Habari wana jf, nimejaribu kukaa chini na kuja na Idea hii ya biashara ambayo tunaweza kuanza na mtaji wa laki moja au hata laki moja na nusu. Biashara yenyewe ni biashara ya kuuza matunda mchanganyiko kwa ku park kwenye vi parkage spesho
Mahitaji:
Matunda kama, maembe, papai, ndizi tango,zabibu,parachichi na kadhalika. Na hapa kwenye matunda nadhani ukiwa na elfu 20 tu itakuwa inatosha kabisa.
Na kingine ni parking za kuweka nadhani bei zake hazifiki hata elfu 50
Mahali nnapopendekeza uuze hiyo biashara yako ni Ubungo bus terminal.
Na bei ya matunda yako itakuwa ni shillingi elfu moja kila bando moja.
Njia ya uuzaji tafuta vijana wawili au watatu itategemea na uzalishaji wako unawapa mzigo ikiwezekena kila mmoja anatakiwa awe na mzigo wa bando mia za matunda jumla utakuwa na bando mia tatu za matunda... mtu mmoja kwa kiwango cha kukadilia auze pisi 60 ambayo itakuwa ni shillingi elfu 60 ambapo hapo kijana utamlipa shillingi elfu 10 tu kwa siku maana yake utabakiwa na elfu 50 ukitowa ghalama zote letsay utabakiwa na elfu 30 kwa kila mmoja maana yake kwa watatu ni elfu 90 kwa siku kwa siku 15 ni shillingi 1,350,000/= nadhani hiyo si faida ndogo ukilinganisha na mtaji wako utakaoanza nao.
Nakaribisha maoni yenu pamoja na michango na kujazia nyama
Llio 002