1) je mabaunsa wa Yanga wanatambulika kisheria kama nani? Ni kitambulisho kipi kinachowaonesha kuwa ni mabaunsa wa Yanga na sio walinzi wa uwanja? Wana mamlaka gani kisheria na kikanuni kiasi kwamba wawe na uwezo na nguvu wa kusitisha jambo la kisheria?
2) Sheria inasema kama kuna sababu ya msingi au dharura je kwanini bodi imeshindwa kuziweka sababu hizo za msingi ama dharura ni zipi hizo?
Dodoma jiji walipata ajali ya bus na kupelekea baadhi ya wachezaji na viongozi kupata majeraha na kupelekwa hospitali hivyo ikasababisha mechi kuhairishwa.
Dodoma jiji walikidhi taratibu za kanuni za kuhairisha mechi sababu
- sababu ya msingi ni majeraha yaliyotokana na ajali
- dharura ilikuwa ni ile ajali.
Sasa twende kwa upande wa Simba je kipi kulikuwa ni sababu ya msingi au dharura ya kuifanya ile mechi ihairishwe?