Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
- Thread starter
- #41
Tanzania ni yetu sote unadhani huko Simanjiro na kiteto wanakaa ng'ombe, hivyo hawastaili miundombinu kama sehemu zngineUlitaka mtu apeleke yutong simanjiro au kiteto
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tanzania ni yetu sote unadhani huko Simanjiro na kiteto wanakaa ng'ombe, hivyo hawastaili miundombinu kama sehemu zngineUlitaka mtu apeleke yutong simanjiro au kiteto
Dah. Na wewe unasemaga una akili?Maisha ya watu wa mikoani magumu Sana...
😂😄...Dah. Na wewe unasemaga una akili?
nyie wanaume wa dar mnatabu🤣Maisha ya watu wa mikoani magumu Sana...
Upo sahihi kabisa,kuanzia stand yenyewe ni takataka kwa jiji km hili la wadhungu,nyumba za ajabu za kizamani katkati ya jiji,mitaa wa nyuma hovyo, mbele magorofa ya maana,nyuma nyumba za matope ni aibu sana,anzia pale HQ za TANAPA mpk mataa ya mbaunda nyumba za ajabu.Sijui Clinton alifikaje pale Cultural Hertage duka la vinyago mpk aseme eti Arusha ni Geneva of Africa,wazungu ni wanafiki kweliYero subahi wanangu wa ngaramtoni, mbauda, ngalimi na sanawari, mtu akisikia unasafiri unaelekea arusha kichwani anakuhusudu kama mtu anayeelekea.
Geneva ya kibongobongo mawazo yake ni sahihi isipokuwa atokuwa sawa akidhania ya kuwa pia unafaidi raha ya kusafiri kwa usafiri wenye comfort na luxury zote za mabasi kama waendao kwenye majiji mengine nchini.
Kiufupi ukisikia kuna Kenya ndogo inayoexist ndani ya Tanzania na hata watu wake hawakijui vizuri kiswahili karibia hapa penye stendi ugly ilojaa malori(fuso,scania na Isuzu).
Malori haya yalobadilishwa matumizi na kubambikiwa show ya mabasi a.k.a chinjachinja, saga kunguni au mabasi ya vijijini au kwenye minada ya ng'ombe yapo katikati ya jiji yakipakia abiria wasokuwa na hatia tayari kwa kuwatia tetenasi na nauli zao zisizo za kutabirika kuelekea DSM, Mwanza, Musoma, Tanga n.k.
Sasa usiguse hayo mangorika,sijuhi mtei, AM coach, coast n.k utaghahirisha safari yako bure ya kutoka nje ya jiji letu pendwa la utalii bado kwenye vi-hiace ndo balaa usisemee hilo vumbi na vuruge lake hapo ngarenaro stendi mbaya kama zizi la mbuzi haina hata vibao angalau kuindicate uelekeo au mitaa.
Kiufupi Arusha katika upande wa usafiri wa abiria kwa njia ya barabara mnaiaibisha Tanzania be modern bwana mbona mji mdogo kama Tarime umeweza na unamabasi mazuri ya wazawa na mengi pengine kuliko makao makuu ya mikoa mingi nchini na usafiri kule ni uhakika muda wote.
Achilia mbali mabasi yao hayana sura mbaya za kuchongwa na kubadilishiwa matumizi ya mizigo kuwa ya wanadamu ebu tafadhali tuwe japo kidogo na utu na huruma maana tunawaonea sana ndugu zetu wamasaai wanaoenda monduli, kiteto kibaya, simanjiro mirerani,tarakea rombo n.k.
Inawabidi walale guest za city center huku wakigeuka walinzi wakiofia kuachwa na mafuso haya yanayodamka usiku usiku huku yamepakia watu kama kuku usawa huu kweli katika karne ya 21 bado watu.
Wanapakia mizigo na mifugo juu ya carrier/bodi nimewapa mfano mdogo wa Tarime wala msijiangaishe kwenda miji mikubwa au kuomba msaada kwingine kawaulizeni kaka zenu wadogo wamewezaje maana.
Mnatuaibisha wenzenu tunawavumilia mpaka tumewashiba tafadhali wamiliki wakale na wakazi wa jiji pendwa la arusha haya mabasi myatenge na msiwe mnayapanda hili wamiliki na serikali wabadilike miundombinu iboreshwe.
Pamoja na magari yenyewe, haiwezekani wengine daily wanapanda vya kuimport luxury and modern japo tulitamani vingeundwa hapa hapa nchini lakini sisi tunakomaa na mamoshi.
Uchafuzi wa mazingira na uchafuzi wa mandhari ya jiji mwishowe watalii waogope kuzuru nchini kwa kutishwa na mabasi yenye sura nzito ka ya mpoto pili yanaifanya nchi yetu iwe na taswira ya mabasi pendwa ya nchi jirani.