Kwa documentary ya Pele hii iliyotoka nitakuwa mpuuzi kuendelea kumlinganisha na watoto wadogo kina Messi

Mkuu hivi mwaka 1999 ukiwauliza wangapi walikuwa wamemuona pele akicheza si ungepata 10 tu ila maradona kastaafu 1994 hivyo mamillion walikuwa wamemshuhudia ndio maana akashinda kura zilizopigwa na mashabiki

Ila walipokaa jopo la fifa lililojaa wataalam wa soka na utafiti na makocha wazoefu wakaja na hitimisho kwamba hakuna kama MFALME PELE
 

Attachments

  • Screenshot_2018-02-01-09-40-35.png
    219.8 KB · Views: 59
Hao FIFA wasijitoe fahamu, ligi hapa ni nani zaidi kati ya PELE na MARADONA..

Wasituletee ushindani na hawa wachezaji walio vishwa PEMPASI utotoni..!
 
 
Ukweli Mchungu ni kua Maradona ameshamshinda Pele waliposhindanishwa
Waliposhindanishwa wapi? Unamaanisha walikuwa uwanjani wawili tu halafu Maradona akashinda au? Mi najua ubora unaonekana uwanjani na si pahala pengine.
 
1. Hoja ya kwamba pele alizungukwa na mastaa hivyo alitembelea kivuli chao nachoshangaa hujiulizi maradona kacheza world cup 1982 ndani ya kikosi ambacho kilikuwa kimechukua world cup miaka 4 nyuma sasa kma hoja ni mastar kivp argentina nayo yale yale tu je na mmi nikisema alitembelea nyota ya mastaa kma jorge valdano, santa maria na mario kempes waliokuwa hot cake enzi hizo

Hata world cup ya 1986 maradona kombe zima hakuwa na impact ila kaja kuwika kuanzia robo fainali hivyo group stages alibebwa na njemba kama kipa nelly pumpido na beki matata kma ruggeri ambaye ni beki bora katioa histoia ya argentina na kina ricardo giusti ukuta ulieruhusu mabao 5 tu kombe zima (3 mtoano) huko mbele ndio usiseme walikuwepo kina valdano aliyekuwa mchezaji bora wa la liga mwa huo huo..... Alikuwepo buruchugga aliyetupia mpaka fainali na kuwapa kombe alikuwepo pia kina hector henrique alafu ndio unataka kusema maradona alikuwa anaibeba timu mwenyewe????

2. Kuhusu ubingwa napoli ...... Pele naye alichukua ubingwa wa ligi mara 6 na santos na mmoja akiwa marekani na NY cosmos jumla ana kombe la ligi 7..... Champions league la America ya kusini (copa libertadores) kachukua mara mbili mfululizo tena akibeba na club world cup la enzi hizo yaani intercontinental cup nalo mara mbili mfululizo.... World cup ndio usiseme amechukua mara 3 kati ya 4 alizoshiriki

3. Kuhusu magoli obvious pele humkuti kwanza ameweka rekodi ambayo sijui nani ataivunja ya hat trick 92!!! Pia ana rekodi ya ratio ya magoli msimu mmoja kuna msimu alicheza mechi 30 akapata goli 59 ilikuwa msimu wa mwaka 1965 kma sikosei hivi nani anaweza sahivi mechi chache hivo goli za kumwaga...... Kingine pele ana magoli zaidi ya 1000 ilihali maradona akijumuisha magoli yake na assist na red card alizowahi pewa kwa kupigana uwamjani bado hafikii hata nusu ya magoli aliofunga pele

Anyway nyie mnaomtetea maradona mnaweza kutuambia amemzidi nini pele
 
Ronaldinho ni mtu mwingine Yule ,
Labda kwasababu nimemuona Ronaldinho live akicheza kipindi yuko Barcelona wakati akiwa kwenye peak! Kwa kifupi yule jamaa ni BEAST.....MNYAMA WA HATARI!
 
Documentary inaitwaje? Inapatikana wapi?

Hii video ya YouTube ya dakika 6 ndo unaita documentary?
 
Maongezi mengi lakini hayazungumzii soka. Ukiwasifu Uingereza ndo unakuwa sio mchezaji bora? Sema Fulani anamshinda fulani kwa sababu kadhaa, sio ngonjera
 
Kuna kosa la msingi tunalifanya, huwezi linganisha uchezaji Wa wakati huo(very local-hakuna off side,yaani utadhani watoto wanacheza) na modern days football

Waliofanya mpira kuwa maisha yao (professional footballer s) ambao hiyo documentary sio kwamba wameiona Leo au Jana ,wanayo siku zote, wanajua mkali ni nani na kwa nini.

In short hata ukichukua highlight za matukio makali ya kichuya yanaweza kumzidi CR7 kwa mbali sana lakini haibadili ukweli kuwa cr7 ni mkali kuliko Kichuya
 
Walikuwepo, wapo na watakuwepo wachezaji wa kila namna lakini kwangu sijawahi ona wa Aina ya Ronaldinho Gaucho
 
Lol [emoji15] [emoji15] ficha ujinga toka lini mtu ukafundishwa dribing?
wewe ndo ungeficha ujinga wango..tunaofundisha watoto soka tunawafundisha dribling..tunatumia cones na mbinu zingine
 
Hujaona 1 ni maradona au kusoma hujui?
Nimeshasema hizo ni kura za washabiki tu ila WATAALAM walioteuliwa na FIFA kwa sauti moja walimpa tuzo Pele sasa unachobisha ni nini..... Hivi mashabiki wanafaham mpira kuliko wataalam???
 
Hapana mkuu enzi hizo mpira ulikuwa mgumu shida sio offside tu

Kumbuka hakukuwa na sub kma siku hizi yaani akiumia mmoja mnacheza 10

Hakukuwa na red card kufikia miaka ya 50 hivyo unapigwa buti na hakuna kutolewa mtu unafkiri sahvi ingekuwa hakuna red card mpira ungekuwaje???

Hakukuwa na penalty baada ya extra time yaani enzi hizo mkidraw mechi inarudiwa kesho asbuhi..... Nakumbuka poland vs Brazil nliona ESPN classics mechi iliisha 4-4 ikarudiwa kesho yake asubuhi ndio brazil akapita kwa 2-1 hivi hawa watoto wa sahivi kina messi wangeweza bila penalty??

Anyway yako mengi ambayo wa enzi hizo walikosa na ssa mnayapata sasa nashangaa unapong'ang'ania offside unasahau na wao walikosa mengi kma nlivyoainisha hapo juu
 
Awe unauelewa mpira
 
Ndyo uone favor kwa kura alipigwa akaandaa vibaka wenzie wakampa tuzo
Sio FIFA tu mpaka shirikisho la mpira la wachezaji wa zamani lilimpa tuzo PELE kma bora wa karne

Kwa ufupi taasisi zaidi ya 10 zilimpa pele kama mchezaji bora wa karne kuanzia shirika la habari Reuters mpaka UNICEF hadi kamati ya olimpiki IOC ilimtangaza sio tu mchezaji bora wa mpira bali mwanamichezo wa karne akiwashinda magwiji kama muhamad ali michael Schumacher na michael jordan kwahiyo hata kma fifa wangempa maradona bado pele angemfunika kwingine kote

Acheni mfalme aitwe mfalme hao kina maradona watasubiri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…