Kwa kauli ya Rais, tuombe sheria ya kodi ibadilishwe, majimbo yote ya upinzani Serikali ya CCM isikusanye kodi hata senti huko

Kwa kauli ya Rais, tuombe sheria ya kodi ibadilishwe, majimbo yote ya upinzani Serikali ya CCM isikusanye kodi hata senti huko

Kodi zikikusanywa na halmashauri huwa zinabaki huko huko halmashauri au zinaenda mfuko mkuu? Rais anazunguka nchi nzima kutishia wananchi waliochagua wapinzani, huku akiwa kimya kabisa wagombea wa chama chake wakimwaga rushwa waziwazi kama njugu! Rais huyu namfananisha na hayati Mkapa aliyekuwa anapanda kwenye majukwaa ya siasa kuhubiri chuki dhidi ya wapinzani. Nina hakika nchi hii itaingizwa kwenye machafuko na rais huyu asiyejua mipaka ya kazi yake.
Hilo la nchi kuingia kwenye machafuko ni ndoto zako tu. Hakuna mwananchi mwenye fikra za kuchafua nchi.
 
Hilo la nchi kuingia kwenye machafuko ni ndoto zako tu. Hakuna mwananchi mwenye fikra za kuchafua nchi.

Ni kweli, kwakuwa wananchi ni makondoo hata uchaguzi unapochezewa, hawana fikra za kutaka maamuzi yao yaheshimiwe.
 
Umemwelewa alichokisema? Kazi ya ujenzi. Wa vitu Kama soko nk Ni ya halmashauri siyo serikali kuu

bajeti yake halmashauri hupitishwa na bunge la halmashauri ambalo Ni madiwani wa hiyo halmashauri na mbunge wa eneo likiwa chini ya spika wao ambaye Ni meya

sasa halmashauri Kama halmashauri haina maendeleo wa kulaumiwa Ni bunge ambalo huptisha bajeti.Sasa kwenye Hilo eneo tatizo Ni Hilo bunge sababu limejaa madiwani na mbunge wa upinzani ambao hupitishwa bajeti kihovyo hovyo bila kulenga maeneo wananchi wanataka
Mbona tatizo hilo hilo lilipojirudia Mkuranga hakuhusisha na mbunge kuwa CCM? Yaani correlation kati ya kufeli kwa manispaa inahusiana nini na wananchi kichagua mbunge wa upinzani? Mbona hakutaja uzembe wa madiwani wa CCM ambao ndio majority kwenye hilo jimbo la Kilwa?

Hizi double standards ni kwa faida ya nani?
 
Ndio wampe my ambaye akiagiza soko lijengwe linajengwa Sio anayesema ohh Mimi na madiwani wetu Sio CCM usitupangie Cha kufanya yutajiamulia wenyewe baraza la madiwani.Lakini wakiwa baraza la madiwani Ni CCM kazi inakuwa ndogo ninkuwaamurisha tu sababu pia Yeye Ni mwenyekiti wa CCM aweza livunja Hilo baraza la madiwani kea kuwatimua uanachama lakini likiwa la upinzani hawezi

Ndio maana inakuwa vigumu kushinikiza maendeleo maeneo yenye madiwani wengi wa upinzani
Wapi Rais alitaja madiwani? Ni lini CCM haina majority ya madiwani Kilwa baada ya wanaCUF kuunga juhudi? Kwanini asimuite pale meya wa CCM amuhoji ila lawama ni kwa mbunge? Anyway halmashauri zaidi ya 90 zipo chini ya CCM na zina umaskini mkubwa je ameshatimua wabunge/madiwani wangapi mpaka sasa?

Then huwa anasema maendeleo hayana chama? Funny
 
Wewe ni kama ni hivyo kwa nini anasema "niliwaambia mnichagulie MTU anayeweza kunisikiliza"?
Mnamtetea sana mpaka mnapitiliza ndio maana hadi JK anaamua kuingilia kati kuwafundisha ili muache ujinga huo
Sasa ulitaka tumtetee Mbowe au!? Au Lissu!?

Kuwa serious kidogo basi.

Hoja ambayo ipo very clear ila Wapinzani mmekusudia kuibadili ni kwamba, maeneo ya kwenye Halmshauri yoyote yanasimamiwa na madiwani na Mbunge ni sehemu ya Madiwani hao.

Hivyo mambo kama stendi, masoko, maeneo ya michezo na vitu vyote vya aina hiyo, ni wajibu wa Hamshauri kuibua miradi hiyo na kuitekeleza. Vyanzo vya ndani mara nyingi ndio utumika kwenye utakelezaji wa hiyo miradi na serikali kuu uwa ina sponsor kidogo tu.

Sasa ulitaka Mzee Magu asiseme huu ukweli ili Wananchi waendelee kudhani upinzani una maana sana kwenye hii Nchi!?

Tutaendelea kumtetea. Mitano tena. Upinzani tupa kule.
 
Nimeyaelewa vizuri majibu ya jana ya Mh. Rais JPM alipowajibu wananchi wa jimbo la Mheshimiwa mbunge BWEGE, hivyo niombe pia sheria ya kodi ibadilishwe ili majimbo yote ambayo wananchi wamechagua upinzani au watachagua upinzani basi waachiwe na kodi zao ili wajiletee maendeleo wenyewe.

Namaanisha seririkali ya CCM isichukue hata senti moja kutoka kwa wananchi wa majimbo hayo ya upinzani ili kama ikiwezekana majimbo hayo yajikusanyie kodi yenyewe na kujiletea maendeleo yenyewe.

Maana haina maana na ni unyanyasaji wa kisiasa kwamba kodi mnatoa wote bila kujali ni CCM au upinzani na mnaminywa kweli kweli kutoa kodi na mnatoa kwa moyo na uzalendo mkubwa halafu linapokuja swala la maendeleo mnaambiwa mkadai kwa mbunge wenu wa upinzani, hii si sawa na si haki nadhani tuwaachie na kodi zao pia.
Tuna mtawala hatuna kiongozi!

Tena mtawala wa hovyo kuwahi kutokea Africa!
 
Meya wa CCM umeambiwa lile ni jiji!? Acha kuongea pumba wewe. Pale panaongozwa na Mwenyekiti wa Halmshauri. Ambae ni CUF. Mpinzani. Maendeleo yatatoka wapi wakati chama chenyewe kila siku kina migogoro isiyo na kikomo!?

Na kama hujui tu, Mbunge ni sehemu ya Halmashauri na wabunge wote ni madiwani kwenye Halmshauri zao.

Soma mifumo yako ya Nchi uielewe ndio uje kutoa arguments humu JF.
Wapi Rais alitaja madiwani? Ni lini CCM haina majority ya madiwani Kilwa baada ya wanaCUF kuunga juhudi? Kwanini asimuite pale meya wa CCM amuhoji ila lawama ni kwa mbunge? Anyway halmashauri zaidi ya 90 zipo chini ya CCM na zina umaskini mkubwa je ameshatimua wabunge/madiwani wangapi mpaka sasa?

Then huwa anasema maendeleo hayana chama? Funny
 
Hilo la nchi kuingia kwenye machafuko ni ndoto zako tu. Hakuna mwananchi mwenye fikra za kuchafua nchi.
Hata mimi sishauri hilo la machafuko na wala siliungi mkono na ninapingana nalo vikali sana ,

ushauri wangu ni kodi tu za majimbo yenye upinzani zisichukuliwe na serikali ya CCM bali waachiwe wenyewe ili wajiletee maendeleo.
 
Umemwelewa alichokisema? Kazi ya ujenzi. Wa vitu Kama soko nk Ni ya halmashauri siyo serikali kuu

bajeti yake halmashauri hupitishwa na bunge la halmashauri ambalo Ni madiwani wa hiyo halmashauri na mbunge wa eneo likiwa chini ya spika wao ambaye Ni meya

sasa halmashauri Kama halmashauri haina maendeleo wa kulaumiwa Ni bunge ambalo huptisha bajeti.Sasa kwenye Hilo eneo tatizo Ni Hilo bunge sababu limejaa madiwani na mbunge wa upinzani ambao hupitishwa bajeti kihovyo hovyo bila kulenga maeneo wananchi wanataka
Usipindishe maneno kabisa kauli yake iko very clear haihitaji tafsiri za upotoshaji kama zako mkuu.
 
Ndio wampe my ambaye akiagiza soko lijengwe linajengwa Sio anayesema ohh Mimi na madiwani wetu Sio CCM usitupangie Cha kufanya yutajiamulia wenyewe baraza la madiwani.Lakini wakiwa baraza la madiwani Ni CCM kazi inakuwa ndogo ninkuwaamurisha tu sababu pia Yeye Ni mwenyekiti wa CCM aweza livunja Hilo baraza la madiwani kea kuwatimua uanachama lakini likiwa la upinzani hawezi

Ndio maana inakuwa vigumu kushinikiza maendeleo maeneo yenye madiwani wengi wa upinzani
Ushauri wangu kuhusu kodi uzingatiwe pia katika majibu hayo ili kuepusha msuguano na ubaguzi.
 
Usipindishe maneno kabisa kauli yake iko very clear haihitaji tafsiri za upotoshaji kama zako mkuu.
Wewe ndio unajaribu kupotosha. Wananchi tumemuelewa Rais na Octoba hatutafanya tena makosa kuchagua wahuni kwenye ngazi yoyote ile. Iwe Ubunge au Udiwani.
 
Wewe ndio unajaribu kupotosha. Wananchi tumemuelewa Rais na Octoba hatutafanya tena makosa kuchagua wahuni kwenye ngazi yoyote ile. Iwe Ubunge au Udiwani.
Ushauri wangu kuhusu kodi uuzingatie pia katika majibu yako maana huko nako wanalipa kodi bila kujali ni wana CCM au upinzani
 
Inapaswa iwe hivi. Wenye kadi za CCM pekee ndiyo wawe walipa Kodi, wenye kadi za upinzani na wasio na kadi ya chama chochote Cha siasa, tusilipe Kodi, maana maendeleo ni ya wana CCM pekee.
 
Ile kauli imemtoka si kwa bahati mbaya bali ni dhahiri anaipenda maana alitaka kuitumia kule Mvomero bahati nzuri akauliza mbunge ikaonekana ni wa ccm, hapo akatahayari.

Kama haleti maendeleo kwa majimbo ya upinzani naunga mkono hoja asichukue kodi
Kwa tunao mfahamu tangu Shuleni tunajua kwamba alicho kiongea ndicho kipo moyoni.
 
Wewe ni nani nchi hii. Huyo mvunja katiba wenu kaeni naye huko huko kwenye mboga mboga. Watanzania wamemchoka.
Wewe ndio unajaribu kupotosha. Wananchi tumemuelewa Rais na Octoba hatutafanya tena makosa kuchagua wahuni kwenye ngazi yoyote ile. Iwe Ubunge au Udiwani.
 
Upinzani wa akina Zitto Kabwe na Tundu Lissu wakuenda kuichafua nchi nani wa kuwachagua, na Mimi naongezea Mkiwachagua Vichaa kama hao waendelee na ukichaa wao. Mbona Majimbo Majimbo Mengine yanaongozwa na upinzani lakini miradi inakamilika.
Kongwa kukoje?
 
Kuchafua nchi ni kwenda kuongelea mabaya ya nchi nje ya Nchi badala ya kupeleka mamlaka husika

Mfano Lisu Alikuwa mbunge hata mtu usipokuwa mbunge Ina mbunge .Kama una issue yeyoye ipeleke bungeni ipatiwe majibu ndani ya bunge .Sasa unakuta mtu mbunge Halafu anabweka nje. Ya bunge akiingia bungeni ansufyata kimya hayo anayobweka nje hajawahi bweka bungeni apewe majibu!!! Hili ndio tatizo la kuitwa wachafua nchi hawatumii proper channels ambazo hata wao wanazo kuwakilisha hoja zao bungeni

Kubweka nchi ndiko kumaitwa usaliti au kuchafua nchi au serikali
Hujui tofauti ya nchi na serikali, Kama serikali inafanya mabaya isemwe popote pale!
 
Back
Top Bottom