Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Mimi mkasa wangu ulinitokea bwawani eneo la darajani, ilikuwa kama saa 6 usiku alitokea mwanamke mrefu

kavaa gauni jeupe na kuingia
barabarani. kwa ghafla na kisha kuanza kunisimamisha huku

akiingia barabarani mwili wangu pamoja na nywele ulisisimka huku nikikumbuka

hapa nikiyumbishwa ni ajali mbaya maana mbele kuna gari zinakuja kwa kasi nyuma yangu pia gari zinakuja kwa kasi

Baada ya hapo wala sikuona kama nimemgonga au kukimbilia upande wa pili wa barabara


Ukitaka kuona haya mambo tembea sana safari za usiku na pia huwa kuna maeneo yanajulikana kwa visa hivyo

Pia kuna baadhi ya vitu huwa vinakutokea lakini uhalisi wake huwa unatokana na uchovu (fatigues)

Barabarani kuna mambo mengi mengine ni tabia za watu hupenda kusifiwa hata kama kitu kipo nje ya uwezo wake, atalazimisha kufanya ili ionekane huyu jamaa ni kiboko
 
Hivi ukutane na mlevi au chizi katikati ya mbuga ya mikumi au Yale mapori ya maeneo ya ruaha ukiwa unatoka mikumi kweli...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Trople Kiss!? Maimuna huyo!

Sent using Jamii Forums mobile app
nakumbuka nilipokuwa dreva wa basi moja linaitwa Tanganyika bus kule MWANZA nilipokuwa ktk route za kwenda Mara ipo siku njiani majira ya saa 3 nikiwa ktk shughuli zangu za udereva nilionana ghafla na jamaa akiwa ana Ng'ombe wawili akikatisha katkati ya barabara tena ni babu kavaa lubega,nilichosema ni kwa jina la Yesu ,Mungu wangu nisaidie sikuwa hata na akili ya kushika breki niliachia mikono na gari ilivuka pale,shukrani kwa utingo jirani yangu baada ya kuona ile hali utingo yule alikanyaga breki huku tukiwa tumevuka lile eneo,baada ya hapo sikuweza tena kuendesha,gari liliendehswa na utingo hadi tukafika nahc ni Mungu tu alisaidia si mimi,tokea siku ile sijaedesha tena gari usiku mwisho ni saa 12 jioni
 
Wakija na wavuvi hapa...nahisi patachimbika'
[emoji2] [emoji2] [emoji2] wakija wavuvi na stori zao wanayoyaona baharini usiku,, nyinyi mtajihisi mnaona midoli tu barabarani. kote nime experience najua udereva mpaka uvuvi,, maana kwetu ni karibu na bahari tangu nina miaka kumi na tatu nilikua navua samaki baharini,, nikaanza kwenda na usiku pia na makarabai,, tunayoyaona huko baharini usiku,, nafkiri barabarani tunaona tom n jery[emoji2] tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napafahamu mkuu pale ni wilaya ya Handeni kwa Wazigua, Ni noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya baharini ndio nilikua nayasubiria kwa hamu mnoooooooo
 
Tupe stori angalau mbili tatu Mkuu. ili na sie tusio wavuvi tufahamu kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikatae ndugu mimi Nisha kutana. Mambo kama hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usikatae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enzi hizo nimetoka moshi naenda mbeya nimepanda hood tumefika mikumi basi ikasumbua.tukasubiri ipone kwa mda wa saa tatu,tumekuja kuondoka Giza limeanza,tumefika kitonga SAA NNE usiku.abiria wawil MTU na mkewe wakaomba kushuka eti wamefika.gari ikawashusha,ilibaki gumzo wanaenda WAP na kipindi hicho hata hakujajengwa kituo cha polisi na pana Giza totoro.
 
Mkuu ulishindwa kuwauliza ? au uliogopa wangeshuka na wewe ?[emoji851][emoji851][emoji851]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah hata konda alibaki mdomo wazi
Kuna jamaa yangu amenipigia simu anasema, Kuna siku alikua anarudi Nyumbani Area C, saa sita usiku. alikua taxi driver, kufika eneo la round about ya kuelekea Area C akasimamishwa na mdada amevaa ijabu, jamaa anasema alimpa maelekezo sehemu anapotaka kwenda. jamaa anasema alipo fika maili mbili aliuliza ni njia Ipi ili afahamu mapema pa kuingilia, lakini aliona kimya akamuuliza tena akaona kimya, ikabidi apaki pembeni akageuka nyuma akakuta siti tupu. jamaa anasema alifungua mlango na kukimbia, gari aliifuata asubuhi na kwenda kukabidhi kwa mwenye gari. Ndio ikawa mwisho wa yeye ku taxi driver. ni miaka ya tisini kwa mujibu wake. jamaa anaishi Dom.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni hayo mauza uza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saa 7 mtu anatokea wapi jamani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…