polokwane
JF-Expert Member
- Dec 16, 2018
- 4,158
- 7,667
Nimeyaelewa vizuri majibu ya jana ya Mh. Rais JPM alipowajibu wananchi wa jimbo la Mheshimiwa mbunge BWEGE, hivyo niombe pia sheria ya kodi ibadilishwe ili majimbo yote ambayo wananchi wamechagua upinzani au watachagua upinzani basi waachiwe na kodi zao ili wajiletee maendeleo wenyewe.
Namaanisha seririkali ya CCM isichukue hata senti moja kutoka kwa wananchi wa majimbo hayo ya upinzani ili kama ikiwezekana majimbo hayo yajikusanyie kodi yenyewe na kujiletea maendeleo yenyewe.
Maana haina maana na ni unyanyasaji wa kisiasa kwamba kodi mnatoa wote bila kujali ni CCM au upinzani na mnaminywa kweli kweli kutoa kodi na mnatoa kwa moyo na uzalendo mkubwa halafu linapokuja swala la maendeleo mnaambiwa mkadai kwa mbunge wenu wa upinzani, hii si sawa na si haki nadhani tuwaachie na kodi zao pia.