Kwa milioni 4 ninunue gari gani iliyotumika?

Itoshe kusema kuwa ww n maskini wa kifikra.
Af em jaribu kuondoa lile wazo la kuwa hata uwekeze utakufa na kuviacha kama ulivyomtolea mfano Mengi....
Jiulize kwanza Mengi amezifaidi vp mali alizojilimbikizia kabla ya umauti wake.
What if asingewekeza akiwa na mawazo hasi kama yako.....
Sio mengi peke yake..... Angalia watu wengine waliofanikiwa kimaisha. Waliwekeza kwa kile kidogo walichokuwa nacho, kikawa kikubwa and wakaishi maisha wanayotaka.

Turud kwa mwenye huu uzi....
Kipato chake per month n laki 6 hadi 8, then ako na 4 millions kama bajeti ya gari.....
Wengi mtapingana na mimi lkn kuna jambo haliko sawa.

Hapa ntabishana na waajiriwa serikalini, lkn kwa mjasiriamali or mfanyabiashara anaelewa nnachozungumzia hapa n nn.

Mfano rahisi ni huu hapa....
Diamond platinumz alikuwa na uwezo wa kumiliki Rolls Loyc hata kabla ya Ginimbi...
Badala yake pesa hio alitumia kutengeneza mifumo mbalimbali itakayompa pesa zaidi mbali na sanaa anayoifanya. Pesa imezaa na amemiliki ndiga ya gharama kiasi kile. Wakati huo ashaitengenezea pesa mikondo kadhaa.

Then simpangii mtu namna ya kuishi, ila nmefanya kumshauri tu.

polokwane ungekuwa ww n MO ungeshanunua ndege yako binafsi kwa mawazo yako ya "kwann niteseke na foleni wakati pesa yakununua plane ninayo".

Soma reply ya igogondwa na Rusumo one #78 na #79 respectivelly.

Amka polokwane

Imagine " Una gari af kipato chako n laki nane kwa mwezi" inasound vp hio...

Unataka kuonekana tajiri, badala ya kuwa tajiri.
 
Achana na mawazo ya kimaskini kama nafasi ya kufanya jambo ipo fanya achana na fikra zako za kimaskini ni hivyo tu.
 
Ila kwa pesa yako kupata gari ambayo bado nzima sana passo ni recomended, ukichukua ingine utapata ilochoka sana
 
Mkuu cheki na vitz zile model ya zamani unapata kwa hela hiyo lakini pia mafuta hakata kusumbua.

Kwa hela hiyo unaweza kupata pia mark ii grande,verosa ila hizi uwe na bajeti nzuri ya mafuta au huna mizunguko mingi kwa siku.

Achukue vitz old model au passo piston 4
 

Kuna gari zinapigwa minada na watu wa mikopo
 
Gari Ni basic needs sio luxury mbona mna complicate Sana mambo...

Yani Gari la dola 1800 ndio linakutoa povu lote hilo
 
Aisee majibu yako yanaweza kuwa sahihi.. Ila hapa sio sehemu yake.. Swali limeulizwa gari la kununua kwa bajeti fulani.. Wewe unaelezea kipato na gari.. Nashauri ufungue uzi wa Kipato vs Umiliki wa gari.. Then tutakuja huko huko kukufundisha pia..!
 
Ngoja nisome comments, kwa uchache tafuta network ya wadada wenye ist namba C Pia check na watoto wa kihindi hutojuta 4m kuna watu wanasubiria kwa hamu No. E utapata gari nzuri sana ongeza 1M utapata gari nzuri sana, Alteza pia zipo kwa hio bei. Ogopa madalali utalia
 
nunua ist. roho ya paka.
 
Mwenye masikio na asikie
 
Kuielewa huu ushauri wa jamaa lazima uwe na akili kubwa, yaani kipato cha laki nane unataka ununue gari, tena kwa milioni 4?? Vijana mna tabu sana aisee
Mkuu wewe ulitaka awe na kipato gani ndio anunue gari?
Ushauri wako mkuu.
 
Kwenye hiyo Milioni 4 weka na pesa ya notebook na peni ya kuandikia namba za simu za mafundi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…