Mnyenz
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 2,933
- 8,112
Mimi sio muumini wa sheria mkononi lakini naamini kwamba tukijaribu ku apply sheria mkononi itasaidia ama kukomesha kabisa hili jambo la kutekana.
kipindi cha nyuma kidogo suala la wizi liliwahi kushamiri sana hasa dar, watu walikua wanaibiwa mchana kweupeee(unaona mtu anakwapuliwa simu,cheni yake na hakuna msaada wowote anaoupata)
Polisi walikuwepo lakini walishindwa kuzuia kabisa matendo hayo kwa asilimia mia, Lilipokuja suala la wananchi kuchukua sheria mkononi matukio ya wizi wa aina hii yalipungua(japo kuna waliowahi kupata madhara ya sheria mkononi na hawakuwa watuhumiwa)
Kipindi bodq zinaingia katika mfumo wa kubeba abiria, boda wengi(sio wote) walikua wanapata ajari kutokana na uzembe wa madereva wa magari, hawa jamaa wa boda sijui walikaaga kikao wapi wakaja na mbinu ya sheria mkononi, matokeo yako madereva wa magari wamekua makini japo si asilimia mia
Nini kifanyike wa hawa wanaoteka watu hovyo???
Tuanze kutembea na filimbi shingoni(waulize askari wa kenya wanaijua nguvu ya filimbi kipindi cha maandamano) ukiona watu wawili au watatu wamekuzuia, wanakulazimisha sijui upande kwenye gari, chomoa filimbi yako uipulize kwa nguvu zoooote ili kila mtu karibu asikie, na atakaesikia kelele za filimbi hana budi kusogea eneo la tukio.
Watu wakishajazana, tuanze kuwahoji hao askari(sio kuwazuia kufanya kazi) kwamba huyu jamaa mnamkamata sawa lakini kutokana na mazingira ya kutekana, basi wapigwe picha askari wakiwa na mtuhumiwa na waseme wanampeleka kituo gani.
Wakigoma kupiga picha basi wapigwe picha kwa lazima ili ikitokea tatizo lolote tuwaanike mtandaoni kuwa hawa ndio waliomteka fulani.
Katika hili tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja sababu leo akitekwa fulani huwezi jua wewe zamu yako lini. Kipindi Roma anatekwa, sidhani kama Sativa alijaribu hata kuwaza kuna siku atakuja kutekwa yeye, lakini na yeye amekuja kutekwa hivyo hakuna alie salama, leo kwangu kesho kwako