sasa mimi natumia hoja yako hiyo hiyo uliyoijenga na kukuuliza kwamba ina maana gani sasa kama aliyepitishwa na baadaye akashinda kisha lawama zikawa nyingi kuliko kwake kwamba ana maamuzi ya papara pia.
Mimi kwangu hii ni hoja yenye contradiction.
 
Usijitoe ufahamu ndugu. Pia Muogope Mungu. Iondoe akili yako kwenye Itikadi za vyama ndipo utakapokuwa na fikra sahihi
 
Mungu hachagui mtu kuongoza nchi Steve, kumbuka hapa ni JamiiForums na sio Kanisani kwa Mwamposa, acha tantalila!

Rais wa nchi anachaguliwa kwa kura na wananchi, na mtu kuonesha nia ya kutaka kuwaongoza wengine sio dhambi wala kosa kisheria. Dunia ya sasa lazima uoneshe nia thabiti ya kutaka kitu ndio upate, haya mambo ya sijui mtu kutumia nguvu nyingi kuutaka urais atakuwa na shida fulani ni imani za kipumbavu na kilofa tu.
 
Lowqssa kuiandika hiyo barua alijimaliza mwenyewe.

Hizo nyingine zote ni detail tu.
Imani ya Lowassa kwa rafiki yake ndio iliyomponza.

Baada ya yote kutokea, sasa ndio narudi kule juu kwa mleta mada aliposema; "JK ataumaliza uzee wake bila amani", kwa sababu ya usaliti aliomfanyia Lowassa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…