Nakumbuka ilikuwa Jmosi fulani hivi, dada mmoja ambaye ni rafiki yangu alinipigia simu. J uko wapi? Nikamwambia niko getho. Nimeboreka home bana, tunaweza kutoka? Nikasema poa.
Tukaenda kijiwe fulani hivi, mi nilibeba 50,000.00. Tulikaa kuanzia saa 10 hadi saa 6 usiku. Nilitumia kama 23,000.00 tu, maana situmii wine, sijui bia. Labda Maji. Mwenzangu sasa, anakula hiki anaacha, mara sijui mbona ladha yake, sijuii nini, mara ili Mradi tu anikomoe!
Mara nifungieni niwapelekee watoto, ana watoto wawili, na msichana wake wa kazi + mdogo wake. Bill inakuja napewa Mimi kulipa 129,000.00/=
Nikamwambia mhudumu, naomba unipe ya kwangu kwanza! Akarudi akaniletea 23,000.00, then akampa yule dada 106,000.00. Nikatoa 30,000.00 nikaomba Chenji yangu. Akanipa 7,000.00 yangu nikatulia.
Namwambia lipa twende, anasema hana hela. Nikamwambia naondoka. Mhudumu nafikir mi sidaiwi naondoka. Akasema hudaiwi kaka, nikanyanyuka. Hivi kweli J ndo unaondoka bila kulipa, mi nishalipa wee ndo hujalipa! Lipa twende!
Akainuka akaenda pembeni, akaongea na simu, baada ya maongezi yale akamuuliza mhudumu unaweza kupokea kw M-pesa! Mhudumu sawa tu, ila uweke na ya kutolea. Mhudumu alivosema tu, nimeiona. Akanyanyuka bila kuniaga!
Tuko nae ofisi moja, hadi Leo hata nikimwambia tukanywe, chai naona anachungulia kwenye wallet yake kwanza, ndo ananyanyuka.