Na pia kuna tabia tunazo wa Africa kwamba mtoto wako ni lazima akusaidie, kitu ambacho hakina ulazima. Ni vema wazazi wakaandaa uzee wao vizuri na siyo kuja kutegemea fadhila za watoto wao, unless watoto wamependa wenyewe kuwasupport wazazi wao hata kama wazazi waliwalea ama hawakuwalea.
Kwa mfano huyu mzee asingekuwa na tamaa za mafanikio ya mwanae ama asingekuwa anamtafuta mwanae kwa sababu ya mafanikio, bali tu kumaliza tofauti zao, hii ingekuwa rahisi sana kusamehewa na mwanae, kuliko kumtafuta mtoto wako kisha kuanza kudai fadhila kitu ambacho si busara na hekima.