Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Siasa za Tz ni mchezo mchafu
 
Wazee wa matukio hao tushawajua, kwahiyo hawatuumizi kichwa
 
Mkuu,

Hata kama CCM inajua mgombea yeyote atakayeteuliwa na CCM atashinda, bado wana CCM, hususan viongozi, wana haki ya kusema hawataki mgombea atakayewapa mzigo mkubwa kumnadi kwenye kampeni.

That is perfectly reasonable.
Hiyo ya 2015 labda ilikuwa CCM tofauti kabisa na ile ya 2020, ngoja tuone ya 2025 itakavyokuwa.
 
Kikwete ndiye aliyekata jina la Lowassa nisiende kupigiwa kura ya kuwa mgombea urais kupitia ccm!!
Hata hili nalo bado linahitaji uhakiki.

Kwa sababu michakato yetu haina uwazi.

Lakini, hata kama ikiwa kweli, Lowassa mwenyewe alijijengea mazingira ya kukatwa kwa kujiuzulu (against Kikwetes advice per Bams).

Sasa, ikiwa Kikwete alikuwa na choice, CCM iende na mgombea ambaye hana wingu la kashfa za ufisadi, ambaye itaweza kuanza naye kampeni moja kwa moja bila kumsafisha, au iende na mgombea mwenye wingu la kashfa za ufisadi, mpaka akajiuzulu, kiasi kwamba huyu mwenye kashfa, chama kabla ya kuanza kampeni, kitahitaji kutumia nishati na muda wa ziada kumsafisha kwanza, kabla ya kuongelea ajenda za chama kwenye kampeni.

Hapo kweli mnaona Kikwete alipaswa kukubali mgombea mwenye wingu la ufisadi aende ku distract message ya ajenda za CCM na kuwabebesha mzigo wana CCM kumsafisha kwanza kabla ya yote?

Kikwete aliona twende na mtu asiye na mzigo wa ziada wa kashfa. Tujikite kwenye kuelezea ilani ya chama zaidi kuliko kumsafisha mtu.
 
Ili ccm kiendelee kutesa watu kama sahivi
 

CCM Wana taratibu zao na yeye ndio alikuwa mwenyekiti wa hicho kikao, kilichomkataa EL ni taratibu za CCM wenyewe ndani ya vikao vyao sio JK.

toka 1995 ninasikia upinzani umeshinda na umeibiwa kura, Watanzania wengi bado ni wajinga ndio maana CCM inashinda maana wengi wanaamini katika CCM. 2015 binafsi nikipiga kura Kwa mara ya kwanza na kura yangu ilienda kwa JPM maana niliamini kwa JPM na ilivyokuwa kwa Watanzania wengi 2015 madai yako EL alishinda na kuconclude alidhulumiwa hayana mashiko zaidi ya "hearsay" maana hakuna chombo huru kilichothibisha hili.
 
Hizo ni minutiae za nuance ambayo big picture optics haijali.

Kwa nini Lowassa alikubali kujiuzulu? Kwa nini alishindwa kusimamia Wizara ya Madini kama PM?

Wananchi wachache sana wanaweza kuchambua mambo hivyo.

Lowassa alivyojiuzulu, Rais George Bush aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kuliondoa jizi hilo Lowassa. Alisema kitu kuipongeza Tanzania "for getting rid of that crook".

Ndivyo ilivyoeleweka hata kimataifa huko. Ndivyo wananchi wengi walivyoelewa, Lowassa fisadi kajiuzulu.

Sasa Tanzania ingeonekana vipi ikiwa "that crook" anarudi kuwa rais na Kikwete anampigia kampeni?

Ingeonekana kumbe haya yote maigizo ya Pwagu na Pwaguzi, hawa wote majambazi tu yanatuchezea akili.

Ndicho Kikwete alichokataa hicho.

Kwenye siasa, hata kama umejiuzulu kwa sababu wewe kiongozi tu, hukushiriki moja kwa moja, optics, imagery matters.
 
Unanishangaza unavyoamini kupitiliza maneno ya JK, mpaka unajigeuza kabisa kuwa kama msemaji wake!.

Angekuwa haogopi maneno yule;

- Asingehangaika kumtuma Makonda akampige ngumi Mzee Warioba wakati wa utawala wake.

- Asingehangaika kuyavuruga maandamano ya Chadema kule Arusha, kwa kutumia polisi na kuwaumiza waandamanaji.

- Wala asingehangaika kumteka Dr. Ulimboka, aliyekuwa akipigania haki za madaktari, akaokotwa ameumizwa kwenye msitu wa Mabwepande, wakati ule wa utawala wake.

Hapo hakuna cha Saigon wala upepo.... tafakari. Anawadanganya na wenzio kwa maneno matupu, mnadanganyika, huku chini chini anachukua hatua kwa vitendo, ndicho alichomfanya Lowassa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hiyo ya 2015 labda ilikuwa CCM tofauti kabisa na ile ya 2020, ngoja tuone ya 2025 itakavyokuwa.
Tutaona.

2025 si "Mama" anamalizia, au kuna nani mwingine tena?

Mkuu,

Kabla ya uchaguzi wa 2005 mimi nilikuwa nakaa na January katika "smart set" yetu na kina Rev. Kishoka, tunazungumza kampeni. Tukawa tunajadili nani anafaa kuwa rais.

January akaomba udhuru asichangie mada hiyo kwa sababu yeye ana mgombea wake wa karibu sana in real life, atakuwa biased, next thing I know, January karudi Bongo namuona anazunguka na Kikwete nchi nzima kumuombea kura, kujibu hoja, kupanga mikakati. Watu wanazunguka nchi nzima.

Hawa watu wanaozunguka nchi nzima ni lazima wawe strategic katika kumchagua mgombea wao, wakiwa na option ya mtu mwenye urahisi kumnadi, of course watachagua hiyo.
 
 

Kwanini wafanye biashara kwenye mali ambayo sio ya kwao? Tanzania si mali binafsi ya mtu yoyote. Ni ya watanzania.

Wote walifanya makosa kama kweli walikubaliana hivyo. Na lazima itakuwa shubiri sababu ilikuwa biashara ya upatu
 

Hawa watu walikuwa wanafanya biashara ya upatu πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Tatizo haya mnayaongea ninyi mkifikiri kila mtu anatumia namna kama zenu ku handle life dissapointents.
Mzee unaweza kuta anaishi happy tu.
 
Hahaha hahaha halafu sasa watu wanataka tuamini wale wanayoamini wao, ukiwapa story za Kitaa za upande mwingine hawataki wakati zote ni "hearsay" tu za vijiweni

Humu kuna mtu anaweza hata kukublock eti kisa umembishia Jambo fulani ambalo hata ushahidi nao Hana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…