Kwa maelezo haya ya Dudu Baya ukiwa na hela bora ukatibiwe India

Kwa maelezo haya ya Dudu Baya ukiwa na hela bora ukatibiwe India

Hii Bongo wanaweza kumsubiri airport anarudi wakaondoka nae, haieleweki kabisa. Ukiwa tofauti tegemea lolote muda wowote
Sindio that's why nikajenga hiyo hofu , labda apitie Kenya na aishie huko huko serikali yenyewe inapenda kusifiwa sifiwa hii kama wehu hawapendi kusikia negativity zinazo lenga kukosoa utendaji wao dhaifu
 
Hili naona imeelekezewa kwa Mwigulu kwamba badala aongeze mashine za kisasa za MRI tuache kutumia machine used yeye anaenda kupambana na kufukuza wauguzi jambo ambalo lingefanywa na Bodi ya Uuguzi/Chama cha Wauguzi (TANNA) wenyewe, kuna kitu nimechukua na watamuita wakamzibe mdomo
Msipoibua hawezi jua yeye haandai Bajeti za manunuzi Wala specs hiyo ni kazi ya msd na Wizara ya Afya.

Hapo uchunguzi ufanyike Je ni kweli tulitakiwa kununua used au Mpya?

By the way Changamoto ni kawaida hata hicho kidogo kitumike vizuri
 
All government Mchana tu tumetoka kuongelea Issue ya DP world hatujapumzika vizuri dudubaya kaja na hili

Unajifunza Nini kuhusu hii Nchi !?
Huko Nyuma Nilimpoteza Mzee wangu kizembe sana pale Muhimbili Unajua Haya mambo kama haujaexperience utaona Dudu baya kama anaongea shits! Lakini ni ukweli mtupu!
 
Hahaha nimeishia kucheka tu hakuna namna hahaha eti unavalishwa Headphones wewe umekua DJ?
Wakimmaindi Dudubaya tutaenda kufungua kesi mahakamani na ushahidi upo wa kutosha mbwa hao!

Yote aliyoyasema Dudubaya hakuna uongo hata kidogo!

Kuna muda huwa tunaamua kukausha tu lakini pamoja na mikausho tunaumia ndani kwa ndani!

Hii nchi ilipofika inabidi tuseme ukweli kama ni kutuuwa ngoja watuuwe lakini naamini haki haiko mbali!
 
Nchini Tanganyika tunafanyiwa mambo ya kipumbavu sana. Watu wengi wanakufa kwa sababu ya matibabu mabovu kwa kutumia mashine zilizokufa na kutupwa huko Ulaya halafu zikaokotwa na kuletwa Tanganyika kwa ajili ya kuwaua raia wasiokuwa na hatia. Inauma na inahudhunisha sana. Hivi ni lini serikali hii ya wakoloni weusi (CCM) itaanza kujali maisha ya raia.
Cc MamaSamia2025 ChoiceVariable Tlaatlaah Ritz Lucas mwashamba Lucas Mwashambwa
Una recruit Watu wa D 3 unategemea nini?

Nimewahi andika Uzi wa kupinga huu ujinga ila wapuuzi wakanishambulia.

Haya ndio matokeo Sasa.
 
Una recruit Watu wa D 3 unategemea nini?

Nimewahi andika Uzi wa kupinga huu ujinga ila wapuuzi wakanishambulia.

Haya ndio matokeo Sasa.
Hapa nitakupinga maana wale wa Diploma ni training! CBET. Ukijua tofauti kati ya education na training ambayo ni hands-on D nne hazitakusumbua
 
Kuna hospital nilipimwa nikaambiwa nina UTI ni ya serkali dawa nikapewa za ugonjwa huo. Vile nafika home ninywe ile dawa nikaona emexpire miezi2 iliyopita!

Daah nikasita kwa sababu nilipewa dawa zaidi ya 3 nikaziangalia zote zime expire asee isipokuwa panadol tu ndo ilikuwa ina expire mwaka ujao!

Nikafikiria hapa huenda hata siumwi UTI kama dawa tu zime expire vipi vipimo vyao hawa?

Nikaenda hospital ya Agakhan nikacheki kila kitu wakaniambia nina typhoid na minyoo. Nikapewa dawa nikatumia nikapona.

Issue ya dawa nilizipeleka zile dawa kwenye ile hospital aliyenipa akashituka kama kapigwa short ya umeme badae akaanza kuangalia nilichoona karibia dawa zote zilikuwa muda wake umeisha!

Mama anaumwa kisukari tulipewa dawa ambazo angemeza basi angekufa kama sio za kisukari basi pressure ingepanda na kufa.....yani kwa ugonjwa wake hakutakiwa atumie kabisa zile dawa bahati nzuri huwa nina kawaida ya kushare kila aina ya dawa tunayopewa kwa ajiri ya matibabu ya mama hasa nikiwa naye mimi kwenye matibabu.

Ndg yetu mmoja wa damu kwenye group yeye ni Dr akasema hizo dawa msimpe msimpe msimpe kabisa ni hatari na atakufa!

Kwa msisitizo huo nikazipiga picha nikamuuliza chatgpt akanifafanulia kwa uzuri mno.

Nikaona haitoshi kuna Dr mwingine nikamtumia nikimwambia "Mama leo tulienda nae clinic tumepea dawa hizi nikazipiga picha nikamtumia maana anajua ugonjwa wa mama" dk0 akanipigia akaniambi mmeshampa akatumia nikamwambia hapana akasema umsimpe tupa kabisa hizo dawa mama hazimfai!.

Mama huyu huyu alichomwa mwiba akawa na kidonda ila kilikuja kupona kabisa miezi kama 3 pakaanza kuuma hapo alipochomwa ule mwiba tukaenda hospital moja ya serikal tukaambiwa tuende kwenye kipimo kiitwacho Dopler ultra sound (sijui kama nimepatia kwa usahihi)

Tukaenda kupima jamaa akatuambia mguu umeoza ukatwe tu. Mama akagoma mnoo sema sisi tiyri tulikuwa tumekubali kuwa akatwe mguu wake.

Na taratibu zingine zilikuwa zimeanza asee ili tumpeleke tu hata kwa nguvu maana alikuwa halali usiku analia kama mtoto japo alikuwa anasema afe tu na mguu wake kuliko kufa nusu nusu!.

Siku moja akaja jamaa mmoja akatuambia tuende kuna hospital moja hivi tukarudie vipimo hii ni baada tu kama ya siku3 kweli nikampeleka kweli alipopima jamaa akasema ..ule mwiba kipindi unamchoma uligusa kabisa kwenye mfupa na ukaacha kama ka ncha fln hivi hivyo akitembea kanagusa nyama na kuitonesha hivyo mama anunuliwe viatu fulani hivi vyenye sponge akatoa na maelekezo kwa kina sana.

Akatupa na dawa za kusaga ule mfupa nk ......hadi leo hii mama kuhusu hiyo shida kashapona kabisa hasemi mguu tena bado tu kisukari ndo tunapambana nacho.

Nilijiuliza kwa maumivu makubwa sana kuhusu huyu Dr aliyetuambia mguu ukatwe asee siku nikimuona basi tu huwa nawaza mengi sana juu yake asee.

Tuweni makini sana na Dr wa bongo na vifaa vyao. Huu uyuhunda ni wakweli kabisa.
 
Niliwahi kuandikiwa kipimo cha CT Scan pale Bugando ila mashine yao ilikuwa mbovu hivyo nikaambiwa niende Shree Hindu Mandal ipo karibu tu na BMC.

Kufika Hindu Mandal,wahusika wa kitengo hawaelewi kipimo kilichoandikwa!😁


Et "ooh kwani unaumwa nini?"
Mimi:Hamjui kusoma? Nachoumwa ni hicho kwenye karatasi.

Niliporudisha kipimo BMC Dr ananiambia,sicho alichohitaji.
 
Kuwa na vipimo vizuri au vibaya ni moja. Lingine kubwa zaidi ni uwezo wa kusoma hivyo vipimo na. X ray au MRI hio hio akisoma Dr A na akisoma Dr B utapata matibabu tofauti.
Niliwahi ambiwa mimba haikui na hawasikii heartbeat inabidi kusafishwa
Kuna mtu akasema kajaribu hospital nyingine, to make a story short mtoto ana 7yrs sasa hivi,
Hivi kwanini Tanzania tusianze kuwashitsk hawa ma dr uchwara walojazana wanajiita ma specialist 😡
 
Hapa nitakupinga maana wale wa Diploma ni training! CBET. Ukijua tofauti kati ya education na training ambayo ni hands-on D nne hazitakusumbua
Kwa hiyo wewe kwako hiyo training unaona inafaa? Hao ndio wamejaa kwenye maduka ya dawa,wanashiriki oparesheni na wanahudimia wahonjwa kama CO na wanaandika rufaa.

Huo ni upumbavu sawa na wale walimu wa four na Three miaka Ile
 
naona umeeleza mambo useless gentleman na sina muda wa hizo mambo.
mimi na mamalioni ya vijana tumezaliwa Tanzania na kwahivyo ni waTanzania na si vinginevyo.

sina muda kuelezea kitu ambacho sikijui kuhusu eneo la kusadikika
Wewe mpumbavu kumanyoko
 
😄😄😄 Mbona wanajua kuwa bitchuka anaumwa na wamempelekea Hela malizia na hiyo ,

Mimi umenielewa vibaya tu mkuu nilichokuwa Nina maanisha ni kwamba kutokana na kwamba serikali yetu inapenda sifa sifa za uchawa ni wazi hawato furahishwa na maneno ya dudubaya cause Huwa hawapendi kukosolewa
Mkuu tupo pamoja sana. Na wala hiyo niliyotukana siyo wewe, samahani kama umeelewa vinginevyo. Nmesema jinga hilo linatoa fedha za magili wakati vifaa vya matibabu ni vya karne iliyiyopita. Samahani sana.
 
Mkuu tupo pamoja sana. Na wala hiyo niliyotukana siyo wewe, samahani kama umeelewa vinginevyo. Nmesema jinga hilo linatoa fedha za magili wakati vifaa vya matibabu ni vya karne iliyiyopita. Samahani sana.
I appreciate 🙏
 
Huko Nyuma Nilimpoteza Mzee wangu kizembe sana pale Muhimbili Unajua Haya mambo kama haujaexperience utaona Dudu baya kama anaongea shits! Lakini ni ukweli mtupu!
Serikali ya tz na taasisi zake kwa ukiritimba ni 🩲🍑 Hilo lipo wazi
 
Katumia dollar elfu 20 kufuata matibabu India.
Kuna baadhi ya hospital kule India zinahusika na kutoa organs kwa makusudi kuwa na tahadhari sana. Bora Thailand au Turkey tena kwa check up Thailand bei yake ndogo sana $400 unakutana na wataalamu zaidi ya 6 na kufanyiwa CT scan,MRI,full blood check up na mkojo na kinyesi pia wanaangalia.

Matibabu,Hotel na Visa total haifiki hata $10,000
 
Baada ya mke wangu kujifungua mtoto wa pili ziwa moja likaanza kumuuma anaponyonyesha,

Tukaenda kwenye hospitali moja ya serikali,
Wakampima na kumpa dawa azitumie kwa siku 30 kisha turudi tena

Lakini kutokana na maumivu ilibidi mke wangu asitishe kumnyonyesha mtoto, maana pia lile ziwa lilianza kuvimba,
Tukarudi hospitali na kuwaeleza, tukawaambia pia kuwa ziwa lina uvimbe,

Doctor akamcheki tena, akatuuliza bado unanyonyesha? Tukamwambia hapana,
Akasema hiyo ni hali ya kawaida ikiwa utasitisha unyonyeshaji ghafla, akatufafanulia kuwa kuna tezi za maziwa zinaweza kuvimba kwa sababu mtoto hanyonyi, tukapewa dawa na tukaambiwa turudi tena baada ya kumaliza dawa,
Ziwa likazidi kuvimba, tukaenda hospitali binafsi, wakampima upya, wakakata kinyama kwenye ziwa la mke wangu kwa ajili ya vipimo,
Tukaambiwa turudi baada ya wiki mbili,

Tuliporudi tukaambiwa mke wangu ana saratani ya ziwa stage 2 na inaelekea 3, tukaanza matibabu ya saratani haraka, tuliandikiwa tuende KCMC moshi, tukauguza hapo for almost 2 years, akapata nafuu tukarudi nyumbani,

Baada ya muda ikarudi tena, tukarudi kcmc, akatibiwa hapo kwa miezi nane na akafariki hapo , sijui wa kumlaumu hapo, japo moyo wangu haujawahi kupona kabisa, nadhani sekta ya afya kwa nchi hii ina shida kubwa, nakumbuka doctor aliyetupima kwenye hospitali ya serikali tulimkuta tena kwenye hospitali hiyo ya binafsi na akatuhudumia tena.
 
Back
Top Bottom