Uchaguzi 2020 Kwa hizi sababu Lissu anaweza kukosa sifa za kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye kumpa changamoto Mgombea wa CCM

Uchaguzi 2020 Kwa hizi sababu Lissu anaweza kukosa sifa za kupeperusha bendera ya CHADEMA kwenye kumpa changamoto Mgombea wa CCM

Na huu umri wangu sijawahi kuona Mzalendo anayewatetea Mabeberu km Lissu
Mtu mzima bila aibu mishipa imemchomoka anawatetea Mabeberu yatuibie raslimali zetu!
Tuache unafiki na chuki za u vyama lisu ni mzalendo wa kweli wa Tanganyika tatizo amegusa maslahi ya wakubwa
 
Hivi hofu juu ya Lissu ni ipi mpaka mnahangaika naye kiasi hiki? Mnadhani mnamchafua kumbe ndio kwanza mnamjenga na kumtangaza zaidi

Jr[emoji769]

Hofu ya ccm ni dhidi ya Lissu ni ya haki. Wanaccm wanajua vyema wakati mgumu aliokutana nao JK uchaguzi wa 2010 dhidi ya Dr. Slaa. Wanaccm wote wanajua udhaifu alionao Magufuli kwenye kujenga hoja, na ubora na ushawishi alionao nao Lissu, wanajua fika ccm itaenda kupoteza mvuto bandia ilioujenga kwa kutumia vyombo vya dola, kunyima uhuru wa vyombo vya habari, kundi la watu wasiojulikana nk. Hivyo hawako tayari Lissu agombee maana wanajua watajikuta kwenye wakati mgumu mno wakati wa uchaguzi, na hasa baada ya uchaguzi.
 
Mkuu Nadhani Wewe unachukua mtazamo wa mtandaoni hasa jamii forum

Ila nenda mtaani utajua balaa la Ccm

Tuombe uhai October nitakukumbusha ushindi wa kimbunga wa Ccm
CCM imekosa dira ya demokrasia sioni haja ya vitisho maana Ccm ina kila kitu hata bila vitisho wanaweza kushinda.
Waambieni wananchi mliyo fanya ni mengi hususan kwenye miundombinu hata kama mna sera mbovu bado nafasi mnayo ila hofu ndiyo imewafanya mmejenga ukatili na manyanyaso kwa kila mnayetofautiana nae
 
CHADEMA kama mnataka msidumbukie shimo kaeni mbali na lissu mtakiua chama akigombea Urais

Kwasababu Lissu amekuwa ni mtu wa jazba asiyedhibiti emotional za ndani.

Ana chuki na vyama vingine vya kisiasa na kuvidharau mfano huita CCM"maccm" yaani yeye watu wa muhimu kwake ni Chadema tu wengine ni takataka huyu moja kwa moja anakosa sifa za kuwa kiongozi

Alimdhalilisha Baba wa Taifa bungeni kwa kutoa maneno ya kejeli na kudhihaki hii haijawahi kutokea kwa kiongozi yeyote toka Nchi yetu ipate uhuru

Wakati akiwa mbunge alkuwa akiwakataza Wananchi wasichangie michango ya maendeleo jimboni kwake hali iliyopelekea shughuli za maendeleo kusimama

Wakati Rais Magufuli anatetea Watanzania juu ya madini yetu yaliyokuwa yakiporwa na Mabeberu tunajua Lissu alikuwa anawatetea watu gani

Kazi kwenu Chadema muamue msimamishe lissu mfe kabisa au muangalie watu wanaoweza kukibeba chama

Kwa maoni yangu watu kama Peter Msigwa, Lema, Nyalandu au Membe wanaweza kuonesha upinzani kwa mgombea wa CCM Rais Magufuli la sivyo mkimsimamisha Lissu hata diwani hamtapata.

Hjashawishi umma ukuelewe kwa sababu hizi, bado lissu atabaki kua mwamba wa kutuvusha katika hali ngumu hii ya maisha
 
Wanzio Chadema wamepata ujumbe wasipoufanyia kazi October hawatapata mbunge hata mmoja

Hakuna uwezekano wa cdm kukosa wabunge chini ya 50 kwa njia ya kura. Hilo toa kabisa kwenye matamanio yako.
 
Kwa hali hii itakuwa makosa kumpitisha kugombea nafasi hiyo kwani ni rahisi kujengea hoja madhaifu yake uliyoyaainisha.
 
Na huu umri wangu sijawahi kuona Mzalendo anayewatetea Mabeberu km Lissu
Mtu mzima bila aibu mishipa imemchomoka anawatetea Mabeberu yatuibie raslimali zetu!
Ngoja niendelee na kazi nikikumbuka nitakujibu nani ni mzalendo kati ya lisu na Magufuli
Kwa bahati nzuri Magufuli ni Mzilankende mwenzangu hata kama sipendi siasa za hovyo napenda Magufuli aendelee
 
Tunataka aje hata mmoja ampe changamoto Magufuli asipate 100% Magufuli apate 98%
Liasu na wote ulowataja hawana sifa za kuwa maRais wa Tanzania labda wawe maRais wa Wasafi. Sioni sababu ya Chadema kuingia kwenye kintang'anyiro cha Urais maana hakina mtu mwenye sifa hata mmoja
 
Mkuu Nadhani Wewe unachukua mtazamo wa mtandaoni hasa jamii forum

Ila nenda mtaani utajua balaa la Ccm

Tuombe uhai October nitakukumbusha ushindi wa kimbunga wa Ccm

Mtaa upi ambao sisi hatufiki, au unadhani watu kunyamaza kwa kuhofia lile kundi lenu la watu wasiojulikana, basi ndio wanaikubali ccm?
 
Mkuu hakuna mwenye hofu mwenyekiti wa Ccm Rais Magufuli amefanya vyote maendeleo ya watu na vitu

October ni km kushuka mlima tu
Acheni hofu jengeni hoja za mliyoyafanya shaurini viongozi wenu msiegemee upande mmoja demokrasia safi ni maendeleo ya watu na vitu.
Tuache kugombana kwasababu ya vyama na watu tutangulize uzalendo wa taifa letu
 
Back
Top Bottom