Kwa hili la mzigo huu, wacha tu bandari ibinafsishwe

Kwa hili la mzigo huu, wacha tu bandari ibinafsishwe

Nina konteina kutoka china, leo ni wiki ya pili tangu meli imefika dar port ila mzigo haujashushwa, sasa hapa kuna nini? Zaidi ni tubinafsishe tu hii bandari ili tulete maendeleo hakuna njia wala namna

Wanaopinga vaeni viatu vya mfanyabiashara kwanza halafu ndio uje na point, tena ziwe fupi fupi
ni kweli ingawa kuna wa2 hawatakuelewa watakutuhumu umetumwa,ukiacha hiyo kero ya kutoshushwa,pia kuna kutengenezeana storage za ajabu kwa kujifanya systeam iko chini,alaf kina m2 anataka pesa,maofisa wa TPA,TRA,TBS,....yaani mpaka mzigo unatoka,mfanya biashara hoi,,,ndo manake wafanya biashara wanapandisha bei makusudi ili kusukumia mzigo kwa mlaji!!! cha muhimu ni kwamba serikali irectfy vipengele tata vya huu mkataba na hawa WADUBAI!!
 
Uchumi wetu utajengwa kwa Exports yaani bidhaa tunazouza nchi za nje na kuleta dollar nchini. Kwa hiyo focus nzima ya mradi wa Bandari ni kuhudumia sisi Majeta wa mali za nje..
Mkuu asante kwa kuja tena jukwaani.

Mkuu najiuliza, hivi Rais akimtoa decree kuwa

"kuanzia Sasa Tanzania itanunua bidhaa kwa hela ambayo bidhaa hiyo imetengenezwa na nchi zote zitanunua bidhaa iliyotengenezwa Tanzania kwa Tanzanian shillings, pia malipo yote nchini yatafanywa kwa fedha za Tanzania".

Ni nini kitaathirika katika kuimarisha Uchumi wa nchi yetu?
 
Kabla ya kubinafsisha, tumia hii kauli "ukitaka kumuuwa nyani usimwangalie usoni" piga chini wote wanaokwamisha mambo, hata kama ni mjomba. Swala Ni uongozi tu!! Bandari Ni yetu Watanzania, tuendeshe mambo kizalendo, majirani watupende ili tukamate pesa za kigeni.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Inaweza kuwa ni kweli, si ni binadamu, anytime unaweza kuzima,hakuna cha ajabu hapo wala uwongo
Kifo kinakuja ghafla
Na history ya mgonjwa ilionyeshwa alilazwa mhimbili na kuruhisiwa Kisha kuzidiwa Tena na kukimbizwa mzena je huko ndo kuchapa kazi?
 
Nina konteina kutoka china, leo ni wiki ya pili tangu meli imefika dar port ila mzigo haujashushwa, sasa hapa kuna nini? Zaidi ni tubinafsishe tu hii bandari ili tulete maendeleo hakuna njia wala namna

Wanaopinga vaeni viatu vya mfanyabiashara kwanza halafu ndio uje na point, tena ziwe fupi fupi
Kwa jumla, Mpango wa Serikali kufanya uwekezaji ili kuleta ufanisi ktk bandari zetu Ni mzuri. Mzuri na muhimu kabisa. Isipokuwa hili la Makubaliano na DPW ndiyo lirejewe upya. Ni wazi sisi Wabongo tumeshindwa kusimamia bandari zetu na sababu kubwa ni wizi na ufisadi. Wabongo wafanyakazi wa bandari wanakwiba pale bandarini Dar jamani! Wizi unaanzia juu kwa Kiongozi wao mkubwa kabisa hadi kwa mfagizi wa ofisi. Nina jamaa yangu tulikuwa wote ndugu zake wakamtoa tuliko wakampeleka bandarini Dar hapo kuwa kwenye kitengo fulani kinachohusika na masuala ya ukaguzi fulani hivi, baada ya miaka kama mitatu hivi alinialika nikaenda kumtembelea, ee bwana'angu ee! Ukwasi niliomkuta nao mwenyezi Mungu nisamehe; Nilimkuta na Nissan patrol mpya na alikuwa anamalizia ujenzi wa jumba la kifahari la ghorofa mbili! Nilijikatia tamaa na kudharau kusoma kwangu. Lakini nilijiuliza kwa Serikali ina upendeleo namna hii?? Jamaa alikuwa kila siku arudipo home akija na shilingi milioni kumi, ananung'unika kweli na kuniambia, aah, leo hali mbaya amepata pesa ya bia tu hata ya kumhonga kimwana haitoshi! Asijue kwangu mie kiasi kile ni mshahara wangu wa mwaka na ushehe.
Bwana, bandari ya Dar ibinafsishwe tuu tufanane. Daadeki!
 
ni kweli ingawa kuna wa2 hawatakuelewa watakutuhumu umetumwa,ukiacha hiyo kero ya kutoshushwa,pia kuna kutengenezeana storage za ajabu kwa kujifanya systeam iko chini,alaf kina m2 anataka pesa,maofisa wa TPA,TRA,TBS,....yaani mpaka mzigo unatoka,mfanya biashara hoi,,,ndo manake wafanya biashara wanapandisha bei makusudi ili kusukumia mzigo kwa mlaji!!! cha muhimu ni kwamba serikali irectfy vipengele tata vya huu mkataba na hawa WADUBAI!!
Hayo mapungufu yote hatuwezi kurekebishana wenyewe mpaka aje mtu kutoka nje? Yaani nchi imekua ngumu hivi kuisimamia mpaka tupate usaidizi kutoka nje?

Hao wanaofanya hizo vitu hawana maboss wao wa kuwawajibisha?
 
Pm majaliwa ameshalisemea hili, penye ulazima patarekebishwa kwa manufaa ya tanzania
Atarekebisha vipi wakati makubaliano yashakuwa ratified na bunge?

Atawalazimisha wabunge wakatae ratification yao ya awali na kuu ratify mkataba upya?

DP World nao watakubali hilo bila kesi ya arbitration?

Unaelewa kuwa IGA ishapita na kuibadilisha ni kesi kubwa sana na DPW?
 
Majitu mengi ya
Nina konteina kutoka china, leo ni wiki ya pili tangu meli imefika dar port ila mzigo haujashushwa, sasa hapa kuna nini? Zaidi ni tubinafsishe tu hii bandari ili tulete maendeleo hakuna njia wala namna

Wanaopinga vaeni viatu vya mfanyabiashara kwanza halafu ndio uje na point, tena ziwe fupi fupi
Majitu mengi yanayopinga hayana hoja yanapinga kwa ushabiki tu na chuki za uzanzibari v/s ubara
 
Nina konteina kutoka china, leo ni wiki ya pili tangu meli imefika dar port ila mzigo haujashushwa, sasa hapa kuna nini? Zaidi ni tubinafsishe tu hii bandari ili tulete maendeleo hakuna njia wala namna

Wanaopinga vaeni viatu vya mfanyabiashara kwanza halafu ndio uje na point, tena ziwe fupi fupi
Nani kakataa ubinafsishaji? Unajua tofauti ya kubinafsisha na kuuza nchi?
 
Back
Top Bottom