Kwa hali hii naamini maneno ya Askofu Gwajima kuwa viongozi wamehongwa ili chanjo ije

Yaani kila nikiskia waswahili wanabeza kuhusu chanjo nacheka mnooo, adi leo tungekua tuliisha wote
Tatizo umeuza akili yako kwa weupe....Kwani uliambiwa tunaishi kwa hisani ya mzungu?
 
Kuna watu wakisikia mzungu wanapagawa. Achana nao mkuu
 
Reactions: Ame
kwenye paragraph ya kwanza. technology ime advance. you dont have to wait 10yrs anymore.
hao hao wataalam, ndio hao hao walo ruhusu chanjo kutumika. unless ni wataalam wa sehem nyingine
 
Unajua kwanini alijitoa UN na nchi yake huyo Jamaa wa Madagascar?

Unajua aliyakinisha kiasi gani huo uchafu wa WHO?

Unajua jinsi gani tumepona na hizo nyungu?
Wengine hatuamini katika nyungu, tunaamini kuwa nyungu ni kazi ya shetani kama ilivyo corona,na kamwe hatuko tayari kupigwa nyungu,ndio maana serekali imetoa hiyari ya mtu kwenda kuchanja corona asiyetaka aendelee na nyungu zake,tusiyo amini katika nyungu tukachanjwe,wewe Gwajima na wenzako ambao mnapinga chanjo semeni ni njia gani mbadala tutumie siye ambaye hatuamini katika nyunguu?.
 
kwenye paragraph ya kwanza. technology ime advance. you dont have to wait 10yrs anymore.
hao hao wataalam, ndio hao hao walo ruhusu chanjo kutumika. unless ni wataalam wa sehem nyingine
Sawa na hao hao wataalamu ndiyo walioutengeneza UKIMWI maabara ili watuuzie madawa ya CD 4 kwaajili ya biashara zao, tufe na huo ugonjwa ili waendelee kututawala vizuri zaidi.
 
Wanasema eti waliochanjwa hizo chanjo miaka ya 1985 hadi 90 wengi ni wafupii [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Go and ask this question to Saudi Arabia government, by the way it is not the only country that reject China’s vaccine.
I ask you based on your allegation made here in this forum.
Go and ask this question to Saudi Arabia government, by the way it is not the only country that reject China’s vaccine.
I ask you based on your uttarance made here in this forum, because Saudi govt refutes what you try to covince people here.
 
Tokwa na hilo pepo chafu wewe, unajua kwanini Mungu alimuumba Adam akamuweka aishi bustanini Eden na ailime na kuitunza?

Unaelewa kiasi gani kuwa tiba na afya yako imejikita ktk miti, matunda, mimea na mazao?

Babu na Bibi zako hawakutumia hizo tiba mitishamba, waliishi miaka mingapi, waliibukiwa na magonjwa ya kiholela holela kama hiki kizazi chetu?

Unajua hata hizo dawa za Hospitalini zinatokana na mitishamba isipokuwa zinaundaa ktk mfumo wa kemikali ili zipate kudumu kwa muda mrefu na ziweze kubebeka na kuwekwa ktk mtiririko mzuri wa kuzitumia?

Ninyi ndiyo mnahitaji sana kufanyiwa maombi, Mungu akusaidie ili uwe na hekima.
 
Hao wanaopata mionzi na ARVs,walisha athirika tiyari ila wanasogeza siku,Sasa kama me sina athali yeyote kwanini nidungwe kitu ambacho sina uakika nacho kama kinaniponya?
 
kama umri wako haujaenda sana ...jitahidi urudi shule 🙄 🙄 🙄 🙄
 
Kwahiyo tuendelee kukubali kudhuriwa?
 
Acha uongo wazee wangu wamepiga sana malimao na nyungu za kutosha, ila waliponea ICU tena nje ya nchi!!

Hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa nyungu inaponya Covid 19.

Having said that, mlikuwa wapi wakati mabeberu wanatengeneza chanjo? Kwanini tusingetengeneza za kwetu ambazo hazina sumu?
 
Ndio, madhara yake ya muda mfupi (chini ya miaka mi5), muda wa kati (miaka mi5) na ya muda mrefu (miaka 10) hayafahamiki.
Kwanini hatukutengeneza za kwetu ambazo hazina sumu? Huwa mnamsifia JPM kuwa aliikataa chanjo ya mebebru mnasahau kuwa alikua anatumia mashine ya beberu kusukuma damu!!

Katika vitu ambavyo JPM aliingia chaka ni Covid 19...... Kwanini hakutengeneza chanjo za hapa hapa?? Au hta aombe licence waje watengenezee hapa hapa kwetu ili tumonitor kila stage?
 
Hao wanaopata mionzi na ARVs,walisha athirika tiyari ila wanasogeza siku,Sasa kama me sina athali yeyote kwanini nidungwe kitu ambacho sina uakika nacho kama kinaniponya?
Umeambiwa priority ni watu wazima ambao immune zipo chini na mtu mwenye magonjwa nyemelezi. Unaweza ona chanjo haina faida ila kma una hypertension ambayo huijui Covid 19 ikipita yaani hutokohoa wala kutapika bali tunakuzika asbuhi tu.

Alternatively Unaweza usione kma una athari lakini unajua unaweza muua baba au mjomba wako mzee sababu tu hujachanjwa??

Kwanini tunakua na hoja za ubinafsi hivi?
 
Kisa unakula nyama ya ng’ombe haimaanishi unywe na mkojo wake, bogus!
 
Una uhakika aina ya vihusika vya chanjo ndivyo hivyo hivyo unavyoletewa wewe?

Hivi dunia nzima ni COVID 19 ndiyo gonjwa pekee linaloua watu ilihali Kansa, TB, UKIMWI n.k hayatuui?

Umeshachanjwa tahadhari ya kazi gani tena?
Si kamati iliundwa kuchunguza unadhani hawakufanya random sampling ya sample za chanjo? Labda wewe uniambie sample za kuja Africa na ulaya zina tofauti gani maana manufacturer wa J & J au AtsraZeneca ni wale wale!!

2.Chanjo ya UKIMWI mbona inafanyiwa majaribio tokea 2007... Ila Covid 19 chanjo imetafutwa faster sababu ni kirusi emerging na kasi yake ya kusambaa na fatality rate ni zaidi ya hayo uliyotaja. So usilinganishe kabisa.

3. Tahadhari coz sio dawa zote zitamkubali kila mtu. Hata mimi huwa nikitumia panadol huwa nawashwa sana ngozi na kichwa kinaongezeka tu kuuma. Ndio maana nlikupa mfano wa Israel wao wamechanjwa zaidi ya 70% ndio maana barakoa sio lazima wala tahadhari wala sio issue coz karibu kila mtu kachanjwa so risk ni ndogo.
 
Kisa unakula nyama ya ng’ombe haimaanishi unywe na mkojo wake, bogus!
Si alisema mumtegemee Mungu kwanini yeye alitegemea mzungu ndio amsaidie kusukuma damu? Ina maana alikua anamfundisha mungu jinsi ya kuendesha mwili wa binadamu??

Ila nyie misukule wake aliwaaminisha msitumie chanjo ila mumtegemee Mungu utadhani hakuna wagonjwa wanaoenda hospitali wanaomcha Mungu.
 
Mimi siamini hizo issue za wazungu kutaka kutuuwa waafrika lakini sio sahihi kusema kuwa et wangetaka kutuuwa wangekuwa washatumaliza kwa sababu et tunatumia madawa na machano yao mengine.
 
Ach Wafuasi wa Gwajima acheni maneno mengi tunaopingana na mtazamo wenu tuwe na pepo mchafu tusiwe na pepo mchafu twambieni ni njia gani mbadala tutumie tusioamini katika kupiga nyungu,halafu kama mnajua kuwa hata madawa yanatokana na mitishamba kwa nini mpinge chanjo wakati ni sehemu ya miti shamba?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…