Yaani nashukuru cdm waligoma kuungana na huyu mzee wa ccm, vinginevyo hii idadi ya watu anaopata Lisu, ccm wangesema cdm ilikuwa imekufa, lakini uwepo wa Membe ndio umeleta watu. Kuna watu huwa ninawaambia kabisa hata mafuriko ya Lowassa hayakumfuta Lowassa, bali Lowassa ndio alifuata kundi la mabadiliko ambalo liko cdm. Iwapo Lowassa angekosea ile 2015 aende chama kingine nje ya cdm, angepata aibu kuliko hii ya Membe. Hata sifa wanayopata ACT ni kwa ajili ya uwepo wa Maalim Seif huko Zanzibar. Wafuasi wa upinzani wa kweli wako cdm kwa huku bara. Ile nyomi ya Membe kule Zanzibar alitembelea nyota ya Seif, ukweli huu Zito alikuwa anaujua ndio maana alikuwa anang'ang'ania muungano na cdm huku bara.