Kwa mtaji wa milioni 12, nifungue hardware, nafaka au phone and accessories?

mkuu hebu chomoa kwanza hata 5m ukatumie... maendo ya starehe ndipo utakapopata idea nzuri za biashara gani ufanye
 
Yeah wewe unapajua kigoma, mji mgumu sana na ushirikina ni wakutisha, kati ya 100%, 99% wanaupractise uchawi nimeona kabisa mwenyewe, na wakati natafuta information mtu mmoja alinambia inabidi nijiweke vizuri pia kwenye hayo mambo, ndio wazo la nafaka likaingiaa maana nafaka ni need, kila mtu anataka ukiwa na nafaka nzuri plus ubora bei chini nauza tu.
 
Nafaka haiwezi kukuangusha ila Faida ndogo sana,Wanasema biashara ambayo inatoka sana,Haina Faida kubwa...kwa vile huko tumeona watu wagumu sana,hujawahi kupata wazo la Kutoa huko Vitu kuleta Dar??Ushapata ABC za Tangawizi??
 
Nafaka haiwezi kukuangusha ila Faida ndogo sana,Wanasema biashara ambayo inatoka sana,Haina Faida kubwa...kwa vile huko tumeona watu wagumu sana,hujawahi kupata wazo la Kutoa huko Vitu kuleta Dar??Ushapata ABC za Tangawizi??
Tangawizi wanalima wilaya Moja inaitwa buhigwe, sijawahi kukaa kuwaza kuhusu tangawizi, maana ni biashara itakayonifanya nitafute mzigo na gari na kusafirisha kuja huko dar, mwanza n.k...
Ulivyosema ni ukweli, Mchele au nafaka kwa jumla inatoka sana lakini faida kidogo lakini hizo biashara zingine ukiupata mzunguko unatoa faster sema changamoto kama ulivyosema huku Watu wanaamini katika ushirikina sana.
 
Tugusie nilichokwambia kwanza,kuhusu kuuza HUDUMA,wewe SI mwalimu,fikiria kitu kama Shule ya chekechea,kitu gani umeona kwenye miji mikubwa kipo but kwa Kigoma Bado hakijafika au watu Bado hawajaanza kuona kama kitu Cha maana?? Nail shop??duka la ice cream??
 
Nakazia hapa biashara yoyote au jambo au kitu au shughuli ya kuingiza kipato inahitaji usimamizi wa karibu Sana wa muhusika

Dunia ya sasahivi imekosa uaminifu kabisa na biashara au shughuli yoyote inahitaji uaminifu kwa mara ya Kwanza inapoanza

Risk taker ndo huwa wanafanikiwa Kwaiyo akitaka kufanikiwa ni lazima achukue maamuzi magumu otherwise atakua wa kawaida Sana
 
Biashara ya hardware ina faida lakini inahitaji mtaji mkubwa angalau milioni 30 ili lionekane vizuri,biashara ya mazao ina faida lakini inahitaji muda mwingi sana wa kusafiri kwenda mashambani ndanindani huko ni ngumu uwe unaenda kazini kila siku halafu upate muda wa kuingia mashambani inahitaji ukisafiri kwenda huko angalau ukae wiki moja kuyasoma mazingira,kukagua mzigo na kuikusanya ili kuisogeza maeneo ya mjini,hata kama utawatuma watu au mawakala huwezi ukawaamini moja kwa moja uwepo wako bado ni muhimu sana.
Na ukija kwenye biashara ya vifaa vya simu inamfaa muajiriwa ni rahisi kila siku jioni au mchana kwenda kuikagua akimaliza kazi lakini faida zake ni ndogondogo na inachukua muda mrefu sana kuurudisha mtaji au labda kama lengo lake ni kupata hela ndogondogo tu za kula.
Ndio maana kuna wadau kama wawili kule mwanzoni walicomment kwamba biashara nzuri ni zile ambazo unabuni huduma fulani ya kipekee ambayo haifanywi na mtu mwingine yeyote katika eneo lako hapo ndipo utaona mafanikio ya haraka ila sio hizi za kuigana,mimi niliwaelewa sana pointi zao.
 
Yeah, nilipokua dsm niliona watu wakiwa na Banda special kwa ajili ya kuuzia juice (kama juice shop flani),maziwa n.k huku kigoma hakuna.
 
Yeah ni kweli mzee, hata Forest Hill amegusia hapo, lakini sidhani kama Kuna biashara mpya, biashara nyingi zipo tayari Mimi nadhani kikubwa ni kujua unataka uifanyaje
 
Nafaka haiwezi kukuangusha ila Faida ndogo sana,Wanasema biashara ambayo inatoka sana,Haina Faida kubwa...kwa vile huko tumeona watu wagumu sana,hujawahi kupata wazo la Kutoa huko Vitu kuleta Dar??Ushapata ABC za Tangawizi??

Nafaka Faida ndogo, pia kuna swala moja watu wenye mitaji mikubwa huwezi kushinda nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…