Habari
Members najua humu kuna watu wa aina nyingi, waliobobea katika biashara, na watu wa sekta nyingine. Naomba kusaidiwa kujua BIASHARA ninayoweza kufanya kwa mtaji wa laki tano tu, ila hiyo biashara iwe na uwezo wa kunipatia faida ya 10000 tu kwa siku!! Hiyo faida ni baada ya kutoa malipo ya kijana msimamizi.
*Nataka biashara ambayo naweza muachia kijana akafanya wakati na mimi naendelea na shughuli nyingine
* biashara ambayo haina utata sana katika usimamizi
* biashara ambayo ni ya kudumu,kwa maana ya kwamba inakuwa kama investment flani hivi inayoweza kukaa miaka kadhaa
* shida yangu ni uhakika wa elfu kumi tu kwa siku
* eneo itakapofanyika ni kati ya MWANZA au DAR
Asanteni!