Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kuna taratibu gani za kiserikali za kufuata au nauziwa kihuni tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Usiingie upande mbaya wa sharia na hicho kitu.
Uhakiki wake unaanzia Kata, Wilaya (kamati za Ulinzi na Usalama), Mkoa hadi Polisi kwenyewe.
Kama una nia na unasafiri sana, hasa safari za mbali na usiku, hizo ni moja ya sababu ya kuombea silaha.

Siyo mchezo ukisafiri usiku, ingalau una ka ulinzi ka kukupa moyo na ujasiri.
Mimi nina visa vingi tu ila majini sijawahi, narudia sijawahi kuyaona!!
 
Dar pale muheza kuna kuti lipo juu kwenye nyaya ya umeme,kuna siku nilipita saa sita usiku naendesha gari nilihisi kama mtu ana bembea ,ni ujasiri tu sikutetereka.
Hahahhaha naweza kuimagine woga ulokua nao
 
Hiyo ajari mpaka leo siielewi
Lile gari la kigwa lina teknolojia ya ku detect any moving object mbele yake pamoja na auto brake
Yani kwa mfano uko speed then mbele ghafla gari lingine hili hap
Lile gari litakutaadharisha usimame na baada ya sekunde kadhaa linasimama lenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Pale kuna twiga sana na speed ni 50kph,twiga huwa na akili nyingi anaweza piga breki ya ghafla na kugeuka akiona hatari.
Waliofika mapema waliona twiga pembeni wawili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka mingi naendesha gari tena usiku,hasa njia ya tanga nimeendesha roli zaidi ya miaka mi4 na mara nyingi napita usiku, na saa hii Niko safari be ktk nchi fulani, sijawahi kuona kitu cha kunitumia, nawasikiaga tu watu wengine, nilichowahi ona ni mtu yuko uchi saa 8 usiku mbele kdg kupita muheza town kuelekea lusanga na mtu akiwa anatembea uchi usiku kipande cha segera hale, lkn wote hawa nafikiri ni wendawazimu tu kama tunaowakutaga mchana barabarani, na siku moja wkt nakaribia kuingia mkata saa 9 usiku nilimgonga bundi nilikuwa speed akajipiga kwenye kioo kikubwa cha mbele mpk kafa lkn kioo hakikuvunjika, lkn nikiwa tanboi zamani wkt nikiwa njia ya tabora arusha wkt huo ktk basi za kampuni fulani hv dereva wangu alitaka kuangusha gari maeneo ya ziba kuelekea nzega baada ya kuruka kwenye kiti akiwa anaendesha baada ya kudai panya kamwingia kwenye suruali, lkn mi nilikua hapo jirani sikuoni panya, lkn baada ya kuwa dereva na mara nyingi nasafiri peke yangu tena nakesha, ninachokijua ukiendesha mda mrefu na ukiwa na uchovu unaweza anza sinzia na kuona kama mko wawili na huyo ulienae anakuongelesha, au unaweza ona kama mtu anavuka au mnyama kumbe ni uchovu tu na usingizi, ushauri paki gari na upumzike hata saa moja,mf.juzi maeneo fulani ya Zambia mchana naendesha nikaona kama farasi barabarani kucheki kwa makini gari inaelekea kulia mwa barabara nikailudisha barabarani kumwangalia kijana nilienae kalala fofofo, napaki gari pembeni anashtuka na kuniuliza anko vp namwambia nasinzia je umeona gari ilivyotaka kuhama njia? ananijibu sijaona, nikamwambia usingizi unaambukiza mi nimesinzia kwa kuwa njia nzima we unalala tu kushoto hapo, nikamwambia nalala baada ya saa moja niamshe, aliponiamsha nikaendendelea na safari, khs kumgonga mtu usimwone inatokea wengine waoga hukimbia baada ya kuguswa na magari kwa uzembe wao, hata mi nikiwa nasoma siku moja utotoni niliingia barabarani bila kuangalia ikatokea hilux moja ikashika bleak lkn inapushi na kuanguka ile dereva kufungua mlango mi nikainuka mbio nyingi, ushauri ukiona unadrive hata kama ni mchana ukaona mauza uza paki gari panda kitandani lala kwa muda, kama haina kitanda kunjua siti lala, mara nyingi kuendesha gari mda mrefu hukupunguzia umakini
Nimesoma coment kuanzia 1 mpka 22 hii,wewe ndo umeongea uhalisia na nilichokuwa nawaza.bt wote wamekaza uchawi uchawi/mauza uza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha...jamaa yangu mmoja anasema na yeye jana tu amekutana na hayo majambazi na gari lile lile akayaoneshea SMG ndo yakakimbia yeye alikuwa anaendesha gari Cadillac SUV ya mwaka 2017.alikuwa speed 170. Baadaye akayaacha alipokanyaga mpaka speee 190.

Mkuu Sub Machine Gun (SMG) ni silaha ya kivita, kumiliki kwa matumizi ya kawaida sio rahisi.
 
Chai chai chai... Kikombe sh ngapi? Acheni fix madogo...
Utingo alikuja kukanyaga brake wewe ukiwa umetoka kwenye kiti cha udereva au ukiwa pale pale?

Aisee... Gari ilinyooka tu sababu barabara ilikuwa imenyooka? Ha ha ha.... Wadau muwe hata mnatufikiria na sisi wasomaji.si kwamba ni wajinga sana. Sometime tunasoma ili tuburudike lakin haimaanishi kuwa ni wajinga sana .
Hii haina part two yake?
naona unawapa Dozi nene
 
Kuna siku ilikuwa 2007. Nikitoka Arusha kwenda Dar saa Saba Nane usiku nilikuwa napita maeneo ya kwedikwazu. Kuna mahala Barbara imenyooka Sana Basi nikawa natembea speed 100-120.
Kuna mrembo mmoja mdada akawa anasimamisha gari akiomba lift. Nikapiga taa kubwa kumwona vizuri mrembo haswaa, sikusimama nikanuoosha goti, huku najiuliza huyu anaenda Wapi saa hizi,. Bwana ile nampita kwa speed ile alinipiga busu Mara tatu hapo dirishani. Maana sikuwa nimefunga madirisha ili nipigwe upepo nisilale. Nilifika dar Sina raha kutwa nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa kwedikwazu nakuelewa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 90 mwanzoni, baba alikuwa anatoka Mwanza kwenda Nairobi, ile ndo ameanza kuiacha tu Mabatini, kufika daraja la Mwananchi hakuona daraja, akaona ziwa limetanda kote, utingo wake akamwambia wewe lenga tu tunapopitaga siku zote. Hammad, kulivuka lile eneo wakashuka wakaangalia walichokiona kabla, hakukuwa na ziwa wala tairi za scania kulowana.


Miaka ya 2000 mwanzoni walikuwa wakisomba mafuta kutoka Kisumu wanaleta either Nyamongo au Buhemba, siku hiyo kaja hom anatusimulia alichokiona milima ya Roketo, kama unaenda Tarime kutokea Musoma. Akatuambia, wakati wanapita usiku waliona ng'ombe mkubwa ajabu akikatisha barabara kuelekea upande wa pili, hakuna aliyethubutu kumgonga wa kusimama, wenzie waliokuwa wanakuja nyuma wakakutana na mwingine tena eneo lile lile.
 
Mwaka huu nipo na Toyota Ipsum new model maeneo ya Gairo naitafuta Dodoma mida kama ya saa tano usiku hivi, ghafla naiona gari toyota carina SI imesimama mbele yangu.

Sijui nini kilitokea ila niliingia nzima nzima wala hakukuwa na kishindo cha magari kugongana ila tairi zilipiga kelele sana maana nilijaribu kuzuia brake na wala hakukuwa na uharibifu wa gari.

Mpaka leo sielewi ile gari ilitokea wapi na kama uchawi basi umeadvance.
dah jaman hizi story nyengine Nina was was Nazo maana mnanieka kwenye dilema, cjui niamini au laaa
 
Mimi ilikuwa ni mwaka juzi nikitoka dsm kuelekea Dom nipo njiani naTezza naitafuta Dom hapo mida ya saa sita usiku nimewasha full ndipo kwa mbele yangu mita kama 70 nitaona kundi la watu kama saba hivi wamesimama pembeni ya balabala wote wana mavazi meupe niliogopa nikaongeza speed ilewkuwapita tu nikahisi gari kama imeongezeka uzito hivi kama kuna mzigo nimepandisha ghafra nilishangaa nikajaribu kuangalia kwa nyuma asalale wale watu wako nyuma ya gari ile butwaa nilopigwa nikayumbisha gari nikakontro na mabreki gari lilivyosimama sikuona mtu, kuanzia hapo akili haikukaa sawa nikawa naitafuta Dom nipate kwawkulala tu hata kulala sikulala usiombe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKUU KUNA siku nilikuwa nakwenda TANGA,,,nipo na jamaa kama 4 kwenye GARI ndogo nikiwa naendesha ,, nakumbuka tulitoka hapa DAR ,mapema kama SAA 12 jioni,,tukaenda mdogo mdogo kufika CHALINZE tukatulia SEHEM vurugu za MABASI NA MAFUSO ZIPUNGUWE,,,kufika kama SAA 4 USIKU tukaanza safari ya kwenda NGAMIANI TANGA,,,TUKIWA kwenye gari story ziliendelea kama kawaida ili DEREVA NISILALE.,,tukaipita MSATA,,salama,,WAMI,,, MKATA,,SEGERA hyo,,,,Salama salmini, HALE ,, tukatoboa MUHEZA SAA nane USIKU,muda huo wenzangu wote nilihisi wamelala,maana ilikuwa kmya,,nlikuwa nasikiliza MVUMO WA INJINI YA GARI NA UPEPO TU,,, sasa balaa likaanza TUMEFIKA kuna SEHEM inaitwa MKANYAGENI,,nikaona mbele kama mita 50 kuna MWANAMKE katikati ya Barabara,,kakaa chini tena yupo UCHI WA MNYAMA,,,amekaa mkao wa kunyoosha miguu kuangalia tulipokuwa tunakuja,,Nikasikia KELELE MMOJA,,,wa JAMAA yangu aliyokuwa mbele ananambiya KANYAGA MAFUTA,,USIFUNGE brake TUTAKUFA,,MCHAWI YULE,,,,,jamaa wote waliamka,,,wakati huo nilikuwa nipo SPEED KAMA 120 HIVI...basi nikakanyaga mafuta nikampitia yule MAMA katikati ,,,means NIMEMGONGA,,,lakini sikusikia DALILI YEYOTE YA KUGONGA,,,,muda huo watu wote walikuwa macho,,,,huku tukiwa na Taharuki ya kugonga MTU,,,nilizidisha speeds ya gari hadi NGAMIANI MJINI,kwa kuwa ilikuwa ni USIKU ilibidi kusubiri kukuche, ,ilipofika ASUBUHI nikaanza kuikaguwa GARI,,AJABU haikuonyesha DALILI YEYOTE YA KUGONGA MTU,,aisee tulishangaa sana,,wala hakuna DALILI KWAMBA TULIGONGA MTU PALE,,PIA,,TULISHANGAA SANA,,, KUNA SIKU ingine nipo PEKE YNGU kwenye GARI,,,ilikuwa kama SAA NANE za USIKU ,, Barabara ya MOROGORO maeneo ya MAGARI SABA DARESALAM , ,,njia ilikuwa imetulia sana muda huo,,,NIKIWA SPEEDS PEKE YNGU BARABARANI,,,,,,mbele kidogo nikaona LORI LINAKUJA KWA KASI WRONG SITE,,means limehama UPANDE wake linakuja kwngu,,ikabidi NIHAME UPANDE wa pili KULIPISHA,,,kuangalia kulia naona kuna LORI LINGINE limewasha taa nalo linakuja kwa speed,,Duu,yaani nipo katikati UPANDE wa kushoto kuna LORI LINAKUJA UPANDE WNGU,,na kulia pia KUNA Lori kwa kifupi niliwekwa katikati ya magari mawili yanayokuja mbele yngu kwa KASI KUBWA,,nilihisi mikono imekufa GANZI,,,pale pale nikapata UJASIRI NIKASEMA MIMI hapa SIENDI PEMBENI,,maana huko pembeni kuna MAKORONGO ,, wakati natafakari ZILE LORI hizi hapa karibu yngu,,yaani zinakuja kwa pamoja mbele yangu,,,,zikiwa zimewasha taa fully..basi na Mimi sijuwi nilipata ujasiri GANI,, nikajikuta nimeng'ang'ania steering huku nakanyaga mafuta,,,kufumba na kufumbuwa nikajiona nimepita katikati ya yale malori lakini sijasikia kishindo,,au DALILI ya KUGONGA,,, na sehemu niliyopita katikati YAKE hata BODABODA HAIPITI..NIKAGEUKA NYUMA SIKUONA HATA DALILI YA GARI KUPISHANA NALO,,..HAPO nilikuwa natetemeka na gari ilizima kwa woga,,,,KESHO,,, nilipo muhadithia jamaa yng mmoja akaniuliza HIVI UNAJUWA YALE MARINGI YA SHABA,, WANAYOVAA MADEREVA WA MASAFA MAREFU MKONONI NI YA KAZI GNI? MFANO MADEREVA WA MALORI AU MABASI MAKUBWA YA MIKOANI,,,,WENGI WAO WANA MARINGI YA SHABA MKONONI,, nikamwambiya sijuwi,,akasema WAULIZE,,vinginevyo usipende kutembea usiku wa manane,,especially peke YAKO,, nikakumbuka kuna kitu natakiwa nikifanye kama DEREVA WA USIKU....

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulifanya kitu gani kama dereva wa usiku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiingie upande mbaya wa sharia na hicho kitu.
Uhakiki wake unaanzia Kata, Wilaya (kamati za Ulinzi na Usalama), Mkoa hadi Polisi kwenyewe.
Kama una nia na unasafiri sana, hasa safari za mbali na usiku, hizo ni moja ya sababu ya kuombea silaha.

Siyo mchezo ukisafiri usiku, ingalau una ka ulinzi ka kukupa moyo na ujasiri.
Mimi nina visa vingi tu ila majini sijawahi, narudia sijawahi kuyaona!!
Umeelezea vizuri sana mkuu hizo ndo taratibu za kufuata mpaka unamiliki silaha na sio kila mtu ata afuate taratibu zote akaruhusiwa kununua/kumiliki silaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usipende kuendesha usiku,nitafute mimi twende wote niwe nakupigisha story
iyo safari ya usiku niitolee wapi? labda huku Oman usiku Ndo mda wa kutoka na sijawah kuskia mauzauza, ila kwa afrika cjawahi kua na safari ya usiku
 
Back
Top Bottom