Upanga nyumba zimezidi kuwa chafu sana
Huu utoko sijui ni (Grime-build up of dirt), labda sababu ya vumbi za barabarani
Aisee, mkuu, sasa hivi kama unaendesha gari bongo ,utashangaa ya hawa bodaboda wa pikipiki, yaani unaendesha njia nzima unawakwepa wao, ni majanga sio kidogo, nitaweka clip uone mwenyewe, hawa ni kama wameruhusiwa kutofuta sheria za barabara, yaani wanapita kwenye red traffic lights, mbele ya traffic amesimama tu, na sio mmoja ni kama nzige, yaani wamevuruga barabara zote, ni makelele yao yao ya honi, halafu wamefunga honi za mabasi, ni fujo tupu barabarani.
Sio ile Dar unayoijua kama hujafika huku miaka 10 iliyopita, kwa kweli haikuvutii kabisa kusema imeendelea ni majanga tupu, hakuna ustaarabu kwenye kila kitu.