Kwa mshahara wa Tsh. 765,000/= nikizama benki naweza kopesheka kiasi gani?

daah umeponda ila umenipa fact
 
ushauri mzuri mkuu
 
Inaonekana iyo business unayofanya inakulipa.
 
Haya muelekeze time management ili aweze kubalansi kazi yake na kuisimamia biashara anayoiwaza.

Pili umkumbushe biashara haianzishwi kwa pesa ya mkopo.

Tatu mwambie ili isimame hiyo biashara inahitaji muda na mtaji.
Kimoja kikikosekana itaanguka.

Tano mpe kabisa takwimu za biashara mpya zinazoanzishwa, ni asilimia 5 tu ndio zinadumu.

Hapo hujaangalia kama zinazalisha faida au lah!

La sita na mwisho hatujajua kazi ya anayofanya

La saba je ana elimu ya fedha, kama Hana mwambie aangalie ambacho ni rahisi kukimanage.
 
Nenda Bayport mkuu,ili uone rsha ya mkopo.
Kwa maana umekuja kututambia huku kuwa unamshahara.
Kawashirikishe ndugu zako Kwanza mkuu.
Ila baadae usije Anza kutulilia humu na kuwatupia lawama Serikali.
 
Mnaomshauri akope 25M
Mwambieni pia atalipa 47,318,177.1(47M),
Mwambieni katika hio 25M cash atakayopata ni 22.5M.
Mwambieni atakatwa 438,131.27 kila mwezi kwa miaka 9.
Mwambieni jumla ya riba atakayolipa ni
22,318,177.1.
Mwambie katika 47M atakayolipa,
Yeye atachukua 22.2M na 24.5M anawaachia Bank.
Mwambieni ni sawa kutoa 226,851 kila mwezi kwa miaka 9 kulipa riba tuu.
Mwambie hio pesa Akiamua kujitunzia mwenyewe angetumia miaka 4 kuipata, huku ⅓ ikibaki pale pale.

Akili Kukichwa.
 
Fact
 
Asikope kwasababu ana idea ya biashara .....hapa ndipo watu wengi wanapofeli katika mikopo.Kopa ili kuikuza au kuitanua biashara ambayo tayari unaendelea kuifanya, inakulipa vizuri na una uwezo wa kuzikabili changamoto zake.

Unakopa ili kuongeza uzalishaji au uingizaji wa bidhaa sokoni. Usikope ili kuanzisha biashara utakuja kukutwa na kitu kizito hutoamini.

Mfano labda ulikuwa unaingiza mzigo mchache unauzika kwa wakati na bado kuna demand kubwa ya uhitaji wa bidhaa yako kwa wateja. Hapa unaweza kukopa ili uwe na uwezo wa kuingiza mzigo mkubwa zaidi ili uongeze faida pia.

Ukifanya hivyo fasta utaweza kuulipa mkopo na utaona manufaa ya mkopo. Mwisho kabisa nakushauri uepukane na mikopo yenye Riba.

Kumbuka RIBA sio faida. Riba ni laana . Wengi wamefeli katika biashara kutokana na kujihusisha na mikopo yenye riba.
 
Ukitaka kufanya jambo lako sasa hivi, usiulize ushauri mitandaoni. Humu kuna watu wa kila aina, wengine humu watakwambia mshahara wa million 1 ni mdogo sana hautoshi kitu kumbe hata kazi hana.

Tafuta ushauri sehemu sahihi na kwa watu sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…