Kwa hiyo adhabu ya mafisadi ni kuwaaibisha?! Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Rais Samia

Kwa hiyo adhabu ya mafisadi ni kuwaaibisha?! Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Rais Samia

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Leo Rais Samia amesema kuwa ripoti ya CAG ijayo itaje wanaofanya vibaya ili waone aibu, hivi anatambua kuwa kuiba ni aibu tosha ambayo wameivumilia hivyo ya kutajwa ni ndogo na hawawezi kuwaza wala kustuka?


View: https://www.instagram.com/reel/DWgypeRjIYe/

Yaani mtu aibe pesa inayoweza kujenga uwanja mwingine wa mpira halafu umtaje jina kuwa aliiba hizo pesa na iishie hapo utakuwa umekomesha? Kwani wewe tangu umeanza kutajwa kwa mauaji ya Oktoba 29 umeona aibu au hujaona ili tujue kama adhabu ya aibu inatosha kwa mafisadi.

Badala ya kuongelea uwajibikaji kuwa hao watu wanastahili adhabu kali kama moja mbili tatu ili kuokoa hata masalia madogo yaliyobaki unawaza kuwaabisha au sababu nawe ni mmoja wa mafisadi ambao umekuwa ukituhumiwa ndio maana unatafuta namna ya kujipa kivuli, eti waone aibu.

Mbona wewe umehusishwa na makaa ya mawe na wengine kina Rostam na hamjaona aibu bado mnaendelea, au hiyo aibu ni mpaka.utajwe na CAG?

Hujui hata ufanye nini kama kiongozi mkuu ajabu sana!
 
Hiyo ofisi ya CAG haina hata tija kwa nchi kama adhabu zenyewe ni hizi!!!

Heri tusijue tu panapovuja kama hatuwezi kupazipa wala kuwajibishana.

NB:Hata ofisi ya CAG ikikaguliwa leo,ni madudu tupu.
 
kuna vitu ili kussuport inabidi ujitoe akili,=uwe MPUMBAVU,watu wale wale wanaotaka SAMIA ashitakiwe ICC kwa mauaji ya October 29,ndio wanaomssuport Netanyau mwenye arrest warrant ya ICC kuua raia atakavyo sababu tu Israel ni Taifa teule🤣😁😃🐒🐒🐒
 
Rais wa viwango vya chini zaidi kupata kutokea Tz, haishangazi HAKUCHAGULIWA na wananchi walio wengi!.
 
Huwa nawashangaa mnao mshangaa huyo Bibi wa Kizanzibar

Yeye mwenyewe kwa Kinywa chake alisema ndoto yake ilikuwa aje kuwa Muhudumu wa Ndege (Air Hostess)huo Urais ni kama zali la mentali tu!

Sasa mnategemea atafanya jambo gani la msingi!

Huwa nawahurumia sana watu ambao huwa mnapoteza muda wenu wa thamani kumsikiliza huyo Bibi!
 
Back
Top Bottom