Tumefika kwenye mteremko mkali sana kama Taifa, njia pekee ya dereva kutusalimisha na yeye kusalimika ni kutulia, avute pumzi, aache papara, wakati huo makondakta wake nao wasimtie presha, wasimshauri ujinga eti ooh....we kanyaga tu tunavuka.....noo!.....tunahitaji kondakta atakayemuambia dereva, break zimekatika, endesha gari taratibu tukifika hapo mbele, simama, shuka, gari ifanyiwe service.
Njia pekee ya kuvuka hapa sio kuteka tena, sio kutisha vyombo vya habari, sio kuua, sio kuficha ushahidi, sio kufunika madhambi, njia ni moja Tu, KUKIRI NA KUWAJIBIKA.