Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Kabla ya kupigiwa kura kuna michakato mingi, elewa maana pana ya sentensi yangu achana na hizo issue za Mwamposya.
 
""KINACHONIUMIZA BINAFSI NI UTU WA LOWASSA, ALIKUBALI KUBEBA FURUSHI LA LAWAMA ALIMRADI AMUOKOE RAFIKI YAKE""
Walutheri wangekuwa na sera za utakatifu basi Lowassa alistahili.
 
Kabla ya kupigiwa kura kuna michakato mingi, elewa maana pana ya sentensi yangu achana na hizo issue za Mwamposya.
Hakuna maana pana hapo mkuu, mchakato wote unahusisha watu na watu ndio wanapitisha watu wachaguliwe kuwa marais. Rais Kikwete inaaminika alienda Dodoma na majina yake matano ya mfukoni, labda kama unataka kusema Mzee Kikwete ni Mungu.

Mungu amekupa Pumzi uyatafute maarifa, Mungu hajawahi kumfanyia mtu chaguo hapa duniani.
 
Hongera Mkuu unachambua kwa hoja nina imani Bams atakuelewa tu
 
Sijui sababu zilizopelekea JK kutoingiza jina la Lowassa katika mojawapo ya majina ya kupelekwa kwa wajumbe kupigiwa kura ila kama ni hiyo sababu ya kujiuzulu kinyume na ushauri wake basi itakuwa sababu dhaifu sana na gubu la aina yake.
Huoni sababu ya kamanda aliyekimbia uwanja wa vita si kamanda anayefaa kuongoza majeshi kuwa ni sababu tosha?

Huoni sababu ya huyu ana wingu la kashfa ya ufisadi mpaka kajiuzulu, na tukimteua awe ngombea wetu, kabla ya kuanza kutangaza ajenda yetu katika kampeni, tutakuwa na mzigo wa ziada wa kumsafisha mgombea wetu kutoka kwenye wingu hili la kashfa ya rushwa, na kwa nini tujipe kazi hiyo ya ziada, ikiwa kuna wengine wengi ambao hawana hilo wingu la kashfa na tunaweza kuanza nao kampeni bila mzigo wa kuwasafisha, huoni hoja hii inatosha kumuondoa Lowassa?
 
Nasikia hakufanya kwa Lowassa tu...bali kwa wengeni wengi

Kama yote yasemwayo ni kweli basi kwa hakika Kikwete hatakuwa na amani
 
Japo nilikua bado mdogo kipindi hicho lakini mambo hayakua marahisi kama ulivyo andika. Right kama mzee kikwete angefanikiwa kuwaweka hao wawili ulio wazungumzia sidhani kama CCM ingepona. Kuhusu kwamba Lowassa alimshinda kura JPM sio kweli. Kilichokua kinaenda kuiua CCM kama Lowassa angegombea kupitia CCM ni zile kashfa. CCM ingekufa palihitajika mtu aliyekua msafi ili CCM ipate kushinda lasivyo CCM ingekufa. Hongera Lowassa, Kikwete na JPM kwa kuiokoa CCM. Na ukumbuke agenda zote za CHADEMA za mambo ya ufisadi zilikua zinamhusu Lowassa na CCM. Mimi kwa mtazamo wangu nawapongeza wote Lowassa, JPM na Kikwete kwa kuendelea kuiwezesha CCM kusurvive.
 
Kama hoja ni Lowassa kukatwa kwa sababu ya kashfa ya Rushwa na angekuwa mzigo mzito kwa chama chake kumuuza kwa wapiga kura hapo nitaelewa hata kama sijui alihusika kiasi gani na kashfa yenyewe, japo pia maswali yanabaki hasa ikijulikana mgombea yeyote ambaye angepitishwa na CCM angeshinda tu kwa namna yoyote ile na hiyo hudhihirika kwa hadhi wanayopewa wagombea wa chama hicho na dola pale wanapoteuliwa hata kabla ya kushika dola yenyewe.
 
JK inawezekana ana matatizo yake, mengi tu.

Lakini, kwenye hili la Lowassa.

Mimi sielewi kwa nini JK analaumiwa kwenye hili.
Kikwete ndiye aliyekata jina la Lowassa nisiende kupigiwa kura ya kuwa mgombea urais kupitia ccm!!
 
Hakuna contradiction mkuu.

Mimi nakataa papara popote.

Kwa Nyerere, kwa Sokoine, kwa Lowassa, kwa Magufuli. Kwa Makonda.

Kwa aliyepita, kwa akiyekatwa. Kwa aliyekufa, kwa anayeishi.

Nikikataa papara kwa aliyekatwa, halafu wewe ukanipa mfano wa aliyepita kwamba mbona huyu naye ana papara, nitakwambia hata huyo naye papara yake niliikataa.

Ushindi wa mtu katika uchaguzi hauoneshi kwamba yuko sawa. Hata Hitler alishinda uchaguzi. Kwa ulaghai.

Inawezekana Watanzania hawajafikia kiwango cha kuielewa na kukataa papara popote wanapoiona, wakaona papara ya Magufuli au ya Makonda ndiyo uongozi wanaouhitaji.

Mimi nasimama palepale kupinga uongozi wa papara, bila kujali huyu kiongozi anapendwa vipi, kachaguliwa kama Magufuki au kakatwa kama Lowassa.

Ameshafariki au anaishi kama Makonda.

Papara ni papara tu.

Sasa wewe ukija na objection yako "mbona Magufuli kachaguliwa wakati alikuwa ana papara" hilo ni kosa la Watanzania waliomchagua, si langu.

Mimi sijawahi kumpigia kura Magufuli, na nimekuwa nikimsema sana utawala wake wote na mpaka kesho namsema kwa papara.

Sasa, hilo swali lako halifai kunitupia mimi, mimi sijamchagua Magufuli. Mimi nimepiga kura uchaguzi wa 1995 tu, baada ya hapo nimekipa kitu viwanja vikubwa, nimepiga kura kwa miguu yangu kuondoka Tanzania.

Kawatupie swali hilo waliomchagua Magufuli.
 

Kwenye kashfa ya Richmond, Lowasa hakutuhumiwa kwa rushwa. Tuhuma za uzembe zilielekezwa wizara ya madini na nishati, kwa nini waipe tenda kubwa ya kuzalisha umeme kampuni isiyo na uwezo. Katika kujitetea, waziri wa madini na nishati akasema kuwa asilaumiwe yeye pekee kwa sababu maamuzi yalifanywa na Serikali nzima.

Lowasa alijiuzulu kutokana na nafasi yake kama kiongozi mkuu wa Serikali bungeni.
 
JK ana bullet proof ya kisaikolojia kwenye hivi vimaneno maneno vya mtaani.

Mtoto wa Saigon yule kazoea matani ya wazee wa Kiswahili yale ya kujambishana kwenye vikao vya kahawa chungu nyeusi na kashata.

Vikao vile kama huna kifua cha kuhimili maneno huviwezi, na JK ndiyo vikao vyake.

Sasa Mswahili kama yule unafikiri unaweza kumtisha kwa maneno tu?

Kashasema "Huo ni upepo tu, utapita" wakati yupo katikati ya heavy scandal.

Unafikiri ataogopa maneno ya waombolezaji msibani?

Mtu kashajipitia life expectancy ya wabongo, kashakula mazuri ya nchi yote, kashaandaa vizazi na vizazi kukaa vizuri hata akifa kesho, anahudumiwa na taifa mpaka kufa, anataka amani gani zaidi ya hiyo?
 
Naunga mkono hoja
 
Mkuu,

Hata kama CCM inajua mgombea yeyote atakayeteuliwa na CCM atashinda, bado wana CCM, hususan viongozi, wana haki ya kusema hawataki mgombea atakayewapa mzigo mkubwa kumnadi kwenye kampeni.

That is perfectly reasonable.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…