Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza ninaomba ushauri, nina Tsh laki nne je naweza fanya biashara gani

Msaada plz
 
Uza mkaa nunua viroba vya mkaa kwa bei ya jumla unaviuza kwa reja reja au kuvifunga kwenye vifuko
Au fungua genge la mboga mboga
 
Chukua freezer ya laki saba kodi kibanda cha kuiweka tafuta vijana kama watatu ay wanne wawe wanafunga maji ya viroba wanaenda kutembeza mbagala huko kwa kila kijana kwa siku anarudi na elfu kumi na tano hapo utakuwa unakula bingo tu
 
Habari members. Unamshauri biashara gani mtu mwenye mtaji wa 5000?

"Ondoa neno haiwezekani kwenye fikra yako na maneno yako yote unayoongea"
Inategemea upo eneo gani Mkuu hii biashara inawezekana kama utakuwa na utayari.

Fanya ivi unanunua matunda mfano parachichi au ndizi hata za buku nne unajenga mahusiano mazuri na mama antilie mnafanya kuwekana sawa kwa upande wa faida mfano ndizi mbili umejumua kwa shilingi 50/= basi mtauza kwa 100/= wakati huo 25/= ya kwako na 25/= ya mama antilie. Vivyo hivyo kwa parachichi umejumua moja kwa 200/= mtauza kwa 500 halafu faida mnagawana 150/= ya kwako na 150/= ya mama ntilie. Kaa sasa mwenyew upige hesabu utapata kiasi gani hapo

Ukiwa kwenye maeneo yenye upatikanaji kwa wingi wa bidhaa hii utapata faida nzuri sana Mkuu msingi uwe na utayari kupiga kazi aise
 
nimekaa na kujishauri kuhusu swala la ujasiriamali nimewaza sana lakini nimeshindwa pata jibu ni biashara gani naweza fanya nanina mtaji wa laki 5
 
Ndugu yangu kama uwezo unao (una wazazi wa kugharamia shule yako)...tumia muda huu kujiimarisha ki elimu kwanza.

Cz baadae amini nakuambia hutoweza kutokana na majukumu and the like.

Thank Me Later.
 
Ndugu yangu kama uwezo unao (una wazazi wa kugharamia shule yako)...tumia muda huu kujiimarisha ki elimu kwanza.

Cz baadae amini nakuambia hutoweza kutokana na majukumu and the like.

Thank Me Later.
Sasa laki 5 ndio itamtosha kulipia ada,nauli na chakula mwaka mzima wa masomo?
Au umemaanisha ajiendeleze elimu gani?
 
Nunua mashine ya cherehani 150,000

Nenda machinga complex kodisha kizimba kwa mwezi 20,000

Anza kushona nguo kwa pesa zilizobakia kisha nenda ukauze madukani kariakoo na posta na mnazi mmoja

NB: Ubunifu ni muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…