Kwa mjazano huu wa ndugu, sahau kabisa kuitwa tajiri

Wewe sio Tu umetoa elimu Bali umetoa Msaada Kwa vijana wa sikuhizi wasiojua kitu na wenye Akili mgando...Hii comment yako ni zaidi ya darasa
 
Ni kweli life lnamna hiyo linarrudisha nyuma maendeleo ama linakufamya maendeleo yagande hapo hapo, mpaka unakufa unakufa na kijumba chako kimoja,

Wengine kusaidia ni sehemu ya maisha yetu, tunajisikia faraja tukishare hiko kidogo chetu, tumezaliwa na kukulia katika familia za namna hiyo, home mpo 15, wazaliwa ni wachache kuliko ndugu.
Mara hawa watoto wa mamkubwa, yupo kijijini huko life limemchakaza, bimkubwa anachukua wawili anawasomesha, hawa walifiwa na wazazi wao, sijui huyu hivi.. yaani familia inakuwa ya kutosha na fresh, watu mnainjoi.
Kuna faida gani mie lufa na kuacha mijengo mingi, ikiwa nilishimdwq kulea mtoto wa marehemu dada/kaka,
Nilishindwq msaidia mtoto wa mjomba wangu ambae mzee wake life lilimgomea
Nilishindwa msaidia kaka yangu, alipokwama?

Japo hii kwa kadri miaka inavyozidi kwenda maisha yanaongezeka ugumu, huko mbele ya safari itawawia watu ugumu sana kuishi maisha ya namna hii.. ugumu wa maisha, tabia za kimagharibi, upendo unafifia, haya yatachangia maishavya hivi kupotea
 
Shemeji ndo umekuja kunianika JF....
 
Ukiona unamiliki nyumba na gari ushakuwa tajiri unataka utajiri gani mwingine
 
Mimi na ndugu zangu wengi tuliokuwa wanafunzi enzi hizo tumepiga sana kambi kwa Baba mdogo hasa wakati wa likizo... yule mzee kawapa hifadhi watu wengi sana nyumbani kwake. Cha kushangaza leo hii yeye ni tajiri mkubwa ila wale wabinafsi wameendelea kuwa vilevile miaka yote. Hata kama huwezi kuwapa malazi nyumbani kwako basi wasaidia huko waliko.... hamuoni wanasiasa wanavyobeba ndugu zao?
 
alaf wengi wao wakiume wanaingia gym kubeba vyuma,na wanawake wanaanza jogging,,mchele kwa siku kilo 15,,nyama kilo 10!!
 
We Huna hela,
Chakula kitu gani ukiwa nazo,
Wali, Ugali, nyama, maharage ushindwe kufanya biashara.
We utakua mbwiga tu.
 
Na wao watajihisi ni part ya familia na wanahusika kwenye uzalishaji utabaini na wanaofaa kuaminika kwenye miradi yako mingine serious.
Mtu mwenye muda usio na matumizi hafukuzwi unatafuta matumizi ya muda wake tu unufaike nao.
 
Mara nyingi wanajaaga wa upande wa mume ..wageni 5 mpaka 6 na wanakaa si chini ya miezi 6 ila upande wa mke akiomba hata ndugu yake kuja kusalimia baba mjengo anatia ngumu ila ndugu zake ruksa..baadhi ya wanaume wabinafsi sana
 
Unatakiwa uwe muwazi, uwaambie sitaki kuwaona kwangu, kwanini uteseke kupitia Mali ulizochuma kwa jasho lako
 
Utajiri ni kuwahudumia ndugu wanaokutegemea hasa kuwapatia mahitaji muhimu. Huo ndyo utajiri,.. wewe ni utajiri upi unaozungumzia? wa kutangazwa?
 
AWafungulie hata genge la chakula wanaenda kumuuzia ,waamke saa 11/10 asubuhi wakapike chapati vitumbua nk.
Una akili kubwa mno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…