Kwa hili Arusha mnatuaibisha Watanzania

Mtoa mada ana hoja ya msingi aisee, yaani huwa nikirudi home Chuga naanza kuujutia urefu wangu. Hiace utadhani umekaa kwenye kigoda huku magoti yamebanwa na seats; basi likiingia stendi mpaka kupaki ni karibu nusu saa yaani mara nyingine ni bora ushukie kabla ya stand uchukue tax kuliko ile jam ya kuingia stendi, wapiga debe wanazingua, na ukienda kule Kilombero kiangazi ni vumbi na masika ni madimbwi ya kutosha. Kiufupi kuna changamoto kubwa ya usafiri kwenye hili jiji.
 
Upo sahihi kabisa,kuanzia stand yenyewe ni takataka kwa jiji km hili la wadhungu,nyumba za ajabu za kizamani katkati ya jiji,mitaa wa nyuma hovyo, mbele magorofa ya maana,nyuma nyumba za matope ni aibu sana,anzia pale HQ za TANAPA mpk mataa ya mbaunda nyumba za ajabu.Sijui Clinton alifikaje pale Cultural Hertage duka la vinyago mpk aseme eti Arusha ni Geneva of Africa,wazungu ni wanafiki kweli

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…