Magwangala
JF-Expert Member
- Oct 4, 2011
- 2,836
- 2,138
1.Umesoma ripoti yote ya bodi?Bodi wamesema kuwa kamati ilibaini kuwa walinzi ambao baadhi yao walifahamika kwa sura kuwa ni walinzi wa Klabu ya Yanga,hii tu inatosha kujua Yanga walihusika na vurugu hizo, Jiulizeni Simba walipopewa adhabu na CAF ya kucheza bila mashabiki,ni kitambulisho kipi kinaonesha wale ni mashabiki wa Simba hadi wakaadhibiwa Simba kwa vurugu za mashabiki?1) je mabaunsa wa Yanga wanatambulika kisheria kama nani? Ni kitambulisho kipi kinachowaonesha kuwa ni mabaunsa wa Yanga na sio walinzi wa uwanja? Wana mamlaka gani kisheria na kikanuni kiasi kwamba wawe na uwezo na nguvu wa kusitisha jambo la kisheria?
2) Sheria inasema kama kuna sababu ya msingi au dharura je kwanini bodi imeshindwa kuziweka sababu hizo za msingi ama dharura ni zipi hizo?
Dodoma jiji walipata ajali ya bus na kupelekea baadhi ya wachezaji na viongozi kupata majeraha na kupelekwa hospitali hivyo ikasababisha mechi kuhairishwa.
Dodoma jiji walikidhi taratibu za kanuni za kuhairisha mechi sababu
- sababu ya msingi ni majeraha yaliyotokana na ajali
- dharura ilikuwa ni ile ajali.
Sasa twende kwa upande wa Simba je kipi kulikuwa ni sababu ya msingi au dharura ya kuifanya ile mechi ihairishwe?
2.Ndio maana nimeuliza umesoma ripoti yote ya Afisa Usalama wa mechi? Sababu za msingi sio kwa mujibu wako bali kanuni zinaeleza wao wakiona sababu za msingi,Ndio maana umeambiwa uchunguzi unaendelea ndio maana mechi imeahirishwa(Kwa kanuni no 34:1(1.3) )ili kutoa hukumu ya haki.
Ni nani aliyekueleza kuwa sababu za msingi ni ajali tu kama ya Dodoma Jiji? Unaweza kuweka ushahidi kuwa sababu za msingi ni ajali tu kwa mujibu wa kanuni?Nenda kasome kanuni ya 12:2 na 12:6 zote zinaipa mamlaka kamati kukutana wakati wowote kuchunguza na kutolea maamuzi jambo lolote la dharura( hii dharura si kwa tafsiri yako). Halafu Yanga wanadai points 3 za mezani,unajua utaratibu wa kupata hizo points 3 za mezani?Mmeenda uwanjani hakuna refa wala wasimamizi wa mchezo waliopelekwa na bodi husika mkategemea kupewa points 3 na hiyo hiyo bodi,hii akili mnatoa wapi?