Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Duu buku kwasiku....kanunue mbegu za bamia pakiti 1000/= ukinunua pakiti hata 10 bonge la bustani unavuna bamia kila Week kwa ratio ya mpishano kwasiku unapata hadi 5000/= wewe na kumwagilia tu hasubui jioni.

Mtaji 10,000/= tu kama kwenu kuna eneo.
 
Habari za kazi wa kuu naomba kuuliza kwa mtaji wa laki moja naweza kufanya biashara gani hapa Moshi town na viunga vyake nikawa napata pesa ya kula .

Maana kuna shughuli nyingne nafanya ila hainibani sana kufanya mishe zangu vyingne msaada wa mawazo.
 
Tegesha kama machinga, tafuta bidhaa ambayo inatoka sana na kwa haraka kisha uwe unaiuza, utaangalia na ulipo nn kinatoka
 
Nina laki mbili,nataka kufanya biashara ya mtaji mdogo usiozidi ela hiyo kwa kuanzia,isiwe ya usimamizi wa moja kwa moja.Naombeni mawazo yenu.
 
Kama laki mbili zinakushinda kusimamia iweje maelfu kwa maelfu..

Ngoja waje mkuu watakusaidia ..mimi naanza na hii ya genge la viungo, mboga mboga
 
Nasubiri jibu
Upo WAP
Unafanya nini

Una experience/elimu juu ya nini?
Nipo Dar,mwajiriwa,nimemaliza chuo uhasibu.Kuliko kusubiri mwisho wa mwezi peke yake nataka kujiongezea kipato,siwezi kusubiria mamilioni nataka kuanza na kidogo nilichonacho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…