Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Habari! Naomba kuuliza
Ni nani kati yenu amewahi kusikia fursa ya ufugaji wa Wadudu Mende kama chakula cha mifugo yani kuku
Mwenye uelewa wa hili swala naomba aeleze kwa mapana zaidi, kwa kuanzia
1 mtaji
2 mbegu
3 uzalishaji
4 uvunaji
5 changamoto
6 soko lake

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimewahi kusikia fursa ya hao mende nikipewa namba ya simu nikawasiliana nao, kifupi ni kwamba ukitaka unapewa mafunzo jinsi ya kuwafuga ila kuna malipo kwa hayo mafinzo, na kama hutaki ni mafunzo pia sio shida wewe fuga mende wao wananunua kilo 5000, kama unataka mawasiliano yao nina namba yao ya simu wanapatikana Dar pale external ubungo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pisi kali naomba iyo location ya nguo za 50k adi 100k ilipo
Kwenye comment yangu nimesema “kama vya kimasai” sijasema vya kimasai

Na vya kimasai vipo vya bei hiyo ila havina shanga, vya shanga ni 6,500

Usiwe mwepesi kubisha kama hujawahi kufanya hicho kitu, mm nimeuza viatu vya kimasai nilikua navifata hadi Boda ya tarakea huko nikikuambia bei utabisha[emoji28][emoji28]

Nguo za laki3 kuna machimbo unazipata kwa 50k-100k tu

Bila samahani’ usijali mwaego
 
Mimi Nina mtaji wa laki 5 naomba mwenye wazo LA biashara akanipa ABC's ili angalau kwa siku niweze kuingiza elfu 10 au 15 hasa maeneo yafutayo.
1.Makambako
2.Njombe
3.Ruvuma hasa songea na tunduru.

Ushauri wako ni muhimu sana ila naomba kejeli tuache ,am serious maana mawazo ya wengi ni bora kuliko pekee yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu!

Ni mara nyingi sana vijana tumekuwa tukihangaika huku na kule kutafuta kipato ila wengi wetu tumekuwa tukiambulia kusema hatuna mitaji ya kutosha sasa leo nakuletea hizi biashara baada ya kufanya utafiti wa kina

1. Kuuza dagaa wabichi
Hii biashara inawahusu watu waishio kando kando ya ziwa hasa ziwa victoria. Kwa wenyeji wa Mwanza natambua wanaelewa vizuri hii kitu. Katika biashara hii unachohitaji ni tenga lako na mtaji usiozidi 50,000 hata kama huna baiskel utakodi kwa siku utalipia 1000 tu. Haina changamoto sanaa tofauti na aibu hasa kama wewe ni msomi itakupa shida mpaka kuizoea

2. Kukaanga samaki na kuwauza
Ni biashara nyingine ambayo inaleta pesa mingi sana zaidi ya maelezo. Hapa mtaji hauzidi 100,000 lkn utapata faida zaidi 15000 kwa siku. Kijana changamkia fursa

3. Kutembeza maziwa maeneo ya mjini.
Aisee kijana hii ni zaidi ya biashara niliwahi kuifanya hapa Mwanza lkn niliacha coz nilienda masomoni liporudi nikawa naona aibu tena hapo ndipo huwa naamini kuwa Elimu ni kifungo cha Maisha

4. Kulangua mboga mboga na kwenda kuuza jumla sokoni pale saba saba.


Kwa leo inatoshaa karibuni kwa mapovu na ushaurii
 
Back
Top Bottom