Kwa Mara ya Kwanza nimeona Mafanikio ya Serikali kwenye suala la Machinga, Hongera Serikali ya Awamu ya Sita

Wameshindwa kuwatoa machangudoa na wala shisha ambao ni wahalifu wataweza kuwatoa machinga ambao hawamwibii mtu yoyote?

Tatizo viongozi wetu huwa hawajifunzi kutokana na historia ni suala la muda tu ngoja hela ziwaishie.
Hivi shisha ni uhalifu? Au ni tafsir yako ya kisukuma tuu
 
Kwa nini unasema ivyo Mkuu?

..hata mimi nina wasiwasi kama aliokua nao Toosweet.

..Kuwapanga wamachinga ni jambo zuri na linapaswa kupongezwa.

..Wasiwasi wangu ni kwamba Wamachinga wanaongezeka kwa kasi kuliko uwezo wa serikali kuwapanga.

..Tunatakiwa tujiulize kwanini Wamachinga wanaongezeka mwaka hadi mwaka, halafu tuje na mbinu za kudhibiti sababu zinazopelekea Wamachinga kuongezeka.

..Kwanini Watz wanaoingia ktk AJIRA RASMI ZA KUDUMU ni wachache kuliko AJIRA ZISIZO RASMI?

..Naamini hilo ndilo swali ambalo walioko ktk Serikali, Vyama vya siasa, Think Tanks, Asasi za Kiraia, wanatakiwa kulipatia majibu.

..Je, zoezi lililofanyika ni la kudumu, au ni la muda mfupi? Je, ndio JAWABU la tatizo la ongezeko la Wamachinga?
 
Jipeni muda kibanga ampiga mkoloni. Hongereni kwa mafanikio
 
Mtu kula yake hajui itakuaje,unamuambia habari za usafi?
Machinga ni kama result tu,huku sababu kubwa ikiwa ni ujinga na umasikini uliotopea.....
 
Nilikuwa napata shida sana nilivyokuwa naiona Dar kila siku inazidi kuwa chafu na ya hovyo.

Nilichoka mwaka jana nilipita Mlimani City nikakuta vibanda vya watu wanakaanga na kupika vyakula nje ya Mlimani City. Niliumia sana
Uumie watu kujitafutia riziki nje ya mlimani city,kwa nini usiumie ndugu zako kijijini kuzaana ovyo huku hawana kipato chochote
 
Hivi Machinga walikuwa wanajisaidia wapi?
 
Hangaya wanamchukulia Poa sana Ila amini nakwambia huyu mama yuko vizuri! Hana mbwembwe ila show zake ni mita 100
Inaonekana viongozi wa mikoa wamepewa maagizo,maana Makala kasema Machinga endapo itafika tarehe 30 halafu wakarudi katika maeneo yao basi ye atakuwa kaehindwa kazi.Kwa sentensi nawashauri waleachinga wabishi wajiondokee wenyewe wasishupaze shingo.Muda huu watumie kutafuta sehemu nyingine za fursa
 
Nenda soko la Karume ( Mchikichini ) kila mmoja anajifanya machinga ila watu wana mitaji mpaka ya 200M hapo.

Na ndio maana hata kipindi kile soko limeungua walirudi kwa kasi kama hakikutokea kitu.
Serikali ya Samia ni serikali ya watoto wa mjini,hiyo michezo yote naamni Samia anaijua.Na serikali yake haina mchezo na kodi.Soon atawafikia,ngoja aweke sawa hili la wamachinga.In short mama anataka kila mtu alipe Kodi
 
Ametengeneza tatizo jipya. Give it one month all jobless machinga will raise in a survival style .
 
Kubali kataa Mwendazake aliharibu.Kusema katika Machinga wapo watu wa system Hilo sio la kubisha.
 
Mnamlaumu tu Magufuli kwenye hili. Machinga na mauchafu yao wamekuwepo hata kabla ya Magufuli kuwa Rais. Labda useme ruhusa yake ilifanya hali kuwa mbaya zaidi ila tatizo tayari lilikuwepo na tayari lilikuwa kubwa.
Magufuli hawezi kwepa lawama.Magufuli kachangia sana uchafu huu
 
Hivi mandate ya kusema Kwa kuwa Rais ni nwanamke mnaitoa wapi .to be honest hii kauli binafsi inanikera na inanikera hata pale inaposenwa na mama mwenyewe it's disgusting to hear such statement .
Alaumiwe aliyekuza utamaduni kuwa, katika wazazi wawili, mtoto abebe jina la mwenye uume hata kama mwenye uume ni dhaifu na hana mchango katika malezi na mafanikio ya mtoto. Sisi wenye uume tunatembelea hiyo nyota na hatutaki ife.
 
Hongera kwa kazi nzuri, miji kwa kweli ilikuwa michafu, nakumbuka kuna wakati Makonda alijitahidi kuisafisha kariakoo lakini jiwe akaamuru waachwe wajinafasi, kwa hili jiwe was absolutely wrong.

Ila kumbuka, umetatua tatizo kubwa...umeibua tatizo kubwa, the jobless.. the kipatoless, soon ukabaji, udokozi na wizi utaanza. Unless measures za uhakika zichukuliwe kunusuru hii hali.
 
Ametengeneza tatizo jipya. Give it one month all jobless machinga will raise in a survival style .
tatizo huwa halishi kwa kuacha tatizo liendelee.

Nimatumaini kuwa tatizo jipya unalolitabiri lipatapata utatuzi

Tatizo la njaa linatatuliwa na kulima

Ukilima unapata tatizo la sugu viganjani

Kuna namna ya kutatua tatizo la sugu na si kwa kuacha kulima.

Maisha ni matatizo yanayotafutiwa utatuzi kila siku.
 
Tusirudie kumpa nchi tena mfuga mifugo mshamba mtu mwenye nongwa. Magufuli kaenda Na aoze kabisa. Ila kuna Antipas Lissu huyo ni wa hovyo zaidi ya Magufuli anaweza ingia Na machungu yake akaruhusu biashara ya umalaya mpaka misikitini Na makanisani.
Tusifanye hilo kosa Kwa watu hao. Lissu ni HOVYO kuliko Magufuli.
Povu [emoji3475] [emoji3476] RUKSAAAA
 
Umenena vyema kabisa!

Usafi uwe utamaduni wetu na kwa kuwa saivi tumeona inawezekana miji yetu kuwa safi serikali haina budi kuwa strict hasa
Mi nafikiri hata somo la usafi na haiba liludishwe mashuleni ili kujenga tabia ya watu kupenda usafi, tabia ikijengwa angali watu wana umri mdogo hakika itaendelea. Tuna barabara zinajengwa kwa gharama kubwa sana lakini unakuta mitaro yake imegeuzwa kuwa majalala, mitaani ni wachache sana wanaojali usafi. Hili tatizo ni zaidi ya kuweka sheria, kuna ustaarabu na tabia ambayo kama taifa inabidi tuanzie kwenye msingi wa malezi ya watoto wadogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…