Kwa hiyo adhabu ya mafisadi ni kuwaaibisha?! Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Rais Samia

Kwa hiyo adhabu ya mafisadi ni kuwaaibisha?! Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Rais Samia

Nimeshangaa mno Rais Samia aliposema kuwa Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali awataje mafisadi na akisha kuwataja wataona aibu na kujirejebisha

Badala apendekezwe mafisadi wakamatwe na wafikushwe kwenye mkono wa sheria, Rais anapendekeza adhabu ya kuwataja ili wapate aibu

Toka lini fisadi akawa na aibu

Awamu hii tumepatikana Watanganyika
 
Kwa adhabu yao kiwazomea tu haooooo
😄
Wakati mtu kwakwapua mabilion

Ova
 
Ipo shida kubwa sana miongoni mwetu ya kudhani, tuna uwezo wa kufanya kosa lolote pasipo kupata adhabu yoyote ile, sababu ni watu wakubwa...kule Ntawara wanasema huyu ntu wa system 😂 😂 😂 😂
Ndio maana inakuwa rahisi kuruhusu makosa makubwa makubwa yanayofanyika yaonekane kama mambo ya kawaida tu
 
Hii nchi kuna watu inatakiwa wanyongwe hadharani hadi kufa, kisha maiti zao nipitishwe barabara kuu ya kutoka Dar hadi Mwanza zikiwa uchi wa mnyama na ziburuzwe hadi zikatike viungo vyote vya mwili....
 
Hivi unajua kwanini waafrika tunadharaulika?
Shida sio ngozi,
Shida ni takataka kama hizi?
Bogus kabisa
 
Anaandika Mh God Godbless J Lema.

Au tutengeneze !!!

TAAKUTA.
Taasisi ya Aibu na Kusuta Tanzania

Kaulimbiu:
Aibu Kwanza, Uwajibikaji Baadaye

Dhamira:
Kuwataja hadharani wale wote wanaosababisha hasara ya fedha za umma ili waone aibu ya taifa.

Majukumu Makuu:
•Kushirikiana na Public Procurement Regulatory Authority na Prevention and Combating of Corruption Bureau kupata orodha ya wahusika
•Kutangaza majina ya “Wasutwe” kila mwaka
•Kuendesha kampeni za VIBE ya AIBU kwenye mitandao ya kijamii

Huduma Maalum:
•Aibu Index: Kipimo cha kitaifa cha nani kaaibisha zaidi
•Wall of Shame: Orodha ya wazi ya waliotajwa
•Badge ya Aibu: Cheti rasmi cha kusutwa kinachoweza kusambazwa online .

Hitimisho:
Kwa sababu wakati mwingine sheria zipo kimya…TAAKUTA inasema kwa sauti kubwa, INATOSHA.
@
 
Kama taifa tuna hasara sana, kwanza niwapongeze kwa kuwa na guts za kusikiliza hizo hotuba.
.Mimi mwenyewe nawapongeza pia, mimi nilishashindwa kusikiliza kabisa
 
Adhabu za kike ndivyo zilivyo...

Cc: Mahondaw
sio kweli, kwa hiyo anawahurumia mafisad,
Mbona Lissu yupo nyuma ya nondo hadi
kama anahurumq hivyo.
alafu nyie ndio mnaotetea ujinga kila siku mara kumuita rais Mama
mara hiyo kauli sijui adhabu ya kike
kama anajijua hana uwezo wa kuwajibisha watu asingegombea, unapokuwa Rais lazima uwe na maamuzi
 
Mwingulu anajifanya kupambana na mafisadi wakati Boss wake anataka wazomewe
 
Mama hapendi mambo ya ukali, kugombezana na kufokeana.
 
Leo Rais Samia amesema kuwa ripoti ya CAG ijayo itaje wanaofanya vibaya ili waone aibu, hivi anatambua kuwa kuiba ni aibu tosha ambayo wameivumilia hivyo ya kutajwa ni ndogo na hawawezi kuwaza wala kustuka?

View: https://www.instagram.com/reel/DWgypeRjIYe/

Yaani mtu aibe pesa inayoweza kujenga uwanja mwingine wa mpira halafu umtaje jina kuwa aliiba hizo pesa na iishie hapo utakuwa umekomesha? Kwani wewe tangu umeanza kutajwa kwa mauaji ya Oktoba 29 umeona aibu au hujaona ili tujue kama adhabu ya aibu inatosha kwa mafisadi.

Badala ya kuongelea uwajibikaji kuwa hao watu wanastahili adhabu kali kama moja mbili tatu ili kuokoa hata masalia madogo yaliyobaki unawaza kuwaabisha au sababu nawe ni mmoja wa mafisadi ambao umekuwa ukituhumiwa ndio maana unatafuta namna ya kujipa kivuli, eti waone aibu.

Mbona wewe umehusishwa na makaa ya mawe na wengine kina Rostam na hamjaona aibu bado mnaendelea, au hiyo aibu ni mpaka.utajwe na CAG?

Hujui hata ufanye nini kama kiongozi mkuu ajabu sana!

Yericko Nyerere una lipi la kusema? Au tatizo bado ni TL?
 
HELA HAIONI AIBU, AIBU WANAIPATA MASIKINI WASIO NA HELA
 
Back
Top Bottom