Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu

Lakini wote walianza kwa kutokujua kitu ndio wakajua kwa hiyo hakuna hoja hapo.
 

1: Ukiona unashauriwa hivyo, basi ujue mtoa huduma ya afya uwezo wake wa kufikiri ndi umefika kikomi. Ingawa haimaanishi kuwa huwezi kusaidika huko mbele, ndio maana kuna referral systems. Inawezekana kimaarifa kazi imekuwa pevu au kiteknolojia pia. Sasa hao hujiongeza kulingana na ubinadamu na asili yetu na mambo ya imani.

2: Njia za uzazi wa mpango zaweza kutokumfaa mtu kulingana na hali yake ya kiafya aliyonayo. Kila njia inaelezwa uzuri vs ubaya na kiasi cha uhakika. Suala la kuchagua ni la mteja baada ya kuelezwa yote hayo. Hivyo, wakati mwingine ni suala la personality/unafiki ya kutokuwa wazi. Kama A haikufai nitakueleza na kwa nini, kama inasemwa usitumie zaidi ya miaka mitano nitakueleza.
 
Na Mimi nakuambia Kwa uzoefu.

Ukiona moja Kati ya hao hawajui kingereza basi jua wanajua kihispania, kireno au kifaransa.

Zingatia; wengi wao sio wote
Mbona kigeugeu Kama popobawa?, Mara kiingereza mara kireno mara kispain. Tuchukue lipi tuache lipi?. Acha kulimbukia lugha za watu, kwani kiingereza ndiyo kinatibu?. Basi usiende hospitali za Kitanzania katibiwe Uingereza, Ureno au Spain. Ushamba tu unakusumbua.
 
Juzi nilikua hospital, hao vijana wameshindwa choma/ weka ile kanule mara 3, anakuja huyu mara yule. Nilijaa sumu kwa mgonjwa wangu

Hivi ni vitu ambavyo hutokea kwa yeyote:
1: Anaweza kushindwa daktari/MD nesi anaweza na kinyume chake.
2: Anaweza kushindwa daktari bingwa wa usingizi, MD au nesi au ward attendant akakuwekea. Haya mambo yaoneni tu yalivyo, siyo ABCD....
Ni mambo yanahitaji ushirikiano na kuheshimiana sana, thamini mchango wa kila mmoja pale.

NB: Unaweza kusikia, furani angekuwepo tusingepata shida, kumbe ni health attendant. Nawe utasema muiteni basi kumbe hujui ndo huku unaona hana maana.
 
Unaweza
Unaweza kuwaza hivyo, lakini si wote wenye D4 ni uwezo wao wa mwisho. Tunapata matokeo hayo baada ya mambo/factors nyingi. Huwezi kumwona mtu hawezi kwa kuona D4 bila kuhua aliipataje.

Mbona haujajiuliza miaka 60 ya uhuru Tanzania one yeyote aliyefanya kitu cha mfano zaidi ya yale matokeo ni yupi??
 
Hii fani imevamiwa na makanjanja mkuu....hulifahamu hilo watakucheka watu😂😂😂
 
Tufanyaje sasa?
Tuboreshe mfumo wetu wa elimu from the scratch ambapo tuandae vijana wenye uwezo wa kuelewa na siyo Kukariri.
Nakumbuka kipindi niko o level tulikuwa tunaambiwa tukariri ili tufaulu mitihani, that's the problem halafu unapata credit za kwenda chuo kwa matokeo ya Kukariri.
Kwenye kiingereza tuache kuprint dictionary za English to swahili tujikite kwenye English verbs to English translation zile za English - swahili zinakaririsha tu
 


Huwezi elewa concept ninayoizungumzia Hapa.

Kingereza ñdio lugha ya kitaaluma na kufundishia na kujifunzia hapa nchini ulitaka nisemeje?
 

Mkuu unaongea points saana sema wadau wamekaza fuvu hawataka kukubaliana na ukweli
 
Kama mtu ni PhD holder anasema taki fosi( task force) unadhani hao form 6 mkuu watakuwaje?
 
Wao darasani walikuwa wanameza nondo tu za kujibia mitihani, wanasemaga Kingereza waachie watu Wa Arts..
 
Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.

Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.

Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza
Hao madaktari hawajui Kuandika Kiingereza,Kusoma Kiingereza au Kuzungumza Kiingereza?. Kuwa specific tafadhali. Lipi hapo?

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Hata jiwe kwake kilikuwa kigumu kukielewa japo cha kibongo bongo kipooooooooooo!!!!!!!!
 
Mbona Mtoa Mada ameweka kila kitu wazi kabisa? sijui kwanini watu wana vichwa vigumu kuelewa... Ngoja nimsaidie

Kwa nchi yetu.. Tanzania, English ndo lugha inayotumika kufundisha, vitabu vyote vipo katika lugha hii, machapisho n.k hivyo kitendo cha kukutana na mtu anaejiita mtaalamu katika fani fulani (Daktari) halafu english inampiga chenga kiukweli kabisa ni swala la kujiuliza na mara nyingi huwa amefika hatua hio kwa kukariri = sio daktari mzuri. Unaongea na daktari hawezi hata kuwasilisha taarifa kwa Kingereza halafu unaamini kabisa kasoma molecular structure akaielewa?? [emoji23][emoji23]

Mataifa yaliyoendelea yana mifumo ya kutafsiri vitabu na machapisho kwa lugha zao. hata waandishi wanaandika kwa lugha zao. Urusi mfano hata "Google" haipo.. wana system zao, china hamna whatsApp n.k nimetaja hivi kuonesha namna walivyo independent.
 
Kama daktari anaweza kuokoa maisha kingereza kinasaidia nini?, Nenda China, urusi, Spain, uarabuni, uone Kama kuna mtu anahusudu kingereza.
Ushaambiwa material zetu za udaktari zimeandikwa kwa kiingereza, hao unaowataja wanavitabu vyao vilivyoandikwa kwa lugha zao, elewa basi.
 
Sijawahi kuona watu wanaongea kiingereza kibovu tena kwa lafudhi mbovu kama waGanda
 
Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.

Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.

Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza
Mi nadhani mother tongue ndio inaathiri kiiingereza cha mtu!sio kila mtu anaweza kuongea pure english mf.kenyans kile sio kiiingereza bali ni lugha zao za asili the same to Nigerians!!!mfano A sukuma can't speak like an englishman!mi nadhani swala la kiiingereza ni pana Sana kuliko tunavofikiri!!halafu kiiingereza cha kuongea mtu sio sawa na cha kuandika wala cha kuelewa maana halisi ya maneno yenyewe!!inaweza ukawa mzuri kwenye kuandika na kuelewa lakini lafudhi ikawa sio!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…