Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Duh mafuta yakiisha hapo balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

We kama muongozo vileee



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bisha tu usilolijua
Rafiki yangu aliwahi kuchukuliwa kichawi akarudishwa
So subiri uje ushuhudie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKUU Mara nyingi tukio linakukuta UKIWA peke yako,,,,hata kama mpo wengi lakini wenzio wamelala muda huo,,,hapo ndy unaona mauzauza,,,,kuna JAMAA ZANGU 2 walipata ajali ile bara bara ya SALENDER BRIDGE,,,DAR,,pale DON BOSCO kwa mbele PANA MBUYU mkubwa kati kati ya Bara bara,,jKITUO KINAITWA MBUYUNI,,,Jamaa zng wamepoteza maisha kwa siku tofauti,,,gari imegonga MBUYU akiwa peke YAKE,,,USIKU wa manane,ALIKUWA AKIENDA KWAKE ,,TENA kila mmoja kagonga kwa SIKU YAKE lakini vifo vinafanana,,,,haya mambo Yapo mkuu,,,hadi yakukute ndy utaamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitomb* ndio nini ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shy wachawi mno
1.kuna siku nikiwa advance, nipo likizo home nikakabwa usiku
2.kuna siku uvunguni mwa gari yetu tukakuta ngozi ya paka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole sana hiyo sehemu naijua mana nimekulia maeneo hayo,ukitoka mombo,kuna vijiji kadha kama mwelia,mwisho wa shama,kikwazu,chekelei,madumu,hizi sehemu ni mbaya sana, kipindi hicho usafiri ni baiskeli nikawaida kuwa beba hao viumbe wajastuka baiskeli imekuwa nzito ghafla pia kaharufu ka jasho la mtu utahisi,salama yenu nikule kumgonga huyo jama vinginevo ni hatari tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2007 mugumu .mkoa wa mara
Kuna jamaa jirani yetu alikua mwalimu wa primaly
Sa kuna siku anaenda job akakutana na bibi kizee mchana wa saa saba
Bibi akaomba lifti jamaa akamtolea nje akasepa
Ghafla jamaa akaanza kuhisi baiskeli nzito akakazana tu .kufika maeneo ya shule, jamaa ile anashuka .bibi nae huyu "Ahsante mjukuu wangu"
Jamaa hakujibu aliogopa mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii chai sasaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Haaaaaaa daah mkuu achaaa hayo huko Sudan/darful ndo shidaaaa

mndamba kutoka Ifakara
 
Hee! Mungu epushia mbali,sijawahi kushuhudia vitu kama hivyo safarini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau mwaka jana nilipopata ajari katika mazingira ya kutatanisha mbeya mjini, niligongwa na Ambulance yaani ilikuwa kwenye kona tumeongozana magari mawili mimi nilikuwa nyuma na gari dogo pia kulikuwa na gari dogo ambalo tulikuwa tumeongoza nalo baada ya kukuta kona ilikuwa ni kama nimepigwa usingizi hadi nilipokuja kushtuka baada ya kusikia kishindo kikubwa baada ya kugongwa na ambulance, bahati nzuri tulitoka wote salama.
 
Bado tu Siku yako itafika utayaona hayo yasemwayo. Yakikutokea zingatia unavyoambiwa :--Usifunge brake, wala usikwepe, nyoosha usukani, to a mguu kwenye kijiko cha mafuta.. "Kalaga baho".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…