Kwa hili la mwaka mmoja wa kifo cha Magufuli, Kanisa Katoliki linapaswa kuona aibu

Pambana na dhambi zako kanisa halita kusaidia , na kamwe halitaona aibu na maisha yataendelea.
Dini haziwaongozi watu kwenda mbinguni tu bali huwafanya watawalike kirahisi pia watawala hupenda kuona dini zikiwasaidia kutawala na maandiko yanasema tutii mamlaka kwa vile hutoka kwa Mungu.
So complex.
 
Ndugu,
Lakini Wakristo hawatakiwi kuwa WANAFIKI kama walivyokuwa Mafarisayo wa wakati wa Yesu.
Unamuaibisha mwenye jina hilo ambae alikuwa imara na mkweli asiyeyumba.
Ukiniita mimi mnafiki Tundu Lisu na Freeman Mbowe wanaoongea Lugha ya CCM hivi sasa sijui utawaitaje?
 
Hao hawahusiki hapa. Acha kuokoteza cha kuongea. Mwenye jina hilo hakuwa hivyo.
Nimekupa mfano wa Wanafiki HAI.

Mchana Chadema usiku wanaomba " Mafao na Misamaha" CCM

Hahahaaaa........ Endelea kushangilia hapo hapo banda la mkaa jirani na ofisi ya Mange!
 
Mimi ni moatoliki, lakini h

awa maaskofu wetu kwa unafiki siwawezi. Hata askofu Nyaisonga kuwa rais wa tec, hawakuzingatia vigezo vingine zaidi ya kuwa mwendazake alikuwa rafiki mkubwa wa huyu askofu.
Kwani Mwenyekiti wa TEC anapaswa kuwa na vigezo gani? Askofu (Mkuu) Nyaisonga hana hivyo vigezo?
 
Yesu Amewafundisha Wakatoliki hivi!
[emoji1370][emoji1370]
Mathayo 5
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;

44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

48 Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Usipo Yafuata na Kuyaishi Mafundisho yake ww sio Mfuasi wake!
 
Suala si kuazimisha kwa ajili yake hapo,......hapo issue ni kuazimisha kumuonyesha aliyopo kuwa 'hatukukubali kiviiile kwa kuwa si mwenzetu'!.
 
Mie nilijua utazungumza kuhusu uwajibikaji serikalini, miundombinu, uzalendo nk. Chacha wange alikufa kwenye ajali ya utata je mbowe alihusika?

Kaka yake mbowe alikufa, je chadema walimuua? Suala la kifo lipo tu ata ungefanya nini.

Alphonse mawazo alikufa kipindi magufuli akiwa madarakani, yule mwandishi wa channel 10 aliyefia iringa je?

Alikufa wakati wa magufuli, kipigo na vifo mtwara wakiandamana kuhusu gesi na mafuta ilikua kipindi cha Magu?

Tuseme kweli, Magu hakuwaita upinzani ikulu kunywa chai, hyo ndio walikasirika. Sasa wameitwa ikulu ni mapambio na kusifu.
 
Ukumbuke kuwa kwa Imani ya katoliki kupokea sakramenti sio kigezo peekee cua kufika Mbinguni. Yesu alisema: 'Aulae mwili wangu bila kustahili anakula hukumu yake mwenyewe'.
Wewe naye kiazi kwelikweli.

Ukiambiwa mtu amepokea Sakramenti kabla ya kufa maana yake amepewa Sakramenti ya Kitubio, Mpako wa Wagonjwa na Ekaristi Takatifu.

In other words, mtu kama huyo ni msafi kwelikweli. Hapo ni mbinguni moja kwa moja unless hapo katikati afanye dhambi ndogo ndio itabidi apitie toharani kwa ajili ya malipizi. considering his health at his death, this is very unlikely.

Nyie ndio Wakatoliki mnaoyumbishwa kwa kutoijua imani yetu vema. Mnatuaibisha sana.
 
ndugu kanisa halilipi kisasi hata maandiko yanasema kisasi si juu ya mwanadamu.kanisa linaamini katika kusamehe na hukumu anaachiwa Mungu sababu ndiye anyejua yaliyopo ndani ya kila mwanadamu.
 
Hivi nyie Ukatoliki wenu mliupata kwa kufuata hatua zote ikiwemo mafundisho? No wonder mkipata challenges tu kidogo kuwa mnaabudu sanamu, mnamuabudu Bikra Maria, mara ooh sijui Papa ni Freemason mnateteleka. Inasikitisha sana.

Nimeshuhudia kanisa hilohilo likihukumu wafu kwa kudai kwamba hakuwa amefunga ndoa, alikuwa na suria, alikuwa hashiriki jumuiya nk; wakati hapohapo likiwatunuku sakramenti hizohizo walevi na majambazi!
Mama Kanisa hayupo hapa kuhukumu mtu yeyote. Ili mtu ustahili kitu fulani, siyo Kanisani pekee hata katika maisha, lazima uwe na vigezo.

• Ukijinyonga maana yake umemkufuru Roho Mtakatifu kwa kukata kwako tamaa and so automatically umejitenga na Mungu na Kanisa. Hatuwezi kukuzika.

• Ukiishi na mtu kama mke ama mume wako wakati hamjafunga ndoa maana yake umeamua kujitenga na Kanisa, haustahili kupokea Sakramenti yoyote and so hatuji kukuzika.

• Tumeagizwa kuishi kwa umoja na mshikamano. Unapoamua kujitenga na Jumuiya maana yake umejitenga na Kanisa. Unapojitenga na Kanisa automatically unajitenga na Mungu. Hatuwezi kuja kukuzika.

1 Yohane 4:20-21
Mtu akisema,
"Nampenda Mungu,"
naye anamchukia ndugu yake ni mwongo.
Kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
Na amri hii tumepewa na yeye:
ya kwamba yeye ampendaye Mungu,
ampende na ndugu yake.


Kwahiyo unapoamua kujitenga na Kanisa maana yake umejitenga na Mungu. Hatuwezi kuja kukuzika.

Hata hivyo, mdhambi akiamua kutubu Kanisa linampokea kwa furaha na mikono miwili, and so atapata huduma na haki zote wazistahilizo watoto wa Mungu na Kanisa.

Kuna walakini kubwa sana katika kuadhimisha uovu na waovu
Magufuli hakuwa mwovu, at least at his deathbed. Tunaamini yupo mbinguni au toharani. Ndio maana tunamuombea yeye pamoja na roho za waamini wengine marehemu waliopo toharani wapate rehema kwa Mungu wafike mbinguni mapema iwezekanavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…