Kwa kweli Bongo bado sana

Kwa kweli Bongo bado sana

😂 aloooh! naona wana'Diaspora mmegoma kuwekeza kwenu pamoja na sera zote zinazowapendelea.

Haya bwana.
Mkuu,tatizo huko uaminifu upo chini sana,wengi tumepigwa na tuliowaamini,hakuna Diaspora ambae hajapigwa,

Mleta mada upo sahihi kabisa,ukitoka mbele unaiona Bongo bado sana (Hapa simaanishi dharau) Angalia hata Lema alivyotoka Canada,kila kitu bongo alikua anaona ni umasikini,mara alaumu Bodaboda,mara aseme sijui vikoba,naona sasa hivi kazowea tena.
 
Wachache watakuelewa bongo ni ya kifala sana. Huitaji kwenda ulaya kulijua hilo, nenda tu pale Nairobl ukae mwezi mmoja afu urudi Bongo kudadeki utakubaliana na wazungu wanaosema Dar ni kijiji pembezeno mwa bahari ya hindi.

Sisi mipamgo miji yetu ni ya kimaskini sana. Afu serikali haijengi miundombinu ya maana kupendezesha miji. Badala yake watu binafsi ndiyo wanaojijengea migorofa huku mitaani
Aisee, umaliza!
Watu hawatokagi nje, ni vigumu kukuelewa
 
Watu wapo wapo tu wamekaa na kusimama kila sehemu 🤣🤣🤣🤣

Aisee kuna vitu vinachekesha.
😂
Kwa kweli sidanganyi kwa hili
Kwangu imekuwa culture shock!
Sababu baada ya muda mrefu na sehemu niliyotoka sijaona watu wamechonga mabenchi yao ya kukaa pembezoni mwa barabara siku nzima
 
Wachache watakuelewa bongo ni ya kifala sana. Huitaji kwenda ulaya kulijua hilo, nenda tu pale Nairobl ukae mwezi mmoja afu urudi Bongo kudadeki utakubaliana na wazungu wanaosema Dar ni kijiji pembezeno mwa bahari ya hindi.

Sisi mipamgo miji yetu ni ya kimaskini sana. Afu serikali haijengi miundombinu ya maana kupendezesha miji. Badala yake watu binafsi ndiyo wanaojijengea migorofa huku mitaani
Uafrika hasa utanzania ni laana.
 
Mkuu,tatizo huko uaminifu upo chini sana,wengi tumepigwa na tuliowaamini,hakuna Diaspora ambae hajapigwa,

Mleta mada upo sahihi kabisa,ukitoka mbele unaiona Bongo bado sana (Hapa simaanishi dharau) Angalia hata Lema alivyotoka Canada,kila kitu bongo alikua anaona ni umasikini,mara alaumu Bodaboda,mara aseme sijui vikoba,naona sasa hivi kazowea tena.

Mkuu me naona mnapokosea ni kukabidhi majukumu ya kusimamia assets kwa wanafamilia ama watu wenu wa karibu. I mean where can you get the audacity to penalize such a close person when they do you wrong?

Kuna classmate wangu wakati nipo campus, yeye ana dada yake yupo Germany. Huyo dada yake akawa anatuma hela ili jamaa aendeleze ujenzi wa apartment yake Kigamboni lakini jamaa akawa anakula bata na shpapi mpaka akanunua na Subaru Impreza. Mwanzo alijenga jenga ila ilipofika hatua ya finishing sijui ndo alitumiwa pesa ndefu akaingia tamaa ndo akachukua na gari.

Sasa mtu ndugu yako wa damu kama hivi utaweza kumpeleka jela?

Issue hizi ni za kufanya na mtu baki kabisa. Mnaingia mikataba na una unakua unamlipa kwa makubaliano yenu. Akizingua mtu wa hivi ni rahisi kumchukulia hatua.
 
Hawa watu wanaotoka ughaibuni huwa wana maneno sana.

Nakumbuka nilikiwa maskani Upanga akaja mchizi wangu kutoka Harlem, anasema Tanzania watu wamepigwa na jua sana mpaka Kariakoo vijana wamepaukaaa wanaonekana kama wazee.

Nilisikitika sana.
 
Jua la bongo sio mchezo
Hata Airport mpya imepauka kichizi
Vituo vya mwendokasi vinaanza kuonekana kama magofu 😂
 
Sijawah fika developed country yoyote duniani. Lakini nashindwa kuelewa Kwanini Watz wanaishi maishi ya kis*nge namna hii, hovyo hovyo tu inanikera mno mno.

In FACT mazingira ya Tz yananiharibu sana AKILI nimeliona hili

Nikienda sitarudi huku.

Kwa hapa Tz sehem nimeona ina afadhali ni Tanga Mjini iko vizuri Sana hata hali ya hewa ni Safi very fresh, Mara nyingi huku dsm I use face mask japo mijitu huwa inanishangaa shangaa
 
Ukilinganisha TZ na ulaya, utakuwa hauitendei haki,
Sie tupo ulimwengu wa tatu! Bado kula yetu tu shida, hata kutengeneza bulb ya element hatuwezi, unatulinganisha na watu wanaotaka kuhamia mwezini!
Tuna siasa mbovu,ccm ndio chanzo cha umaskini wetu,
Nchi kama Malaysia, tuekey, china, zilipiga hatua baada ya mtu mmoja sio kundi kuamua kutumia rasilimali za, nchi kwa manufaa ya wananchi wote!, Sie, tumejaza majizi, tu na mijitu isiyofikiria,
Chukulia kwa mfano, wa Afrika wa ECOWAS, wanajipanga kuishambulia nchi ya wa Afrika wenzao! Unamwaga damu ya me Afrika mwenzako ili kumtii mzungu!!
 
Inabidi ujiandae kisaikolojia kukubali hali ya kwenu.

Hapo ndiyo kwenu, na hao ndiyo ndugu zako, hata kama umechukua uraia nje.
Tulikuwa anza za kupanga jinsi ya kurudi mazima halafu dada yake mke wangu ndio tulikuwa tunahasishina nae sana kuanza kufikiria kujipanga na kurudi mazima yeye alitutangulia wiki mbili kabla yetu.
Duh! Tumemkuta ameshachoka na ile nguvu ya kurudi imefifia kama si kupotea!

Mapicha haya hapa
Huu ndio ule famous Haile Selassie road niliokulia maisha ya shule-nyumbani, enzi hizo nilikuwa na roller skate nachezea barabarani, hii hapa ni hali ya sasa!

1691758966916.jpeg

1691759032724.jpeg

1691759084305.jpeg

1691759261242.jpeg

Na hii ndio Chole road, hiki kibanda kipO next to IST of Tanganyika
Barabara imejaa daladala na bodaboda

1691759319461.jpeg

1691759576491.jpeg

1691759451714.jpeg

1691759483203.jpeg

1691759518758.jpeg

1691759710425.jpeg
 
Daah,

Mwenyewe nimechoka.

H.I.M Haile Selassie imekuwa kama Hussein Shekilango.

Wamejitahidi kupiga viraka lakini.

Umenikumbusha sana viwanja vyangu na marehemu Ras T na Gotta Irie hapo miaka kibao iliyopita.

Ukikunja kidogo unaingia studio kwa Master J, wadogo zetu walikuwa wanaenda kucheza basketball kwa Mzee Kimaro wa TANESCO. Mzee poa sana kwake alikuwa na basketball court na studio ya muziki.

Mimi kwa sasa nasubiri msiba au harusi mtu wa karibu, na harusi zenyewe zishaisha kwa sasa labda msiba tu.

Na hivi wananitaka nije Kisarawe kwa visa ndiyo kabisaaaa hawanipati.

Nilisema nitakuja kutembea kila miaka 10 huu mwaka wa 11 unapita sasa sijakanyaga.

Na hivi washua wanakuja huku US kila summer ndiyo kabisaaa nakosa hata motisha ya kuja huko.
 
Tulikuwa anza za kupanga jinsi ya kurudi mazima halafu dada yake mke wangu ndio tulikuwa tunahasishina nae sana kuanza kufikiria kujipanga na kurudi mazima yeye alitutangulia wiki mbili kabla yetu.
Duh! Tumemkuta ameshachoka na ile nguvu ya kurudi imefifia kama si kupotea!

Mapicha haya hapa
Huu ndio ule famous Haile Selassie road niliokulia maisha ya shule-nyumbani, enzi hizo nilikuwa na roller skate nachezea barabarani, hii hapa ni hali ya sasa!

View attachment 2714539
View attachment 2714540
View attachment 2714541
View attachment 2714542

Na hii ndio Chole road, hiki kibanda kipO next to IST of Tanganyika
Barabara imejaa daladala na bodaboda

View attachment 2714544
View attachment 2714552

View attachment 2714546
View attachment 2714547
View attachment 2714549
View attachment 2714553

utoko.jpeg

Hivi huu utoko utoko mweusi kwenye rangi za nyumba, nafikiri unatokana na nyumba kupigwa mvua halafu rangi ku react, hakuna rangi ambayo haita react na mvua kutengeneza huu utoko?

Nikiuona najiuliza sana. US nyumba zinakaa four seasons bila kupata utoko huu, sanasana ukiwa na nyumba yenye vynil nje utafanya power wash mara moja baada ya miaka 5 au 10, na hata usipofanya uchafu hautakuwa visible hivyo.

Watu hawaoni au hawajali?

Ukienda Upanga kuna nyumba chafu hivyo kichizi, halafu, hata ukipiga rangi haichukui mwaka zikipiga mvua inarudia vilevile.
 
View attachment 2714588

Upanga nyumba zimezidi kuwa chafu sana
Huu utoko sijui ni (Grime-build up of dirt), labda sababu ya vumbi za barabarani

Aisee, mkuu, sasa hivi kama unaendesha gari bongo ,utashangaa ya hawa bodaboda wa pikipiki, yaani unaendesha njia nzima unawakwepa wao, ni majanga sio kidogo, nitaweka clip uone mwenyewe, hawa ni kama wameruhusiwa kutofuta sheria za barabara, yaani wanapita kwenye red traffic lights, mbele ya traffic amesimama tu, na sio mmoja ni kama nzige, yaani wamevuruga barabara zote, ni makelele yao yao ya honi, halafu wamefunga honi za mabasi, ni fujo tupu barabarani.
Sio ile Dar unayoijua kama hujafika huku miaka 10 iliyopita, kwa kweli haikuvutii kabisa kusema imeendelea ni majanga tupu, hakuna ustaarabu kwenye kila kitu.
 
Back
Top Bottom